Uhalisi wa ndoa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhalisi wa ndoa.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, May 18, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Jana nlianzisha thread kuuliza wale ambao bado hawajoa/olewa kama wangependa kufanya hivyo mbeleni na kama ni ndio au sio kwanini??!
  Majibu niliyopata yalikua yanatofautiana kwanzia waonataka kuwa na watu wa kushea nao maisha....mpaka wanaotaka kupendeza tu siku ya harusi na wa wanaotaka security!!

  Nikajikuta najiuliza kwa wale ambao wapo kwenye ndoa je nini kilichowashawishi na je walipata yote waliyotarajia na kutamani kuyapata
  kwenye ndoa???!

  Kwahiyo naomba niwaulize kwa faida ya wale wote tuliopo nje...
  ...Je wewe ulitaka/kubali kuoa/olewa kwasababu gani??!
  ...Baada ya kuingia mambo yalikua kama ulivyotarajia!?
  ...Kama mambo yalikua tofauti na matarajio yako je ni kwa uzuri au kwa ubaya???!
  ...Umewahi kujuatua au kushukuru Mungu kumchagua uliyemchagua???!
  ...Ungepata nafasi ya kurudi miaka kadhaa nyuma mpaka ulipokua unaamua kufungwa pingu za maisha ukiwa inajua kila kitakachotokea mbeleni ungefanya uamuzi tofauti na uliofanya???

  Please tupeni experince tujifunze kabla hatujaingia huko na matarajio kibao alafu tushindwe kuvumilia hali halisi!
   
 2. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  hapo kwenye red ningefanya uamuzi tofauti.
   
 3. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hhahahahhahahhaha imenibidi kwanza nicheke.

  1 Mie niliolewa kwa sababu nilimpenda/tulipendana,
  2 Na huku ndani hakika inakuwa ni ngumu kwa kile nilichotarajia kukipata nipata 100%
  3 Mara nyingi namshukuru Mungu kwa kunipa mume huyu, japokuwa mara chache nasema laiti ningejua, au Mwenyezi Mungu angekuwa anaonyesha kesho itakuaje, (sababu kila mtu anamapungufu yake) na kukwaruzana kupo
   
 4. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hahahahaha ni wengi wangefanya ivyo
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Lizzy dear thanks for the thread... Interesting...lol... Umewaza nini???? Enways....

  Je wewe ulitaka/kubali kuoa/olewa kwasababu gani??!

  Lizzy nampenda shemejio vibaya mno na namshukuru Mungu ndoa
  haijafanya Mapenzi yapungue bali yawe stronger... Nafikiri inachangia
  pia na the fact kua we both appreciate each other and compromise
  in cases were neccessary... For instance sipendi football (najua nitazomewa hapa..lol)
  but whenever anipi attention sababu ya mpira i don't care...

  Baada ya kuingia mambo yalikua kama ulivyotarajia!?
  I think nimeijibu above... It's wonderful, ndo mana Partner nimekazana
  kupiga debe so that soon and very soon upate wako...lol

  Kama mambo yalikua tofauti na matarajio yako je ni kwa uzuri au kwa ubaya???!
  I think kwa uzuri zaidi... I thot itakua kazi saana, kumbe jamaa kanizimia kama
  nilivyomzimia.. the rest vinafuata..

  Umewahi kujuatua au kushukuru Mungu kumchagua uliyemchagua???!

  Partner HELL Nooooooooooooooooooooo!!!!

  Ungepata nafasi ya kurudi miaka kadhaa nyuma mpaka ulipokua unaamua kufungwa
  pingu za maisha ukiwa inajua kila kitakachotokea mbeleni ungefanya uamuzi tofauti na uliofanya???

  Kabla ya ndoa ningemsisitiza kua i want not less than 4/5 children... ili asing'ang'anie namba
  ndogo ya watoto.
   
 6. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  mmmmh.mengine usitake kuyajua mapema Lizzy,
  unaweza kushindwa kutoa maamuzi,
  uzuri wa ngoma ni uingie ucheze bibie, sio ubaki mtazamaji!!!!!!!!!!!!
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwanini???Maelezo kidogo basi...`
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  angalau kidogo,
  inaonyesha kuna kaukweli fulani hapa...............
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Partenerrrrr....nataka kumchunguza kuku kabla sijamla!!Kwa kukusoma naona ukimpata wako ambae nae wewe ndo wake inakua raha mustarehe hata kama vijitatizo vya hapa na pale havikosekani!!

  I‘m happy for you partner...nakuombea miaka kumi ijayo uwe na mawazo kama haya haya kuhusu shem wangu au hata mazuri zaidi!!
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ni vizuri kujiandaa....
  Embu tupe expiriensi‘!
   
 11. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nikajikuta najiuliza kwa wale ambao wapo kwenye ndoa je nini kilichowashawishi na je walipata yote waliyotarajia na kutamani kuyapata
  kwenye ndoa???!

  Kwahiyo naomba niwaulize kwa faida ya wale wote tuliopo nje...
  ...Je wewe ulitaka/kubali kuoa/olewa kwasababu gani??!
  ...Baada ya kuingia mambo yalikua kama ulivyotarajia!?
  ...Kama mambo yalikua tofauti na matarajio yako je ni kwa uzuri au kwa ubaya???!
  ...Umewahi kujuatua au kushukuru Mungu kumchagua uliyemchagua???!
  ...Ungepata nafasi ya kurudi miaka kadhaa nyuma mpaka ulipokua unaamua kufungwa pingu za maisha ukiwa inajua kila kitakachotokea mbeleni ungefanya uamuzi tofauti na uliofanya???

  nikijibu baadhi ya maswali hapo juu:
  ......kuoa/kuolewa ili kama itatokea basi watoto wawe wa halali (not bastards), watakaoendeleza ukoo (genetic transmission)
  ......so far so good, milima na mabonde, lakini tunapata muafaka baina yetu
  .....baadhi mambo yako poa, baadhi mambo huenda kinyume cha matarajio ila mara zote yameweza kurekebishika, kwa kiujumla mambo yetu poa sasa ni miaka 21
  .....sisi sote wawili tunamshukuru mwenyezi mungu kila siku, that we are compatible!
  ......uamuzi wangu usingebadilika hata kwa kidogo, kwani niliyemchagua amenifaa, na anaendelea kuongezeka ubora kila siku

  Hivyo, Lizzy usiogope kuolewa/kuoa ni kuzuri
  kazi ipo kwenye kuchagua!
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Sorry to say this,kwa wanawake sijui lakini asilimia kubwa ya wanaume tunapokuwa vijiweni kwetu tunapiga ulabu mazungumzo huwa ni yale yale......utasikia 'yaani aisee itokee mi na waif tuachane wallah sioi tena' na wakati mwingine kwenye group kama kuna member ambaye kamtaliki mkewe na hajaoa tena utasikia..'heri yako bwana maana sisi lol'.....au utasikia wanamwambia .....'aisee usioe tena...'.Nisameheni bure kinamama lakini hapa nimeeleza uzoefu wangu kwenye mazungumzo ya kina baba,AshaD najua nimekukwaza because you sound happy in your marriage,lakini mimi naeleza ninachosikiaga.
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Lizzy,

  Nina wasiwasi na unakoelekea sasa!

  Ndoa zoote uwa inatokea kama ajali - Hakuna watu waliofunga ndoa baada ya kufanya tathimini kama unazofanya - No, Never.... Ndoa haina KPI wala Bench-Marking, Not at all ... Normally, Ndoa ni mwanzo mpya - Ni kama unavyozaliwa - Hakuna aliyetuma maombi kwa Baba na Mama yake kuwa atungwe mimba na kuja dunia - It is simply natural... Sijui kama ulishawahi kufikiri kuwa "Ni heri usingezaliwa.."
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo wanajutia??!!Aiseee mi sitaki kua na mtu alafu ajutie!!!
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  BE hichi ni kizazi cha kutafakari bwana...hata kupata watoto watu wanapanga mwaka mzima wakati zamani ni kuzaa tu!!Yote hiyo ni kwasababu ndoa za siku hizi nyingi ni ili mradi tu.....na mimi sitakua kua kwenye kundi la wanaoolewa ili mradi!!
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Hujanikwaza Bishanga... Mi naelewa how baadhi ya minds za wanaume zilivyo, hasa mume wangu na najua akiwa kijiweni atasema kama hao wakaka wengine... We ni mwanaume na naamini unaelewa hakuna anae brag kua oo mke wangu anafaa sana au vipi.. Mimi kua na furaha na amani katika ndoa yangu haimanishi nayeye ni hivyo hivyo - ukute kujitahidi kwangu kote anaona sawa tu na ndo kwanza ana mwanamke nje... But sababu hajanionesha kitu chochote cha kunifanya niwe na wasi; saizi am content ...

  Na Bishanga note kua most ya hao wakaka wakijiweni wakipata matatizo ya ndoa wako makini kutatua matatizo kuepusha kuvunjika kwa ndoa...
   
 17. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  nimekupata mtu mzima,
  ukubwa dawa!!!!!!!
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  ndivyo inavyoonyesha..
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0

  hapo kwenye red unanikumbusha story ya jamaa ambao wakiwa bar kila mmoja anajitutumua kuwa yeye undava undava tu mwanamke hambabaishi nyumbani kumbe weeeee akiingia tu 'mama Kayai nisamehe nimechelewa,sio mimi ,ni Bishanga kanichelewesha na porojo zakeeeee,maneno kibao huku amepiga magoti!
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  am learning something.. keep talkin guys
   
Loading...