Uhakiki wa watumishi hewa utamalizika lini?

GIPAMA

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,103
541
Ndugu zangu, kama mnavojua 13.06.2016 Tume ya utumishi wa UMMA ilitoa waraka wa siri kuhusu usitishwaji wa ajira mpya kada zote kwa mwaka 2016 ili kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa, baadae 22.06.2016, rais mh Dkt John Pombe Magufuli akasema wamesitisha ajira kwa muda ili kupisha zoezi la uhakiki kwa watumishi hewa na akasema itachukua mwezi mmoja ama mwezi mmoja na nusu lakini haitafika miezi miwili.

Swali langu ni:

1(a) Je, huo mwezi mmoja ama mwez mmoja na nusu ulianza kuhesabika lini na utakamilika lini?

(b) Je, aliposema haitazidi miezi miwili alimaanisha haitafika miezi miwili ama inaweza kufika miwili lakini isizidi hapo yaani kufika mitatu?
MWENYE KUELEWA NAOMBA ANISAIDIE.....

GIPAMA from Bunda-Mara.
 
Mi nadhani tuache kurudia rudia sentensi, ni kwamba WATANZANIA WAMEKUWA WAKIZALIANA KUPITA KAWAIDA hivyo kila aliyesomea Ualimu aanze kufundisha watoto wake ama familia yake maana MAADILI HAYAANZII SHULENI BALI NYUMBANI. Watoto tunao majumbani kwetu kwanini tusubiri kwenda kuwafundishia mashuleni?. Nakushauri anzia kufundisha ngazi ya uzao wako, familia yako, taifa lako etc na Mungu akubariki. Kwasasa Rais yupo busy kutumbua Majipu kila siku!
 
Mkuu ushauri wako nime ukubali Teh Teh..
 
elewa ajira hakuna kabisa tafuta shamba tu walioajiriwa mwezi wa tano mwaka huu wamerudishwa wote wengine walikuwa wamekula na pesa za kujikimu
Sawa, maana uwezo wako wa kufkria umekomea hapo.
 
Next week mkuu zitatangazwa,but cdhani kama watachukua walimu wote maana nimeskia eti kama walimu watakuwa na upungufu wataongeza kwa idafdi hiyo ya upungufu means kama arts wanahtajka ,10000 ,bs wataajiri kiasi hicho hicho wengine watatoswa sa sjui kweli or wat
Nani kakuambia?
 
Jamani naomba tumpe Rais nafasi apange safu yake na aweke taratibu nzuri za kuiongoza nchi. Nadhani hata ungelikuwa wewe ukipewa madaraka hata madogo ya ualimu wa mazingira, yapo utakayofanyia marekebisho japo awali alikuwepo mwalimu mwingine aliyekukabidhi nafasi hiyo. Vuteni subira uongozi ni kazi ngumu.
 
Acha siasa taka wewe kuwawash brain watu wakati maisha magumu wape hela sasa
 
Back
Top Bottom