Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Kama uzalishaji hautoshi yeye afanyeje???Mnazalisha kiasi gani,Unakumbuka kabisa huu upungufu uliletwa na kukataza uagizaji,wakati hatuna mikakati endelevu,kuhakikisha utoshelevu.
 
Wawaruhusu na nyie muuze kahawa huko Uganda

Ova
Thubutu! Wao hawajatuuzia miwa, wametuuzia sukari. Na sisi tuwauzie kahawa iliyosindikwa!! Tukitaka hivyo hapo ndipo picha halisi itakapoonekana, atanuna! Hata Kenya tukitaka kuwauzia unga watanuna! tulipaswa kuwauzia unga wala si mahindi. Tusipoangalia tutakuwa koloni la kuzalisha mali ghafi kwa nchi jirani. Wananchi wetu waelimishwe na wawezeshwe!!
 
Lazima pia aliombwa....Ni Bora kuchukuwa sukari ya Uganda nai watupe bomba la mafuta...

Sukari ya Brazil sisi wanatupa Nini? Dunia unaendeshwa na kanuni ya nipe nikupe....

Hata mwalimu alimkbenout alipohindua uchumi Ni mbovu na yeye Kama yeye hakuwezantena kurudi kwa beberu imf kuomba pesa....ilibidi amuachie ruksa.....sio kwamba alingatuka kwa kuamua......alingatuka kuokoa nchi....

Taratibu nadhani namuelwqa mama. Ana kawisdom flani hiv amazing....
 
Huyu mama ni mkurupukaji sana, sijui hana washauri au hao washauri ndo wanamuingiza chaka, mweeeeeh

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Nyuma yake yupo Dr.Mpango.

Ila sijawahi kuelewa kwankni viwanda vyetu vya sukari hawezi kuilisha bongo.Mbona toka tulipopiga marufuku importation ya sukari,bei yake haijawahi kushuka,halkadharika kwenye mafuta ya kula.Hii maana yake supply ni ndogo,so nadhani kwa kupunguza makali ya maisha waimport tu.Tuseme Tz viwanda vya sukari havina faida,tuwekeze kwenye viwanda vingine labda vya kusaga mahindi
 
Kaulize wakulima wa kahawa wa Kagera watakutajia
JPM hakutaka Tz tuendelee kuuza mazao yasiyosindikwa, bali tuyaongeze thamani kwa kuyasindika ndio tuyauze. Lakini majirani zetu wanapenda tuwauzie mazak ghafi halafu wao wayasindike halafu watuuzie tenà sisi kwa bei juu!! Kahawa iliyosindikwa itoke Kenya na Uganda kuja Tanzania!! Ni mjinga tu anayeweza kuona jambo hili ni sawa!! Ukiuza mazao ghafi maana yake huna ndoto za kukuza viwanda!!
 
PRIVATE sector ya Tanzania inapenda zaidi uchuuzi kuliko Uzalishaji wa viwandani

Tatizo letu private sector yetu imejaa illiterates darasa la saba na wasiosoma kabisa ndio wanaoendesha private sector

Hata ukute mamilionea ni wachuuzi tu sio producers!!! au wazalishaji wa viwanda!!! Jirani zetu Kenya Private sector wasomi ndio wamejazana kuna viwanda balaa
Huijui Kenya! Viwanda vingi Kenya ni vya mabeberu wa kigeni na mabeberu wazalendo wachache. Waliobaki ni manamba!!
 
Habari wadau!

Sasa kilio cha upungufu wa sukari kitapungua maana mama amefungua milango na kuamuru sukari iingie nchini.

Mubashara toka Kololo Uganda kupitia TBC 1 kwenye uapisho wa Rais Museveni .Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven leo katika hotuba yake amemshukuru Rais wa JMT mheshimiwa Samia Suluhu Hassani kwa kumruhusu kuuza sukari nchini Tanzania.

Asante mama tuna imani na wewe endelea kufungua milango yote iliyofungwa ili kazi iendelee.

Mitano tena kwa mama
 
Thubutu! Wao hawajatuuzia miwa, wametuuzia sukari. Na sisi tuwauzie kahawa iliyosindikwa!! Tukitaka hivyo hapo ndipo picha halisi itakapoonekana, atanuna! Hata Kenya tukitaka kuwauzia unga watanuna! tulipaswa kuwauzia unga wala si mahindi. Tusipoangalia tutakuwa koloni la kuzalisha mali ghafi kwa nchi jirani. Wananchi wetu waelimishwe na wawezeshwe!!
Umewahi peleka unga Kenya ukazuiliwa au kahawa iliyosagwa ukazuia uganda.Tusijiduni Sana hivyo.
Ujamaa umetulea vibaya umetuletea giza la kutoona fursa.Ardh tele lkn watz fukara kama sisi sio maiti ni nini sasa.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom