diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
BAADA ya Tanzania, Kenya na Rwanda kuendelea kujiimarisha katika sekta ya usa ri wa anga, Uganda nayo iko mbioni kupokea ndege yake ya abiria, ikiwa ni hatua ya awali ya kufufua Shirika la Ndege la Uganda, ambalo kwa miaka kumi halikuwa linafanya kazi. Shirika hilo linatarajiwa kupokea ndege yake ya abiria aina ya ya Bombardier CRJ-900 mwanzoni mwa mwezi ujao.
Awali, ndege hiyo ilikuwa itue Uganda mwezi huu. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Uganda, Ephraim Bagenda alipozungumza na wanahabari katika jengo la Wizara ya Kazi na Usarishaji, jijini hapa. Bagenda alisema kutokana na hali hiyo, wamelazimika kusogeza mbele uzinduzi wa shirika hilo hadi mwanzoni mwa Aprili mwaka huu, huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Yoweri Museveni.
Aidha, Bagenda alitaja sababu za kushindwa kuwasili kwa ndege hiyo mwezi huu, kama ilivyopangwa kuwa ni kutokana na Wizara ya Kazi na Usarishaji, kushindwa kuteua Mwakilishi wa Ukaguzi wa Utengenezaji (DMIR) ili kusimamia taratibu za utengenezaji wa ndege hiyo kufuatana na matakwa ya mnunuaji. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, DMIR ni mtu, kampuni au shirika ambalo huajiriwa na mnunuzi kuhakikisha kuwa utengenezaji wa ndege hiyo, unafuata vigezo vyote na unakidhi mahitaji ya usari wa anga.
Sababu zingine zilizochangia kuchelewa kwa utengenezaji hadi kukabidhiwa kwa ndege hiyo na nyingine ni kuchelewa kupatikana kwa Leseni ya Kuendeshea Safari za Anga (AOC), kutokuwa na rubani mkuu, kukosekana kwa mkurugenzi wa uendeshaji wa shughuli za anga na mkurugenzi wa matengenezo ya ndege. Shirika la Ndege la Uganda linaamini kuwa mpaka kuka mwezi ujao, vigezo hivyo ambavyo vinahitajika ili ndege kuruhusiwa kufanya shughuli za anga, watakuwa wamevitekeleza kwa kiasi kikubwa. “Tunaamini uzinduzi utafanyika mwezi Aprili mwaka huu kwa sababu hadi kuka Februari tuna uhakika tutakuwa na vigezo vinavyotakiwa ili tuweze kufanya shughuli zetu,” alifafanua Bagenda.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, Mamlaka ya Usari wa Anga (CAA) haiwezi kutoa leseni ya kufanya shughuli za usarishaji ikiwa moja ya vigezo hivyo havijakamilika. Pia usajili wa ndege husika, hauwezi kufanyika kama hakuna leseni ya kufanya shughuli za usarishaji. Vilevile hadi leo Shirika la Ndege la Uganda, halijapeleka wanafunzi wa mafunzo ya urubani ili kupewa mafunzo ya urubani. Kazi hiyo imepangwa kufanyika katika kipindi cha miezi mitatu ya Septemba, Oktoba na Novemba. “Shirika letu linahitaji marubani wapatao 36 na watapewa mafunzo katika vipindi tofauti vya miezi mitatu ya Septemba, Oktoba na Novemba,” alisema Bagenda.
Baada ya kupokea ndege hiyo, Uganda inatarajia kupokea ndege nyingine mbili mwaka huu za Airbus A330-800. Rais Museveni aliahidi kulifufua Shirika la Ndege la Uganda katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2018 hadi 2020, ambapo aliahidi kuwa shirika litakuwa na jumla ya ndege saba.
Wakati Uganda ikifufua shirika lake, Tanzania kupitia kampuni yake ya ATCL, imekuja kwa kasi baada ya kununua ndege mfululizo na kurejea kwa kishindo katika safari za ndani na nje ya nchi. Imenunua ndege sita ndani ya miaka mitatu, huku nyingine ikitarajiwa kuwasili baadaye mwaka huu. Rwanda nayo kupitia Kampuni yake ya RwandAir, imeendelea kujiimarisha na inakusudia kuongeza ndege nyingine mbili hivi karibuni. Kenya kupitia Shirika la Ndege la Kenya (KQ) ni kinara kwa usari wa anga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Burundi na Sudan Kusini ndizo pekee katika EAC, ambazo hazijajiimarisha katika usari wa anga.