Mi pass yangu nimechukulia mkoani wala haikuwa nanshida yoyote.Kama kawaida watu wa kanda (maalum) ya ziwa huwa tunasahau hata salamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye mada,
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu vitabu vya hati ya kusafiria, kila mtu anasema lake leo nimekosa kazi nikaenda mapema kujionea makao makuu ya uhamiaji kurasini Dar es salaam, nilikaa kwa masaa mawili nikagundua yafuatayo vile vibanda vya kutoa copy pale nje ni biashara cover up kiuhalisia wale bila kumung'unya maneno nawaita mawakala wa pass port, niliingia duka la kwanza kutoa copy nikakuta kuna watu kadhaa nao wana subiri huduma hiyo yule dada mtoa copy anaongea na simu nanukuu "unataka express ama ya kawaida, kama ni express ni laki tatu inatoka ndani ya wiki" mwisho wa kunukuu yaani alikuwa anaongea bila uwoga na kwa ujasiri ukiangalia dukani humo kuna watu wengi kila mmoja anakukaribisha tena wababa wazima nikabahatika kumuona mmoja anamuhuri wa mwanasheria tayari kwa kutengeneza affidavity sh 15000.
Nikatoka nikaenda duka la pili baada ya kuona pale kuna msururu wa watu yule dada alikuwa ananitolea copy huku ameweka simu masikioni naye anaongea na mtu "ya wiki ni laki 3, wiki mbili laki 2 ya kawaida laki na nusu, kwa wewe unayesafiri haraka ntakupa hii ya laki tatu hiyo haipungui na kama uko serious njoo haraka manake naenda kumuona afisa mkubwa" kilichokuwa kinaendelea pale ni kwamba watu waliokuwa wanafika pale uhamiaji kwa ajili ya ku process passport wanaanza kupokelewa kwa kukatishwa tamaa na yule ndugu anayekaa pale kwenye dawati la huduma kwa wateja hivyo wanashawishika kurudi pale kwa wale watoa copy nje.
Swali langu kama mimi niliyeenda pale kwa mara moja nimejionea hayo niliyoona, hakuna wahusika ambao wanajua kuna biashara hii haramu? na je nani ni wanufaika wa mradi huu. Ntakuwa nikileta mrejesho ambapo kwa ukiwepo ushahidi wa picha na video Kama kuna watu wamekataa kuwajibika ngoja sasa tuwawajibishe [HASHTAG]#unokoniuzalendo[/HASHTAG]
Nimejaza fomu nikasubiria siku 30 nikaitwa kuichukua. Nikawahamasisha na wenzangu nao wakajaza wakapata bila kikwazo.
Mi nadhani tatizo la dar ni msongamano unaosababishwa na uhitaji mkubwa
...Mi niliwaambia nataka kwenda kusoma nje hivyo nimekwama kuendelea na application wanataka pasipoti namba na kwenye barua nilijieleza
.....,