Ombi kwa Bernard Membe

msweken

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
441
1,714
Ni ukweli usiopingika kuwa Mzee wetu Edward Lowasa hawezi mikiki mikiki ya Kampeni tena, na hata kama atajitahidi CCM watatumia mbinu zilezile za kumchafua kwa kusema kuwa ni mgonjwa. Na ni ukweli tena usiopingika kuwa mzee hayupo vizuri sana (kwa kuangalia video mbalimbali zinazorushwa mitandaoni zikionyesha akihangaika kutembea, kushuka ngazi).

Upinzani hakuna mtu mwenye haiba za kuwa Rais wa Nchi hii wa kuweza kupambana na JPM hata kama amekua ni mtu wa kufanya makosa mengi, JPM amekua akipoteza mashabiki wake wengi sana wa kisiasa kuanzia Wafanyakazi (kutokupandishwa mishahara, kutokulipwa malimbikizo yao, ongezeka la makato kutoka bodi ya mikopo, upendeleo wa dhati kwa mfanyakazi namba 1 wa Dar, maigizo ya uhakiki wa vyeti na mengi), Wanachuo (kukosa mikopo, kufukuzwa vyuo kwa kuambiwa hawajakidhi vigezo etc) wahitimu waliopo mtaani (hawa ajira wanaisikia Nchi jirani ya Kenya huko, si kwa walimu, Madaktari na wahitimu wengine), wafanya biashara (kodi nyingi kuliko makusanyo), Raia wa kawaida hawa wanalia kuwa pesa imekua adimu kuliko miaka yote iliyopita.

Upinzani kuna watu makini sana wanaoweza kuwatumikia Watanzania kama Mawaziri na watendaji wengine lakini wanakosa mtu wa kuweza kusimama kama kichwa na kupambana katika nafasi ya Urais.

Kwa mtazamo wangu mimi huu ni muda wa kumuomba Ndugu BERNARD MEMBE atoke huko alipo na apinduke upande wa pili kwa ajili ya kumsimamisha akiwakilisha upinzani na LOWASA abakie kutoa support na si kuwa mgombea. Natambua kuwa hawa wawili walikua na ligi yao huko CCM ila ni vyema kwa maslahi mapana ya Nchi hii wakaungana kwa ajili ukombozi. I can’t imagine collabo ya Lowasa na Membe wote wakisimamia kitu kimoja.

Mh. Mbowe naamini kuwa wewe ni muelewa na unajua vyema kuusoma upepo wa kisiasa hapa nchini, na najua kuwa unajua Watanzania tunampenda kwa dhati Lowasa, tafadhali piga sarakasi zako kidemokrasia kabisa kumfanya mzee wetu abakie kutoa Support na tuletee BERNARD MEMBE aje akimbizane na figisu figisu za ndugu zake CCM akiwa upande wetu wa upinzani.

Mh. Bernard Membe, hii nchi ni ya kwetu sote si ya kuizira wala kuitelekeza. Uliutaka Urais ukiwa huko CCM na umeukosa na hakuna dalili kuwa JPM atakubali upinzani ndani ya CCM, HAMIA UPANDE WA PILI NA UJIPANGE MAPEMA KABISA KATIKA VITA YA UKOMBOZI.

Nchi hii sio group la watsap useme tunaweza kujitoa, Tumezaliwa Watanzania na tutabakia kuwa Watanzania ipo haja ya kuungana na kukubaliana na ukweli kuwa ni lazima Tuungane bila kujali yaliyopita, vyama vyetu na itikadi zetu ili kulinusuru hili Taifa.
 
We Jamaa Una Akili Sana Vijijini walikua wanajaa Mikutanoni kuangalia Lowassa ambaye Propaganda za ACT zilisema anajinyea.

Lowassa hadi Leo hawezi kukaa akihutubia kwa dakika 10. Atanishangaza sana kama atagombea Urais pia amepoteza ushirikiano wa Maneno na Mdomo anaongea vitu havieleweki Yaani ni Mzigo mpaka sasa ule Mkono wake wa Kulia Unaonekana kabisa ni Mbovu

Mimi nikimuangalia huwa naona kama mdori au Mtu aliyechorwa Lowassa has no Balls to win election
 
Back
Top Bottom