Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

Uhamiaji bado kuna tatizo kubwa sana

mng'oa kucha

Senior Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
150
Reaction score
179
Kama kawaida watu wa kanda (maalum) ya ziwa huwa tunasahau hata salamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye mada,
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu vitabu vya hati ya kusafiria, kila mtu anasema lake leo nimekosa kazi nikaenda mapema kujionea makao makuu ya uhamiaji kurasini Dar es salaam, nilikaa kwa masaa mawili nikagundua yafuatayo vile vibanda vya kutoa copy pale nje ni biashara cover up kiuhalisia wale bila kumung'unya maneno nawaita mawakala wa pass port, niliingia duka la kwanza kutoa copy nikakuta kuna watu kadhaa nao wana subiri huduma hiyo yule dada mtoa copy anaongea na simu nanukuu "unataka express ama ya kawaida, kama ni express ni laki tatu inatoka ndani ya wiki" mwisho wa kunukuu yaani alikuwa anaongea bila uwoga na kwa ujasiri ukiangalia dukani humo kuna watu wengi kila mmoja anakukaribisha tena wababa wazima nikabahatika kumuona mmoja anamuhuri wa mwanasheria tayari kwa kutengeneza affidavity sh 15000.

Nikatoka nikaenda duka la pili baada ya kuona pale kuna msururu wa watu yule dada alikuwa ananitolea copy huku ameweka simu masikioni naye anaongea na mtu "ya wiki ni laki 3, wiki mbili laki 2 ya kawaida laki na nusu, kwa wewe unayesafiri haraka ntakupa hii ya laki tatu hiyo haipungui na kama uko serious njoo haraka manake naenda kumuona afisa mkubwa" kilichokuwa kinaendelea pale ni kwamba watu waliokuwa wanafika pale uhamiaji kwa ajili ya ku process passport wanaanza kupokelewa kwa kukatishwa tamaa na yule ndugu anayekaa pale kwenye dawati la huduma kwa wateja hivyo wanashawishika kurudi pale kwa wale watoa copy nje.

Swali langu kama mimi niliyeenda pale kwa mara moja nimejionea hayo niliyoona, hakuna wahusika ambao wanajua kuna biashara hii haramu? na je nani ni wanufaika wa mradi huu. Ntakuwa nikileta mrejesho ambapo kwa ukiwepo ushahidi wa picha na video Kama kuna watu wamekataa kuwajibika ngoja sasa tuwawajibishe [HASHTAG]#unokoniuzalendo[/HASHTAG]
 
Daah
Ushaharibu mkuu madili ya watu.lakini uko sahihi
Kuna wakati nilitaka kwenda sauzi kutafuta maisha.nikaenda pale nikajionea haya.
ukitaka ya 50,000 utaganda.
 
We umejua kabisa mtoa copy sio afisa uhamiaji i mean ni kishoka sasa kwa nini utake kuhudumiwa nae na unajua kabisa yule lazima awe kama kishoka ambae ameongeza kiasi chake kwa juu.Yaani mi ninachoona hapa ni kama kupewa kazi ya kupigisha mswaki mamba so usishangae kumezwa.
 
Ukiingia katika lile jengo.utakayokutana nayo. Lazma uwatafute wale wa nje.
passport ya Tanzania INA masharti mengi.hasa kwa sisi ambao uwa tunaamua kutoka kutafuta maisha.kuna mlolongo was vitu vingi. Mpaka unakata tamaa.
Mimi nilishawahi kupitia hyo hali.na kama viambatanisho havijakamilika.unanyima.sasa kwa nini usitoe rushwa ili upate??
 
Mkuu mbona passport yangu nililetewa nyumbani, nilipiga picha tu na kujaza form.
 
Ukiingia katika lile jengo.utakayokutana nayo. Lazma uwatafute wale wa nje.
passport ya Tanzania INA masharti mengi.hasa kwa sisi ambao uwa tunaamua kutoka kutafuta maisha.kuna mlolongo was vitu vingi. Mpaka unakata tamaa.
Mimi nilishawahi kupitia hyo hali.na kama viambatanisho havijakamilika.unanyima.sasa kwa nini usitoe rushwa ili upate??
Kumbe kukamilisha mahitaji au vigezo vinamnyima ofisa wa uhamiaji kula rushwa mi mbona niliipata pasiport yangu bila milolongo yoyote nilipewa maelekezo yote nikayatimiza .Unajua mwanya wa rushwa unakuja pale unapotaka urahisi ungefanya mwenyewe mahitaji yote angeshindwa kukuomba rushwa
 
We umejua kabisa mtoa copy sio afisa uhamiaji i mean ni kishoka sasa kwa nini utake kuhudumiwa nae na unajua kabisa yule lazima awe kama kishoka ambae ameongeza kiasi chake kwa juu.Yaani mi ninachoona hapa ni kama kupewa kazi ya kupigisha mswaki mamba so usishangae kumezwa.
Kishoka anapata wapi nguvu yakufanya kazi zaserekali?
 
Kuna idara zina shida sana. Passport isiwe kama nyara ya serikali mtu akiwa na sifa za kupewa.

Tunatengeneza mianya ya rushwa bila sababu.
Unataka kurahisisha mambo Si Ndio? Passport aitolewi km njugu mjomba.
 
Siyo uhamiaji tu. Bado tuna tatizo kubwa katika nchi hii na naamini kuwa itachukua muda mrefu sana mpaka kubadilika.

Kitu kikubwa kinachoniudhi mimi ni hii ishu ya kujuana. Yaani kama humjui mtu basi huduma utaipata kwa shida sana. Watu mmekaa mstarini kwa masaa halafu anakuja mtu anapita moja kwa moja kwa vile tu ana mtu anamfahamu.

Uhamiaji pale hata utimize masharti yote bado utazunguka mno wakati wenzio wenye watu wanaowafahamu wanapata passport zao upesi. Mimi huwa nasimamia principles na huwa sitoi rushwa kirahisi lakini Uhamiaji kidogo nikwame. Kuna matatizo makubwa pale !!!
 
Kumbe kukamilisha mahitaji au vigezo vinamnyima ofisa wa uhamiaji kula rushwa mi mbona niliipata pasiport yangu bila milolongo yoyote nilipewa maelekezo yote nikayatimiza .Unajua mwanya wa rushwa unakuja pale unapotaka urahisi ungefanya mwenyewe mahitaji yote angeshindwa kukuomba rushwa
Ngoja nikuulize swali.passport yako ulipo kwenda uliwaambia unataka kwenda wapi na kufanya nini..
 
Kama kuna Taasisi ya hovyo hapa Nchini basi ni pale uhamiaji.
Ni aibu sana kwa taasisi kama ile unafika kupata huduma unaambiwa Vitabu hakuna.
 
Ngoja nikuulize swali.passport yako ulipo kwenda uliwaambia unataka kwenda wapi na kufanya nini..
Mi niliwaambia nataka kwenda kusoma nje hivyo nimekwama kuendelea na application wanataka pasipoti namba na kwenye barua nilijieleza
 
Mi niliwaambia nataka kwenda kusoma nje hivyo nimekwama kuendelea na application wanataka pasipoti namba na kwenye barua nilijieleza
Unaona sasa.
Ungejaribu kuwaambia kwamba nataka kwenda Kenya kutafuta maisha.
Ungeona hayo maswali yake kwenye kaunta mpaka kwenye form.
 
Unaona sasa.
Ungejaribu kuwaambia kwamba nataka kwenda Kenya kutafuta maisha.
Ungeona hayo maswali yake kwenye kaunta mpaka kwenye form.

ndugu mjinga acha kumpotosha mwenzio! Au wewe ndio miongoni mwa vishoka hapo uhamiaji!?
 
Back
Top Bottom