Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Siyo kweli jamani awamu hii ufisadi, rushwa na wapiga dili wamekomeshwa kabisa,hamuoni viongozi wanavyojivua nyadhifa zao ilikuunga mkono juhudi.
 
ndugu mjinga acha kumpotosha mwenzio! Au wewe ndio miongoni mwa vishoka hapo uhamiaji!?
Mimi ni muhanga wa kunyimwa passport. Sihusiki chochote na zile fremu pale nje.
Lakini jamaa yupo kweli 100.passport ni ngumu.sasa ukishajua hilo hapo lazma ujiongeze pale nje.vinginevyo unarudi kwao mikono mitupu.
 
Mkuu acha kupotosha watu
Kama hauamini basi .sikulazimishi.
Mimi sijaleta hyo mada.
Ila nilishawahi kwenda kuomba passport niende cape town kuhangaika na maisha.form niliyopewa na viambatanisho nilivyokutana navyo ni kikwazo tosha.
Ukiomba passport kwa safari yoyote kuna viambatanisho vyake.na vyote vitimie.
 
Rushwa pale ni kama kwenye çhaguzi za ndani za ccm hawana hata aibu wala woga
Kweli kabisaaaa. CCM na Rushwa ni sawa na Uhamiaji na Passport. Nashangaa Uhamiaji wanatoa work permit kwenye NGOs Yaani unakuta NGO ina foreigners kibao ambao wangeweza Kurudi kwao tu
 
Control lazima ianze kwenye kuzaliwa na kufa. Kila kitu kiwe na record ya kueleweka. Mtu anapoenda kwenye passport isiwe kama kinaanza kitu kisichoeleweka
 
Swali langu kama mimi niliyeenda pale kwa mara moja nimejionea hayo niliyoona, hakuna wahusika ambao wanajua kuna biashara hii haramu? na je nani ni wanufaika wa mradi huu. Ntakuwa nikileta mrejesho ambapo kwa ukiwepo ushahidi wa picha na video Kama kuna watu wamekataa kuwajibika ngoja sasa tuwawajibishe [HASHTAG]#unokoniuzalendo[/HASHTAG]


Tulitegemea haya yafanywe na PCCB lakini nao wamekula samaki aina ya pono, kama JPM alivyofika kwa dharura bandarini na kwingineko, hali kadhalika angefika maeneo kama haya na vituo vya polisi ambako rushwa imekithiri, kuna sub offices ndani ya ofisi halisi za serikali

Unachokisema ni kweli kipo, ila ni kwamba kuna genge la maofisa pale kurasini wanaojihusisha na biashara hiyo, na wana connection na wale wa madirishani na wale wanaoprint hizo passport, sina hakika kama boss wao mkuu anayajua hayo
 
Uhamiaji ilishaoza imeshindikana. Wanasubiri hadi rais ndio akatumbue wahusika wametulia wanachekelea rushwa inavyotembea pale. Ni jambo lililowazi bila kupepesa.


Watumishi wanashindana kuuza huduma
 
Kwanza kabisa nakupongeza mtoa post kwa kueleza kile ulichokiona pale Uhamiaji na kuamua kushea nasi!

Mimi sio afisa uhamiaji au mhusika kwa namna yoyotr ile na uhamiaji ila naomba nikujibu kwa ufafanuzi ufuatao;
1. Idara ya Uhamiaji kama utakumbuka mwaka jana ilizindua huduma za e-Services ambapo waombaji wa passport na permit walielekezwa wafanye maombi kupitia website ya idara hio www.immigration.go.tz. wakati huo huo utaratibu wa kujaza fomu za kawaida (hard copy) ukiendelea mpaka stock ya form hizo utakapokwisha na hakuna form zingine kuchapishwa.
2. Stationery zilizopo hapo sio mradi wala hazihusiani na afisa yeyote wa uhamiaji, ni ofisi zilizoanzishwa na watanzania wajasiriamali kujitaftia rizki zao kwa kutoa fotokopi, kupiga picha za passport na wengine wanasheria kufungua ofisi zao humo.

3. Fomu ya passport imewekwa kisheria ndani ya Passport and Travel Documents Act Namba 20 ya Mwaka 2002 ambapo mojawapo ya sharti la fomu kukamilika na kupokelewa na afisa uhamiaji lazima isainiwe na mahakama, mwanasheria au wakili aliyesalijiwa.

4. Affidavid ni suala linalohusika na Mahakama/Wakili/Mwanasheria hivyo afisa uhamiaji ni kuhakikisha kuwa kwenye viambato vyako kama kunahitajika affidavit anakupa maelekezo ukailete, suala la wapi na nani katoa sio la uhamiaji, muhim afisa atajiridhisha kuwa aliyetoa kasajiliwa.

5. Yawezekana kwa sasa form za kawaida (hard copy) zimekwisha ndio maana yule afisa wa kaunta kakuelekeza uende mtandaoni kujaza fomu na ww pamoja na wananchi wengine wakiambiwa hivyo huishia kwenye vibanda hivyo kupata huduma tena kwa bei anayotaka mhudumu ambapo uhamiaji haihusiki kwa namna yoyote ile.

7. Kwa uzoefu wangu najua kwamba passport hutolewa ndani ya siku saba hadi 14 lakini pia huwa kuna wahitaji wanaotakiwa kupata passport kwa haraka zaidi mfano kuwahishwa kwenye matibabu nchini India, Uhamiaji kwa kuwajali wananchi hutoa kipaumbele kwa watu wa namna hio.

8. Asilimia kubwa wa wateja wa huduma za uhamiaji huwa waoga na hivyo kuomba kusaidiwa hata kujaza fomu tu ya maombi, mfano ninao kuna dogo mmoja alikuwa kwenye stationery moja kazi yake kujaza fomu tu na kila fomu akijaza kwa elfu 2. Sasa leo kiti kipo mtandaoni unategemea dogo atakuwa anapiga bei gani?

I stand to be criticized

6.
 
Tatizo watanzania wanapenda kufanyiwa kila kitu ndio wajanja wanapata upenyo wa kuwalia pesa zao. Mfano kuna dogo mmoja alikuja kwenye steshenari mojawapo za hapo karibu na uhamiaji kama mpiga picha za paspot, lakin badae aligeuka kuwa mtaalamu wa kujaza fomu za paspoti kwa elfu 2 tu. Kwa siku alikuwa na uhakika wa kutoka na elfu 30 achilia mbali kazi yake ya kupiga picha.
Na wewe unapata wapi ujasiri wa kumfuata akusaidie huku ukijua huyo sio authorised officer wa pasipoti? Watu wengine tubadirike bwana we unaenda kuchezea mzinga wa nyuki wakikuuma unashangaa
 
Tulitegemea haya yafanywe na PCCB lakini nao wamekula samaki aina ya pono, kama JPM alivyofika kwa dharura bandarini na kwingineko, hali kadhalika angefika maeneo kama haya na vituo vya polisi ambako rushwa imekithiri, kuna sub offices ndani ya ofisi halisi za serikali

Unachokisema ni kweli kipo, ila ni kwamba kuna genge la maofisa pale kurasini wanaojihusisha na biashara hiyo, na wana connection na wale wa madirishani na wale wanaoprint hizo passport, sina hakika kama boss wao mkuu anayajua hayo
Inawezekana kukawa na connection baina ya afisa na vishoka ila sio kwa utawala wa huyu mama kamishna.

Nakumbuka mara ya mwisho watu wanaohisiwa vishoka karibu 8 walikamatwa pale kupigwa picha na kuamriwa kutofika eneo hilo na iwapo wataonekana watakamatwa na kufikishwa mahakamani
 
Tatizo watanzania wanapenda kufanyiwa kila kitu ndio wajanja wanapata upenyo wa kuwalia pesa zao. Mfano kuna dogo mmoja alikuja kwenye steshenari mojawapo za hapo karibu na uhamiaji kama mpiga picha za paspot, lakin badae aligeuka kuwa mtaalamu wa kujaza fomu za paspoti kwa elfu 2 tu. Kwa siku alikuwa na uhakika wa kutoka na elfu 30 achilia mbali kazi yake ya kupiga picha.
WaTz tunapenda kulalamika bila kucheck ground na ile form imeandikwa kabisa ijazwe na mhusika na imetaja mahitaji kadri ya nia ya safari ya mhusika ila kwenye hiyo kutoka kwa pasipoti siku 7 au 14 limekaa ki siasa zaidi kwa sababu kuna uvumi ulikuwa unazagaa kuwa hakuna vile vijitabu watu wamekaa muda mrefu sana bila kupata pass zao mpaka leo watumishi wenzangu hawajapata pasipoti zao na miezi kama mitatu
 
Kama hauamini basi .sikulazimishi.
Mimi sijaleta hyo mada.
Ila nilishawahi kwenda kuomba passport niende cape town kuhangaika na maisha.form niliyopewa na viambatanisho nilivyokutana navyo ni kikwazo tosha.
Ukiomba passport kwa safari yoyote kuna viambatanisho vyake.na vyote vitimie.
Watanzania wengi tuna shida sana. Labda nikwambie kitu, Passport ni kitambulisho cha raia wa kigeni ndani ya nchi ambayo mwenye pasipoti sio raia. Pamoja na kwamba pasipoti anapewa mtu lakin bado inabaki ni mali ya serikali kwa maana matumizi ya hio pasipoti yaendane na kufuata sheria na taratibu za kiuhamiaji kwa nchi unayokwenda.

Sasa pamoja na kwamba pasipoti ni haki ya kila raia lakin lazima ukidhi vigezo vilivyowekwa kisheria ili kuweza kupatq pasipoti. Pamoja na kuambatanisha vyeti vya kuzaliwa, afidavit na vitambulisho vyote lakin lazima ulete documents za MADHUMUNI ya safari ambazo wengi hapo huwa wanakwama.

Madhumuni ya safari ndio yanayopelekea raia wa Tanzania upewe pasipoti kwani sio kitambulisho cha kukaa nacho ndani ni kitambulisho chako ukiwa nje ya nchi.

1.Madhumuni yanaweza kuwa ni Matembezi Binafsi hapa utatakiwa kuleta bank statement ili kujiridhisha kuwa huko uendako hutoigharimu serikali kukuridisha nchini baada ya kuwa Destitute huko. Binafsi ingine unaweza kuwa unaenda kumtembelea nduguyo nje ya nchi hivyo utatakiwa kuleta barua ya mwaliko na pasipoti na permit ya nduguyo huko aliko kama ni mtanzania, kama ni raia wa huko basi anatakiwa aandike barua ya mwaliko pamoja na kitambulisho cha uraia wake au paspoti.

2. Madhumini ya kibiashara unatakiwa kuwa na leseni na tin namba

3. Madhumini ya kimasomo unatakiwa kuwa na admission letter toka chuo unachokwenda kusoma.

4. Madhumini ya kidini, barua ya bakwata kwa mahujaji na barua zingine toka taasisi za kidini kama kanisani kwa ziara za kwenda israel.

Mengine utaongezea na ww ila jua kuwa vijana wengi wanadanganya wamealikwa na ndugu zao arabuni kumbe wanaenda kuwa watumwa wa kingono na mahausigeli tu. Watanzania wengi wanaoenda Sauzi wanakuwa mapusha na mateja kiti kinachoitia aibu serikali kila mara na pia kuigharimu kuwaridisha nchini.
 
Back
Top Bottom