Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Tatizo hamjui kanuni za uchumi. Marehemu alichokuwa anafanya ilikuwa ni primitive economy, na kamwe asingefanikiwa.

Kinachohitajika ni kuuchangamanisha uchumi wetu na uchumi wa Dunia. Watatuuzia sukari, lakini nasi tutawauzia bidhaa nyingine.

Ukifungia bidhaa za wengine, na wewe za kwako zitafungiwa. Wewe unajua hasara waliyoipata wafanyabiashara wa mahindi, mbao, korosho na matunda, kutokana na maamuzi ya hovyo ya marehemu ya kuanzisha chokochoko ambazo hazikuwa na msingi wowote dhidi ya Kenya?
Ushaliwa kichwa ww
 
We ndio mkurupukaji! Unajua urasimu uliopo Tanzania kwenye viwanda vya sukari vinavyomilikiwa na wanasiasa akiwemo hayati mkapa na genge lake?

Unajua bei ya sukari kutoka Uganda ni 1500?

Unajua pia sukari kutoka Malawi ni 1500?

Unajua maana ya free market economy?

Unajua sisi tunauza sana Uganda kuliko wao wanavyouza huku?

Msijikite kulaumu tu wakati sukari ikipanda vile vile mnalaumu.

Pumbavu kweli ufahamu chochote kuhusu uchumi acha kulaumu Rais kwenye swala la uwekezaji yupo sawa kabisa mwenyewe namuunga mkono.

Tusifanye chuki zetu zitutoe ufahamu Tanzania bado hatujitoshelezi kwa Sukari, cement Na mafuta tuache siasa tufanye biashara.
 
Kwa miaka mingapi hivyo viwanda vya tz vimepewa nafasi ila vimeshindwa kukidhi mahitaji ya soko? Yaani viwanda viendelee kuwafanya watu wakose sukari kisa bei ipo juu kutokana na demand kuwa kubwa kuliko supply? Acha sukari ije bei ishuke, simple!
Ajira je huna ndugu labda huko viwandani na mkulima miwa?
 
Tundu Lissu hawezagi kukosoa sera za uchumi yy anaweza masheria sheria tu na ubishi mwingi...
issue kama hizi hatii pua kabisa......
yule ni mwanasiasa wa mabishano tu
 
Umeandika nini?
Nauliza ajira vipi? Wengi watapoteza ajira kwa sukari ya nje kuwa rahisi wakiwemo wakulima Wa miwa wanaouzia viwanda miwa !! Hiyo bei juu ilikuwa inasaidia nduguyo kuwa na ajira na wakulima kuwa na ajira kilimo cha miwa na vibarua kibao

Bei itashuka ila ujiandae nduguzo kupoteza ajira kiwandani na mashambani
 
Hayahaya tuliyakataa, nchi haiwezi kuendelea kwa kuimport tu. Sasa pesa yetu ya madafu inaenda kuzorota zaidi.
Sijui watanzania tumelogwa .....sasa sukari tunazalisha lakini haitoshi tunaishia kuuziwa bei kubwaa kisa tunalinda viwanda vyetu .Mm naona sawa tu maana km hapo zambia sukari ipo kibao bora tuagize na wazambia nao watachukua mchele hivo hivo hata kwa waganda wanakuja sana kanda ya ziwa kuchukua mchele, dengu na nk ...tuishi kwa kutegemeana .
 
Kwa miaka mingapi hivyo viwanda vya tz vimepewa nafasi ila vimeshindwa kukidhi mahitaji ya soko? Yaani viwanda viendelee kuwafanya watu wakose sukari kisa bei ipo juu kutokana na demand kuwa kubwa kuliko supply? Acha sukari ije bei ishuke, simple!
hakuna anaegoma sukari isije. Kwa taarifa yako Tanzania kila mwaka ina deficit ya zaidi ya Tani 120,000 za domestic sugar. Industrial sugar yote tuna import.

Ila kwa watu wenye akili ambao tumeiokomboa Uganda toka kwa dikteta Idd Amin 1978 na nchi ikawa haitawaliki mpaka 1986 Museveni alipoingia akitokea Tz; ni aibu kuuziwa sukari ila hatuna budi kununua maana mahitaji ya viwanda vya ndani hayana uwezo wa kukidhi soko.

Na hii sio kwenye sukari, kuna mafuta ya kula kila mwaka tuna-import tani 320,000/mwaka. Moja ya nchi inayotuuzia mafuta ya kula ni Malaysia walikuja kuchukua mbegu za mawese miaka ya '80; leo Malaysia ni nchi ya pili kwa export ya mafuta ya kula ikiwa nyuma ya Indonesia. Kwa lugha rahisi kuna pahala hatujatumia akili zetu vya kutosha kwa R&D namna ya ku-maximize potential ya ni Tz inaweza kufanya.
So nakubaliana nawe kama sukari toka Uganda na affordable kwa mlaji; ila swali linabaki, mpaka lini lini tutaendelea ku-import.

Simple understanding, kama tungezalisha ndani kwa kuanzisha viwanda vikubwa vya kisasa na kutotegemea Mtibwa, Kilimbero, Kagera na TPC Moshi (viwanda vya enzi ya Nyerere) kuna vijana wangepata ajira, kuna out-growers wa miwa wangepata soko, TRA angeongeza tax base, pension funds zingeongeza wanachama. Ripple effect kibiashara na kiuchumi ni kubwa sana.

Well, kuna siku tunainuka usingizini.
 
Back
Top Bottom