SoC03 Uhaba wa dawa na vifaa tiba ni kilio kikubwa kwa jamii ni vyema serikali kuhakikisha hali hii inakoma

Stories of Change - 2023 Competition

Run final

New Member
Jun 26, 2023
2
2
UHABA WA DAWA NA VIFAATIBA NI KILIO KIKUBWA KWA JAMII NI VYEMA SERIKALI KUHAKIKISHA HALI HII INAKOMA
Utangulizi
Uhaba wa dawa na vifaatiba kwenye hospitali, zahanati na vituo mbalimbali vya afya zikiwemo za serikali hapa nchini. ni hali ambayo kwa kweli bado imekuwa ni changamoto kubwa kwenye taifa, hali iliyopelekea hata kuwe na huduma duni za afya kwa jamii, huku vilio vya watanzania vimekuwa ni vingi.

Ndani ya andiko hili nitagusia sababu kadhaa ambazo kwa asilimia kubwa, zimekuwa zikisababisha uwepo wa hali hii ya uhaba mkubwa wa dawa na vifaatiba kwenye taifa, ambazo ningependa kuona zikifanyiwa mabadiliko ili kuhakikisha hali hii ya uhaba wa dawa na vifaatiba inakoma.

Katika uhalisia, ndani ya siku kadhaa zilizopita nilifika kwenye hospitali iliyopo mkoa wa dar es salaam, ambayo inaitwa hospitali ya amana. mimi ni kijana mwenye tatizo la kutosikia vizuri, ambapo sikuzaliwa na tatizo hili lakini kutokana na mazingira ya kimaskini niliyokuwa naishi tangu nikiwa mdogo nilijikuta nikiwa na tatizo hili. hali ambayo inanipa changamoto sana hasa kwenye kujitafutia ridhiki na kutafuta Kazi, hivyo baada ya kupata fedha kidogo nilifika kwenye hospitali hiyo ya amana kwa lengo la kupata huduma za afya.

Nilipofika kwenye hospitali hiyo nilifuata utaratibu wote wa pale hospitalini, lakini sikuweza kupata huduma zozote za afya, ambapo hata nilipomuona daktari aliniambia kuwa hospitali hiyo haina dawa wala vifaatiba vya masikio, kwa kweli niliumia sana.

Lakini pamoja na hayo, ni wazi kwamba nchi yetu bado imekuwa na dawa nyingi tu kwenye bohari kuu ya dawa (MSD), ambazo zimekuwa zinaharibika tu ghalani, wakati watanzania tunateseka na kuangamia kwa kukosa dawa. (Rejea ripoti za CAG 2021/22)

Inamaana kwamba wakati watanzania maskini tukiteseka kwa kukosa dawa, kumbe kumekuwepo na dawa nyingi tu ambazo zimefungiwa kwenye maghala ya bohari mpaka zinaharibika, ni wazi kwamba bohari kuu ya dawa kwa asilimia kubwa imekuwa ikisababisha kuwe na uhaba mkubwa wa dawa kwenye taifa. yani ndio maana ukienda mfano hospitalini unakuta dawa hakuna, kumbe dawa nyingi zipo zinaharibika tu kwenye maghala ya bohari kuu.

Lakini pia, licha ya CAG kuliongelea suala hili la kuwepo kwa dawa zinazoharibika kwenye maghala ya bohari kuu, lakini mpaka sasa hatuoni hatua zozote zilizochukuliwa na serikali kuhusiana na suala hili, yani utazani kama vile hakuna chochote kibaya kilichotokea, wakati suala hili sio tu kwamba limesababisha uhaba mkubwa wa dawa kwenye taifa, lakini pia ni suala ambalo limesababisha hasara kubwa za mabilioni ya pesa kwa serikali, alafu wala hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali mpaka sasa.

Logopit_1690385447317~2.png


Mapendekezo
  • Nashauri serikali ni vyema kuchukua hatua kuhusiana na suala hili la kuharibika kwa dawa na vifaatiba kwenye bohari kuu ya dawa ili suala hili lisije kujirudia tena hapo baadae; Kwasababu licha ya CAG kuliongelea suala hili la kuharibika kwa dawa nyingi kwenye bohari kuu, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na serikali mpaka sasa kuhusiana na suala hili, inamaana kwamba wale wote waliosababisha dawa zenye thamani ya mabilioni ya pesa kuharibika ghalani, bado wapo wanadunda tu kama kawaida kwenye bohari kuu ya dawa wala hawawajibishwi. hali hii inaweza kupelekea kusiwepo na uwajibikaji mzuri kwenye bohari kuu na hata kupelekea baadae dawa zijekuharibika tena ghalani na kuzidi kusababisha uwepo wa uhaba mkubwa wa dawa kwenye taifa. sasa basi nashauri serikali ni vyema kuchukua hatua kuhusiana na suala hili, ili kuwepo na uwajibikaji mzuri kwenye bohari kuu ya dawa.
  • Nashauri serikali kuhakikisha kwenye utendaji mzima wa bohari kuu ya dawa kunakuwa na uwazi ili tuweze kuwajibishana mapema kabla ya tukio likiwa bado halijatokea, sio kila kitu kusubiri mpaka CAG aje aseme ndo tuwajibishane ambapo tukio likiwa tayari limeshatokea na kusababisha kilio kwa jamii; Katika uhalisia ndani ya nchi yetu mara nyingi tumekuwa tukisubiri mpaka CAG akiongea ndio tuanze kuwajibishana, ambapo wakati huo tukio linakuwa tayari limeshatokea na kusababisha kilio kikubwa kwa jamii au hata hasara kubwa. Mfano ripoti za CAG kuhusu dawa na vifaatiba zilizoharibika kwenye maghala ya bohari, hili ni tukio ambalo tayari limeshatokea na kusababisha hasara za mabilioni pamoja na vilio vya uhaba mkubwa wa dawa na vifaatiba kwa jamii. sasa basi nashauri serikali ni vyema kwenye utendaji mzima wa bohari kuu ya dawa, kuwe na uwazi ili tupate nafasi ya kuwajibishana mapema kabla ya tukio likiwa bado halijatokea, ambapo kwa kupitia njia hii kutapelekea kuwe na uwajibikaji mzuri kwenye bohari, ili kusiwepo na dawa zitakazokuwa zinaharibika tena kwenye maghala ya bohari, kwasababu mpaka dawa zinafikia kuharibika hivi ghalani, ni wazi kwamba kumekuwa hakuna uwajibikaji mzuri kwenye bohari kuu na tukisema tusubiri mpaka CAG aje kuongea ndo tuwajibishane, tunakuwa tushaingiza hasara kubwa, huku vilio vya uhaba mkubwa wa dawa vinakiwa kila sehemu. lakini Kama kwenye utendaji wa bohari kuu ya dawa ukiwa na uwazi, tutaweza kuepukana na vitu vingi, kwasababu kutakuwa kunakuwajibishana mapema kabla ya tukio likiwa bado halijatokea.
  • Nashauri serikali ni vyema kwenye usambazaji wa dawa kuhusishe pia na vituo vya afya ili kusiwepo na uhaba wowote wa dawa kwenye vituo hivyo; katika uhalisia kwa miaka mingi sasa ukienda mfano kwenye hospitali zetu nyingi hata zile zilizopo mijini ambazo ni rahisi kusambaziwa dawa, unazikuta pia zina ukosefu mkubwa wa dawa, alafu wakati huo dawa zinaharibika tu kwenye maghala ya bohari, ni wazi kwamba kumekuwa hakuna usambazaji mzuri wa dawa unaofanyika. sasa basi nilikuwa nashauri serikali ni vyema kwenye usambazaji wa dawa kuhusishe pia na vituo vya afya, ili kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa na dawa za kutosha. yani vituo hivyo vitakuwa vinafuata dawa kwenye maghala ya bohari kisha vinajisambazia moja kwa moja, pale tu vitakapokuwa na uhaba wa dawa na sio unaenda kwenye hospitali unaambiwa dawa hakuna, kumbe dawa zipo kwenye bohari kuu ya dawa na kunauwezekano wa kuzifuata. lakini pia kumbuka kutosambazwa kwa dawa kwenye vituo vya afya kunaathiri watumishi wa umma kiutendaji kwenye kutimiza wajibu wao, hivyo njia hii itachochea pia uwepo wa uwajibikaji.
  • Nashauri serikali kuanzishwe utaratibu wa viongozi kutembelea angalau kwa mara kadhaa kwenye vituo vyote vya afya, ili kusikiliza maoni ya jamii ambayo yatasidia kuboresha huduma za afya na kupelekea uwepo wa uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Hitimisho
Mwisho nitoe shukrani kwa jamiiForums, kwa fursa hii nzuri kwa jamii ya kujielezea na kutoa mawazo yenye tija, ambayo yanaweza kuleta madaliko chanya kwenye taifa.
 
Back
Top Bottom