Shirika la ndege la taifa la Israel kusitisha safari za ndege kuelekea Afrika kusini

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Shirika la ndege la taifa la Israel El Al litaacha kutoa safari za ndege kwenda Afrika Kusini kuanzia mwisho wa Machi, shirika hilo la ndege lilisema Ijumaa, likitaja kupungua kwa mahitaji ya wateja.

“Kutokana na hali ya usalama ilivyo sasa, kumekuwa na upungufu mkubwa wa mahitaji ya wasafiri wa Israel wanaokwenda maeneo mbalimbali, ikiwemo Johannesburg nchini Afrika Kusini,”El Al ilisema katika taarifa yake..

"Kwa kuzingatia hili, kuanzia mwishoni mwa Machi 2024, tutasimamisha shughuli kwenye njia ya Johannesburg-Tel Aviv."

Tangazo hilo linakuja muda mfupi kabla ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutoa uamuzi wa awali kuhusu iwapo itaiamuru Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza.

Kesi hiyo katika mahakama ya ICJ ni sehemu ya kesi iliyoletwa na Afrika Kusini, ikiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Israel inakanusha vikali shtaka hilo.

Afrika Kusini imekuwa muungaji mkono mkubwa wa Wapalestina katika mzozo unaoendelea, na kusababisha mvutano na Israel.
#BBC
 
Sijui ni kitu gani kimewafanya S.A wahangaike na hii kesi ambayo hata kama wakishinda hakuna chochote wataweza kuwafanya Israel kusitisha mashambulizi yao dhidi ya Palestina.

Hawa SA siku za mbeleni wanaweza kujikuta wanatumia muda mwingi kurekebisha mahusiano yao na Israel, na kama washirika wa Israel nao watachukua uamuzi kama huu wa Israel, hapo ndipo SA watajiona wajinga.

Watajiona wajinga kwasababu ya kesi ambayo hata kama wakishinda, bado hawana nguvu ya kubadilisha chochote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
SA sijui wametumia kiumgo gani kufikiri. Israel imezungukwa na nchi za Kiarabu za Algeria, Tunisia, Morocco, Misri, Libya, Lebanon, Uturuki, Syria, Iran,Saudi Arabia, Qatar, Yemen, Iraq...hizi zote malengo yao ni kulifuta Israel. October 7 Hamas waliwavamia Waisraeli na kuua watu 1,200 huku walisherehekea kwa kuimba Allahu Akbar, Allahu Akbar. Hivi SA hawakuliona hili? Au mauaji ya KIMBARI (genocide) yanaanzia watu wangapi kwa akili ya SA? Nchi za Kiarabu walikaa na kujadili Cha kufanya, mmoja wao aliuliza swali kwenye mkutano huo kwamba: "Ikitokea Taiwan ikaivamia China kijeshi, litakuwa ni wazo la busara?" Wengi walijibi halitakuwa wazo la busara kwa kuwa matokeo yake yanajulikana ni kuchakazwa tu. Hivyo basi Hamas wakati wanaivamia Israel October 7 wakijua matokeo yake yatakuwaje, inashangaza Hamas walikuwa wanasherehekea mauaji ya Waisraeli kwa kuimba Allahu Akbar, Allahu Akbar, Sasa wanaililia Dunia isitoshe kipondo. SA Wana akili kama za Hamas.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Du mawazo haya, Kawaambie zile nchi tatu za West Africa zimefukuza wafaransa na wao watakuwa kwenye matatizo au vipi??? Unaamini kinachoendelea kule ni sawa tu...Una moyo wa jiwe au barafu mkuu.
 
S. A ni namna nyingine ya Afrika kuonekana hatuna akili
Sijui kwa nini tunajidharau hivi
South Afrika kufungua kesi ni akili kubwa sana
Ni kupima uhalali wa hiyo mahakama
Waliona uwezekano wa kushinda kesi ni mkubwa sana
Swali je tukishinda kesi hawa jamaa watachukuliwa hatua stahiki?
Waligundua kuwa ni ngumu, kama ni ngumu basi hii mahakama itakuwa haina maana tena
Hilo ni pigo kwa wazungu walijua mambo lazima yaharibike ni nani ambaye utamshtaki tena hapo kwenye mahakama yenu ya mchongo?

Akili ya hawa wazungu ni ipi sasa umeshindwa kesi mahakamani unaenda kuzuia ndege zisiende south Afrika jambo ambalo hata wewe binafsi linakuathiri
Kwasababu wamezuia wao sio kwamba hawaathiriki na hilo ni kwamba tu hawana akili za kutosha
South Afrika wako salama sana na dunia ipo kwenye mchakato wa kukomesha mambo ya kijinga ya wazungu
Kwanza wamechanganyikiwa huko walipo hawajui hata nini cha kufanya mpaka sasa hivi
Kila wanapogusa ni pamoto hawaamini macho yao wafanye vita na nani

Wewe baki chini ya ccm milele kwako hiyo ndiyo akili
Lakini wenzio huchukua hatua kuondokana na fedheha ambayo ni gharama na lazima uwe tayari kuilipa
 
SA sijui wametumia kiumgo gani kufikiri. Israel imezungukwa na nchi za Kiarabu za Algeria, Tunisia, Morocco, Misri, Libya, Lebanon, Uturuki, Syria, Iran,Saudi Arabia, Qatar, Yemen, Iraq...hizi zote malengo yao ni kulifuta Israel. October 7 Hamas waliwavamia Waisraeli na kuua watu 1,200 huku walisherehekea kwa kuimba Allahu Akbar, Allahu Akbar. Hivi SA hawakuliona hili? Au mauaji ya KIMBARI (genocide) yanaanzia watu wangapi kwa akili ya SA? Nchi za Kiarabu walikaa na kujadili Cha kufanya, mmoja wao aliuliza swali kwenye mkutano huo kwamba: "Ikitokea Taiwan ikaivamia China kijeshi, litakuwa ni wazo la busara?" Wengi walijibi halitakuwa wazo la busara kwa kuwa matokeo yake yanajulikana ni kuchakazwa tu. Hivyo basi Hamas wakati wanaivamia Israel October 7 wakijua matokeo yake yatakuwaje, inashangaza Hamas walikuwa wanasherehekea mauaji ya Waisraeli kwa kuimba Allahu Akbar, Allahu Akbar, Sasa wanaililia Dunia isitoshe kipondo. SA Wana akili kama za Hamas.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ukiangalia SA inavyoendeshwa na matukio ya uhalifu yalivyojaa kila pembe unaona kabisa shetani katamalaki.
 
Back
Top Bottom