Mahusiano na ndoa!

Big Phil

Member
Nov 20, 2019
50
338
Wanaume huwafuata Wanawake kwa mambo mawili, ambayo ni MAPENZI na SEX. Lakini inapofika hatua ya Kuoa, Wanaume hawaoi kwa sababu ya SEX au MAPENZI, wanaoa kwa sababu ya kutafuta AMANI NA UTULIVU WA NAFSI (STABILITY).

Mwanaume anaweza kukupenda na asikuoe
Mwanaume anaweza kuwa anafanya mapenzi na wewe tena mkadumu kwa muda mrefu lakini asikuoe. Lakini akampata mtu mwingine akamuoa hata kama mahusiano yake na mtu huyo yalikuwa ya miezi miwili.

Wanaume wengi hutizama mbali zaidi pale wanapotaka KUOA. Huwa hawafikirii habari za suti kali za harusi na sherehe ya gharama, vitu ambavyo hufikiriwa zaidi na wanawake kila wanapoiwaza ndoa.

Wanaume huwaza, iwapo mwanamke huyu anaweza kuijenga familia bora, anaweza kuwahudumia watoto? Hatanipa stress huko mbeleni, hatanisumbua katika masuala ya tendo la ndoa?

Wanaume wanaotaka kuoa huwa hawapendi wanawake wanaowapa mawazo,

Binti mmoja aliwaambia wazazi wake kuwa ana mchumba na anakuja kujitambulisha, wazazi waliitana na kuandaa kila kitu lakini yule mchumba hakutokea, alitafuta udhuru wa ajabu ajabua na binti kwa aibu aliwaambia wazazi wake kuwa kapata matatizo atakuja wakati mwingine.

Muda ulipita na binti aliendelea na mahusiano na yule Kaka ahadi zikiwa zilezile nakupenda, nitakuja, subiri hiki subiri kile.

Siku moja Bibi yake alimuita na kumuambia ni mwaka sas atangu utuambie una mchumba je bado uko naye au ushamuacha

binti akasema yuko naye lakini haoni kama kuna ndoa tena, anahisi mwanaume anampotezea muda. Bibi akamuuliza kama unahisi anakupotezea muda kwanini usimuache atakuumiza. Binti akamjibu “Bibi hawezi kuniumiza tena nishamjua hata akiniacha siumii tena hata mimi

nampotezea muda tu sijali tena!” Bibi alitabasamu, siku iliyofuata Bibi alimuomba mjukuu wake kumsindikiza sehemu, waliondoka mpaka kufika sehemu kulikua na ndoo yenye maji machafu, Bibi akamuambia mjukuu wake kubeba binti alishangaa lakini bibi alimlazimisha akabeba, uchafu ulimdondokea na maji yalikua yakinuka sana, walitembea mpaka sehemu nyingine, wakakuta kuna ndoo ya maji masafi, Bibi akamuambia kuwa amsaidie kubeba tena, binti akamuambia hataweza kwani ana ndoo nyingine kichwani.

Bibi akamuambia kama hawezi basi waondoke na ile ya maji machafu, binti akasema waweke chini ile ya maji machafu ili wachukue masafi lakini Bibi alikataa alimlazimisha abebe zote, ile ya maji masafi akashika mkononi na ile ya machafu akaweka kichwani.

Walitembea sana akachoka na kuachia ile ya maji masafi akabaki na machafu. Walifika nyumbani kachafuka na ananuka, Binti hakuelewa maana yake lakini Bibi alimuuliza kama kajifunza kitu akasema hapana!
Bibi alimuambia mjukuu wangu unapokua na mpenzi ambaye haeleweki ukaendelea naye na kudhani unampotezea muda tu ni sawa na kubeba ndoo ya maji machafu, unajua ni machafu lakini unabeba tu, ila kumbuka una kichwa kimoja, ukiwa umebeba maji machafu unajizuia hata

kubeba maji masafi na hata ukiyabeba kwa mkono basi utachoka tu na kuyaachia. Kama mpenzi unaona ni mzigo kwako unapoendelea kuwa naye unazuia nafasi ya mpenzi mwema kuja kwako.

C&P
 
Back
Top Bottom