Uhakiki wa watumishi hewa utamalizika lini?

Rais kwa umakini wake hawezi kuruhusu ajira ifanyike na watu wale wale waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa.Marehemu baba waTaifa Mwalimu Nyerere alisema mtu akila nyama ya mtu hawezi kuacha atarudia tena.Nafikiri ajira itaanza tena baada ya Mh Rais kusafisha maafisa utumishi wote waliofanya malipo hewa .
 
madeni ya watumishi- uhakiki 2010 ukiulizia leo utaambiwa yatalipwa uhakiki ukimalizika ,bunge lijalo utasikia uhakiki ukimalizika yatalipwa mwaka huu wa fedha....ndio utendaji wetu.vivyo hivyo ajira zitatolewa....muwe na subira!
 
huo uhakiki uishe tu ili zile bilioni 900 za madeni alizoenda kuzizuia kwa Prof. Nduru,mshkaji aziachie watu walipwe kama kweli alikua na nia njema na kama kweli watumishi hewa ndio waliokua sababu kwa yeye kuzuia haki za watu !
 
Ndugu zangu, kama mnavojua 13.06.2016 Tume ya utumishi wa UMMA ilitoa waraka wa siri kuhusu usitishwaji wa ajira mpya kada zote kwa mwaka 2016 ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa, baadae 22.06.2016, rais mh Dkt John Pombe Magufuli akasema wamesitisha ajira kwa muda ili kupisha zoezi la uhakiki kwa watumishi hewa na akasema itachukua mwezi mmoja ama mwezi mmoja na nusu lakini haitafika miezi miwili.

Swali langu ni:

1(a) Je, huo mwezi mmoja ama mwez mmoja na nusu ulianza kuhesabika lini na utakamilika lini?

(b) Je, aliposema haitazidi miezi miwili alimaanisha haitafika miezi miwili ama inaweza kufika miwili lakini isizidi hapo yaani kufika mitatu?
MWENYE KUELEWA NAOMBA ANISAIDIE.....

GIPAMA from Bunda-Mara.
Sasahivi tunahakiki wanafunzi hewa , tukimaliza kuhakiki wanafunzi hewa ,tunahakiki afya za watumishi.....
 
Baadhi ya ofisi hasa kwenye mashirika ya umma ndio kwanza zoezi limeanza, kumbuka pia kuwa hii inakwenda sambamba na ukaguzi wa vyeti vya waajiriwa wa taasisi na mashirika haya.

Nadhani kwenye lile tangazo sasa tumefuta ''kipindi cha miezi miwili'' na inabidi isomeke '' mpaka tutakapotangaza tena''.

Wasalimie Bunda, nilipita hapo nikielekea Nyamswa miaka michache iliyopita.
 
Kwanini watu wengi wakitaja bunda lazma waseme nyamswa, kuna nn pale!?
 
Kwanini watu wengi wakitaja bunda lazma waseme nyamswa, kuna nn pale!?
Mkuu mi nakumbuka nyama pori tu. Miaka ile ilikuwa inapatikana kwa wingi sana pale, ukitaka nyama ya swala, nyati na nyinginezo unapata za kutosha.
 
Baadhi ya ofisi hasa kwenye mashirika ya umma ndio kwanza zoezi limeanza, kumbuka pia kuwa hii inakwenda sambamba na ukaguzi wa vyeti vya waajiriwa wa taasisi na mashirika haya.

Nadhani kwenye lile tangazo sasa tumefuta ''kipindi cha miezi miwili'' na inabidi isomeke '' mpaka tutakapotangaza tena''.

Wasalimie Bunda, nilipita hapo nikielekea Nyamswa miaka michache iliyopita.
hahha sio kisorya
 
Uhakiki haujaisha mnatakiwa kuhamia dodoma
haraka sana na mara moja
 
Back
Top Bottom