Ufisadi wa Nyumba za Serikali

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
297
Huu mradi wa kuuziana nyumba sio tu kuwa uliingiza serikali hasara, bali kama alivyosema mwandishi Katabazi, ni ulikuwa ni ufisadi wa aina yake. Ni wakati umefika kwa bunge/ serikali kulichunguza suala hili kama ufisadi na ikiwezekana kuzirudisha nyumba zote zilizouzwa, kwenye pool ya serikali, ili ziweze kuendelea kutumika kwa watumishi mbali mbali wa umma.


Rais anza kurejesha nyumba yako serikalini

Happiness Katabazi

UADILIFU wa serikali hautokani na hotuba nzuri za viongozi bali vitendo ambavyo viongozi hao wamevifanya na vinaonekana kwa wananchi.

Hapa nchini, ipo kanuni ya maadili ya viongozi inayosema uongozi ni dhamana.

Maana halisi ya kanuni hii ni kwamba, uongozi si mali ya mtu, wala nchi hii si mali ya kiongozi, bali vyote viwili ni mali ya wananchi.

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa Serikali ya Awamu ya Tatu na Awamu ya Nne, imeshindwa kutafsiri kanuni hii kwa kivitendo, badala yake viongozi wa CCM wanaamini kwamba uongozi wa nchi ni mali yao, na hakuna binadamu mwingine anayestahili kuupata. Pia nchi hii ni mali yao na wanaweza kufanya watakavyo.

Wanaweza kuuza mali ya serikali na kuuza nchi yenyewe bila kuulizwa na mtu. Aina hii ya mtazamo tumeiona katika uamuzi wa kuuza nyumba za serikali.

Jambo hili limepigiwa kelele sana na watu wenye heshima na maadili mema, wakisema mtumishi wa umma, hawezi kuchukua nyumba ya mwajiri wake na kuifanya yake au hata kuiuza.

Kitendo cha viongozi wa serikali ya CCM kujigawia nyumba za serikali ni aina nyingine ya ufisadi.

Nyumba zile zilianza kujengwa wakati wa mkoloni, zikaongezewa na uongozi wa Awamu ya Kwanza wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Awamu ya Pili.

Haikumithilika kamwe katika awamu hizo mtu kujiuzia nyumba za serikali, lakini, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, tuliyeambiwa kuwa ni ‘Bwana Msafi’, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuvunja mwiko huo.

Alijichukulia nyumba iliyopo pale Sea View, Upanga na kisha akawaruhusu wenzake wachukue nyumba walizokuwa wanakaa.

mawaziri, makatibu wakuu, majaji na wakurugenzi, kila mmoja kwa nafasi yake alitafuta nyumba na kuinunua. Nyumba nyingine zilikarabatiwa kwa mamilioni ya fedha za walipa kodi na kisha zikauzwa kwa bei chee.

Je, ni halali nyumba ikarabatiwe kwa sh milioni 300 halafu ije kuuzwa kwa mtumishi wa serikali kwa milioni 30 au 40, tena fedha zenyewe anazilipa kwa awamu?

Kichekesho zaidi ni pale familia nzima, yaani baba, mama na watoto wawili eti kwa vile wote wanafanya kazi serikalini, kila mmoja amenunua nyumba ya serikali. Huu kama si ufisadi ni nini?

Jambo hili lilifanyika kwa usiri mkubwa bila kupata idhini ya Bunge. Tunashangaa hadi sasa hakuna hoja iliyowasilishwa bungeni kujadili ufisadi huu.

Tuelezane ukweli kwamba nyumba za serikali zimejengwa kwa kodi ya wananchi. Si halali watumishi wa serikali kugawana nyumba hizo kwa madai kuwa eti wameuziwa. Huo ni wizi.

Rais Jakaya Kikwete aliiga kampeni za washindani wake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwamba endapo ataingia Ikulu, atazirejesha nyumba hizo.

Mara baada ya kuchaguliwa, Kikwete alilitangazia taifa kuwa yeye amekubali kuuziwa nyumba ya serikali baada ya kulazimishwa, lakini alilaani mpango mzima wa kuuza nyumba za serikali, kwamba ulikuwa mbovu.

Kwa kukubali kuchukua nyumba ya serikali, rais naye alishiriki kwenye dhambi hiyo, akawa mmoja wa waliozawadiwa nyumba hizo.

Rais aonyeshe mfano, aanze kwanza kurejesha serikalini nyumba yake ili wengine wafuate. Watanzania wamechoka kuwalipia viongozi na watendaji wa serikali mabilioni ya fedha kwa kuishi mahotelini, kwani wapo wanaolipiwa sh 300,000 kwa siku kwa kukaa hotelini baada ya serikali kukosa nyumba ya kuwaweka..

Hivi huo ubadhirifu wa kodi ya wananchi utaisha lini? Je, ni lini umaskini tutaupiga vita?

Mara ya mwisho wakati akiadhimisha miaka miwili ya kuwa Ikulu, Rais Kikwete alisema, serikali bado inaendelea na utafiti wa jinsi ya kurejesha nyumba hizo. Napenda kumuuliza, lini utafiti huo utakwisha na lini kazi ya kuanza kurejesha nyumba hizo itaanza?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Simu: 0755 312859.

katabazihappy@yahoo.com; katabazihappy.blogspot.com
 
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,

Kwenye zoezi hilo, taifa letu limewanusuru viongozi wetu wasafi na waovu kuanzia kina Sozigwa mpaka kina Makani, ambao hawakuiba wakiwa madarakani, the ishu ni kuwa kuna waliouziwa ambao hawastaili, lakini sio otherwise, bila ya hili zoezi kina familia ya marehemu Mnauye, ambaye hakuiba hata senti tano ingeishi wapi?
 
Mzee ES ,

With all due respect I beg to differ with you , kwanza sio kazi ya serikali kuhakikisha kwamba familia ya Nnauye itaishi wapi baada ya kustaafu .Ndio maana alikuwa analipwa mshahara na hata baada ya kustaafu alipewa pensheni .

Pili unapozungumzia suala la free market nashindwa kuelewa kidogo . Kama kweli lengo lilikuwa kupunguza gharama kwa nini hizi nyumba hazikuwekwa kwenye free market ili soko (market) ndio ipange bei. Hivi inaingia akilini kuuza nyumba Oysterbay kwa millioni kumi ? Wakati kiwanja tuu kina worth Millioni hamsini ?
 
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,[/QUOTE]

Unajua kweli unachoongelea? Ulipitishwa lini na bunge? IMF na World Bank walihusika vipi? Kama unavyodai kila siku, tupe ushahidi, bwana!
 
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,

Shukhran kwa ufafanuzi, sasa tupatie huo ushahidi wa IMF, WB nk.

Kwenye zoezi hilo, taifa letu limewanusuru viongozi wetu wasafi na waovu kuanzia kina Sozigwa mpaka kina Makani, ambao hawakuiba wakiwa madarakani, the ishu ni kuwa kuna waliouziwa ambao hawastaili, lakini sio otherwise, bila ya hili zoezi kina familia ya marehemu Mnauye, ambaye hakuiba hata senti tano ingeishi wapi?

Personal responsibility. Sijui ulijuaje kuwa hakuiba, lakini kama aliweza kununua nyumba ya O'bay/ Masaki, basi asingeshindwa kujenga nyumba kubwa zaidi Gongo la Mboto, Tabata nk. Kule kijijini kwangu kila mtu anajijengea nyumba yake, including mwenyekiti wa kijiji.
 
Hawa majambazi ni kuwa WALIGAWANA NYUMBA za uma. Hizi nyumba ni jasho la watanzania wote. Kama kigezo ni kutumikia uma, kila mtu ametumikia uma na kila MTANZANIA alistahili kuwa na HAKI SAWA ya kununua. Kama ni mikwaju wakati wa mkoloni walichapwa watanzania wote. Kama ni kuteseka vipindi vya hali ngumu inayopitia nchi, tunateseka wote. Mbona kule kwenye vita vya kagera hawakwenda vigogo kupigana, si wao wanajiona ni watanzania zaidi!!?

Kuna familia nyingi zililazimika kuhama hizo numba na kurudi uswazi mara baada ya mzazi aliekuwa anafanya kazi serikalini kustaafu au kufariki. Hakuna alieona huruma kipipndi hicho, lakini ilikuwa ni sahihi sababu zilikuwa ni nyumba za serikali na ni kwa ajili ya KUWAHIFADHI watumishi wake. That was really fair.
 
jamani let us be realistic hakuna nyumba iliyouzwa million 10 huko masaki. kama mtu ana ushahidi aulete humu humu tuujadili.

kama kumbukumbu zangu ziko sawa, nakumbuka uamuzi wa kuuza nyumba ulipitishwa vizuri kwani nyumba zilikuwa zinaendeshwa kwa hasara. Hata ukiangalia state ya nyumba nyingi za serikali hali inatisha jinsi watu wasivyozijali ile inavyopasa.

nafikiri uamuzi ulifikiwa baada ya kujua vile waTZ wengi tulivyo kuwa hatujali kitu ambacho si chetu. na mmoja wetu hapa kishasema nyumba zimejengwa enzi za ukoloni, hivi unafikiri hata mtu akinunua hapo kajipatia nyumba ya kuishi from the get-go au inabidi aingie gharama ya kutengeneza? Issue ya muhimu zaidi ni kuwa nyumba ziliuzwa kwani zilionekana hazitoweza kuserve for long bora kupata hiyo 50M na kujenga nyingine somewhere kuliko kusubiri ianguke. na si kila nyumba iliuzwa, zile za posts za juu ziliachwa ili kuwe na makazi kwa wale wanaokuja kuchukua zile nafasi, kwa hiyo basi waliofaidika zaidi ni wafanyakazi wa ngazi za hapo kati.... msilaumu jamani kama wewe hukuwa serikalini na hukupata ya kununua usilaumu mbona wenzio tunajenga huko kitunda?
 
na si kila nyumba iliuzwa, zile za posts za juu ziliachwa ili kuwe na makazi kwa wale wanaokuja kuchukua zile nafasi, kwa hiyo basi waliofaidika zaidi ni wafanyakazi wa ngazi za hapo kati.... msilaumu jamani kama wewe hukuwa serikalini na hukupata ya kununua usilaumu mbona wenzio tunajenga huko kitunda?[/QUOTE]

Mt z Halisi

Unasema hivyo ukiwa huna ushahidi kamili. Unakumbuka siku ambayo Raisi kikwete akihutubia Wananchi wa mji wakilindoni kisiwani Mafia , Kwamba hata nyumba ya Mkuu wa polisi wa wilaya ilikuwa imeuzwa. nyumba ambayo ilikuwa mita kumi tu toka kwenye kutuo hicho cha polisi cha wilaya. Kwa hiyo mkuu wa kituo anakosa pa kuishi.

Hii si sahihi kabisa. Viongozi wanatakiwa wafanye maamuzi machungu ya kurudisha nyumba hizi.
 
MTZ- Halisi,

Mimi nadhani uitaji kuwa rocket scientist kujua ya kuwa zoezi zima la kuuza hizi nyumba lilijaa rushwa !Hivi kweli inaingia akilini viongozi kutumia office zao kama kigezo cha kujipatia hizo nyumba . Mimi naona hapo kuna conflict of interest ...Mtu anayenunua Nyumba na anaye set price ni mtu mmoja, Mtz halisi uoni tatizo kabisa katika hilo.

Pili aiingia akilini kusema ya kuwa lengo lilikuwa ni kupunguza gharama , kama kweli lengo lilikuwa ni kupunguza gharama kwa nini tena wajenge nyumba nyingine kwa ajili ya mawaziri?

Tatu kwa nini Nyumba hizi ziliuzwa kwa usiri mkubwa ? Serikali hata siku moja aioperate hivi. Kwa nini zabuni ya kuuza hizi nyumba haikutangazwa ? Kwa nini hizi nyumba hazikuwekwa kwenye soko ili serikali ipate faida kubwa ambayo ingeweza kutumika kwenye mambo mengine.

Hivi unajua kunaa baadhi ya Nyumba wangeweza kuuza hata millioni 300? Mimi naamini ya kuwa kufanya kazi serikali hakumpi mtu kibali kuwa mbele ya mstari katika kuuziwa Nyumba za public.
 
ilipotolewa idhini ya kuuza nyumba, naamini kulikuwa na malengo mazuri tu ya kuisaidia serikali. Being the way we are, yawezekana kweli wapo waliojiuzia kwa misingi tofauti. But still I stand by the decision of selling the same considering how we Tanzanians operate.
 
I don't undesrtand what you are talking about , are you saying it is okay for public officials to use their office for their own benefit . I repeat again it doesn't make sense at all for a guy who is going to buy a house to also be a appraiser.

Though the government has lost millions of dollar you still stand by that decision. When are we going to learn about accountability ? if we are not going to hold these people responsible and expose them for who they are... then who will do that ?

MTZ - hALISI , Let me ask you a simple question just to make sure that we are on the same page ..Do you understand anything about the so called conflict of interest ?
 
Nyumba ziliuzwa kukidhi mahitaji binafsi kuliko kuisaidia serilkali. Wakati tunaambiwa kuwa serikali iliuza nyumba hizo kwa kuwa zama hizi serikali haitakiwi kuwa mmiliki wa nyumba, serikali hiyo hiyo inalazimika kujenga nyumba zingine ili kuweza kuwa accommodate maofisa wake ambao baadhi wamelazimika kuishi mahotelini kwa gharama za kutisha. Nakumbuka kabla ya kura za maoni 2005 Kikwete alitamka kuwa akishinda angerejesha nyumba za serikali zilizouzwa. Baada ya kauli hii alishambuliwa sana na wenzake aliokuwa anachuana nao akituhumiwa kuwa anakuja na ilani yake binafsi badala ya ile ya chama. Ilibidi abadili kauli na kusema kuwa hata yeye anayo nyumba ya serikali aliyonunua. Lets hope that kwa kuwa sasa ni mwenyekiti wa chama anaweza kutumia influence yake kubadili hiyo ilani inayoumiza watanzania.
 
Katika sera za soko huria ambzo tunazo bongo sasa hiv, serikali huwa haimiliki nyumba, ila inakusanya kodi kutoka kwenye nyumba n property, uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulipitishwa na bunge hilo hilo kwa kushinikizwa na IMF na World Bank, under Mkapa,

Kwenye zoezi hilo, taifa letu limewanusuru viongozi wetu wasafi na waovu kuanzia kina Sozigwa mpaka kina Makani, ambao hawakuiba wakiwa madarakani, the ishu ni kuwa kuna waliouziwa ambao hawastaili, lakini sio otherwise, bila ya hili zoezi kina familia ya marehemu Mnauye, ambaye hakuiba hata senti tano ingeishi wapi?

FMES unaweza kurudia maneno yako na kuthibitisha madai yako juu ya bunge kuwa lilipitisha kwamba nyumba ziuzwe ? IMF pia una ushahidi nao ?
 
jamani let us be realistic hakuna nyumba iliyouzwa million 10 huko masaki. kama mtu ana ushahidi aulete humu humu tuujadili.

kama kumbukumbu zangu ziko sawa, nakumbuka uamuzi wa kuuza nyumba ulipitishwa vizuri kwani nyumba zilikuwa zinaendeshwa kwa hasara. Hata ukiangalia state ya nyumba nyingi za serikali hali inatisha jinsi watu wasivyozijali ile inavyopasa.


mTZ_Halisi,

Hebu tuelezee jinsi hizo nyumba zilivyokuwa zinaendeshwa kwa hasara. Ukimaliza tufahamishe jinsi utitiri wa magari ya umma unavyoendeshwa kwa faida.


mTZ_halisi said:
nafikiri uamuzi ulifikiwa baada ya kujua vile waTZ wengi tulivyo kuwa hatujali kitu ambacho si chetu. na mmoja wetu hapa kishasema nyumba zimejengwa enzi za ukoloni, hivi unafikiri hata mtu akinunua hapo kajipatia nyumba ya kuishi from the get-go au inabidi aingie gharama ya kutengeneza? Issue ya muhimu zaidi ni kuwa nyumba ziliuzwa kwani zilionekana hazitoweza kuserve for long bora kupata hiyo 50M na kujenga nyingine somewhere kuliko kusubiri ianguke.

Kwa hiyo serikali iliwatapeli wafanyakazi wake kwa kuwauzia magofu?


na si kila nyumba iliuzwa, zile za posts za juu ziliachwa ili kuwe na makazi kwa wale wanaokuja kuchukua zile nafasi

Hivi mawaziri sio ngazi ya juu? Mbona walikosa pa kukaa awamu ya JK ilipoanza kazi?

kwa hiyo basi waliofaidika zaidi ni wafanyakazi wa ngazi za hapo kati.... msilaumu jamani kama wewe hukuwa serikalini na hukupata ya kununua usilaumu mbona wenzio tunajenga huko kitunda?

Tupe data ya kuonyesha kuwa walifaidika wadogo kuliko wakubwa
 
With all due respect I beg to differ with you , kwanza sio kazi ya serikali kuhakikisha kwamba familia ya Nnauye itaishi wapi baada ya kustaafu .Ndio maana alikuwa analipwa mshahara na hata baada ya kustaafu alipewa pensheni .

Mkuu kwenye hili msalie Mungu wako, viongozi wetu wanaolitumikia taifa kwa kila walichonacho, hawawezi kuwa na muda wala hela za kuweza kujenga nyumba zao, kwani mshahara ulikuwa ni hela ngapi mpaka useme kauli nzito hivi mkuu?

Pili unapozungumzia suala la free market nashindwa kuelewa kidogo . Kama kweli lengo lilikuwa kupunguza gharama kwa nini hizi nyumba hazikuwekwa kwenye free market ili soko (market) ndio ipange bei. Hivi inaingia akilini kuuza nyumba Oysterbay kwa millioni kumi ? Wakati kiwanja tuu kina worth Millioni hamsini ?

Mkuu wangu with all due respect, hakuna nyumba Obey iliyouzwa kwa shillingi millioni 10, zote ziliuzwa kuaiza millioni 50, na juu, nyumba hazikuwekwa kwenye freemarket kwa sababu hapa bongo sio huko majuu mkuu, na pia sisi kwa ustaarabu wetu tuliamua kuwa tuwaenzi wananchi kwanza kwa kuwakopesha hela za benki na kukuza uchumi pia,

Huko US serikali ina nyumba mbili tu za rais na makamu, wengine wote hupanga kwa House alowance ndio kukuza uchumi wa taifa huko mkuu!
 
Personal responsibility. Sijui ulijuaje kuwa hakuiba, lakini kama aliweza kununua nyumba ya O'bay/ Masaki, basi asingeshindwa kujenga nyumba kubwa zaidi Gongo la Mboto, Tabata nk. Kule kijijini kwangu kila mtu anajijengea nyumba yake, including mwenyekiti wa kijiji.

Mkuu uliousema hapo ni uongo wa mchana, siku alipofariki alizikiwa kwa Makamba, kutokana na kuwa na nyumba ndogo sana ya serikali,

na besides, binamu yangu yaani mtoto wa dada wa baba yangu ameoa mtoto wake marehemu Mnauye, kwa hiyo believe me sibahatishi mkuu na ninayoyasema, mnaposema uongo kuhalalisha hoja zenu mumuogope Mungu kidogo, tena hasa mnapoongelea bina-adam aliyetangulia mbele ya haki kama marehemu Mnauye(RIP)!
 
Hawa majambazi ni kuwa WALIGAWANA NYUMBA za uma. Hizi nyumba ni jasho la watanzania wote. Kama kigezo ni kutumikia uma, kila mtu ametumikia uma na kila MTANZANIA alistahili kuwa na HAKI SAWA ya kununua.

Mkuu nyumba zimeuzwa kwa level tofauti, zimeuzwa mpaka Tabata, sidhani kama kuna waziri anaishi kwenye yale magorofa, au magorofa a Central, halafu jaribu kuwa na kauli nzuri na heshima kwa viongozi wa taifa na waliochaguliwa na wananchi wengi, hawaitwi majambazi, hata kama hukuwapigia kura,

Halafu kuwaita majambazi, ni kushusha hadhi yetu wananchi na taifa ka ujumla, kwamba tuliwachagua na sisi ni majambazi, maana huwezi kuchagua jambazi wakati wewe si jambazi, heshima ni kitu cha bure, hoja kukubalika sio lazima kuwe na matusi,

Nyumba wameuziwa mpaka masikini pia mkuu, nenda apartment za bandari hakuna waziri mle mkuu!
 
Thank You Kwa Kunikaribisha,

Tatizo Sio Mimi, Na Uwezo Wa Kujenga Hoja Upo Mkubwa..tatizo Ni Watu Wengine Hamjawa Makini Katika Kutathimini Habari Mnazopata Bila Kujua Wanaotoa Hoja Wana Malengo Gani..

Sababu Ya Mimi Kutoa Jina Langu Ni Kuonyesha Jinsi Ambavyo Vijana Wengine Au Wana Jf Wanapokuwa Washabiki Na Kuendeleza Uchochozi Na Kumuita Kila Mtu Aidha Fisadi Au Anaytetea Ufisadi..

No Jambo Forum Sio Moto Wa Fisadi, Get It..

Its A Forum.period & Ufisadi Is Not The New Tanzanian Political Agenda...sasa Hivi Ufisadi Umekuwa Ni Snowball Affect Na Ni Mbinu Ya Wa Hariri Kuuza Magazeti.. Tukosoe Lakini Tunajukumu La Kujenga Nchi Na Sio Kubomoa..

Nani Asiyejua Kuwa Waandishi Hawatoi Habari Bila Kulipwa Kidogo Dogo? Awe Waziri, Awe Nani, Ufisadi Sasa Ndio Journalistic Gold Mine Tanzania & People Dare To Threat Others (wana Jf) Kutoa Majina Ya Watu Wanaonekana Kupinga Mwenendo Huu..jf A Reality Check..sasa My Name Is Twalipo, Nice Meeting Y'all..

I Love My Country Kama Ninyi, Lakini Ufisadi Imekuwa Inatumiwa Kisiasa---understand That..fumbukeni Macho Watanzania, Mimi Ni Mtanganyika, Wengi Mumuezaliwa Baada Ya 1964, Watanzania Halisi..

Sasa Hivi Kuna Coronation Ya Former Prime Minister Mr.edward Lowassa Kujisafisha Na Watanzania Hamuulizi Kwa Nini Ghafla Huyu Waziri Mkuu Wa Zamani Anapewa Press Nzuri (pe..he Has Openned An All Out Assault On President Jakaya Mrisho Kikwete (ambaye Tofauti Na Wengi) Mimi Ninamjua Personally Toka Zamani , Na Hata Lowassa Namjua (sijisifii)..kwa Anayewajua Hawa Mabwana Angejua Kuwa Tofauti Ya Jk Na El Is Like Night & Day...the Guy Ni Mtu Wa Watu, Genuinely..na Lowassa Ni Self Centered (my Opinion & Observation)opportunistic, Anajifanananisha Na Mwinyi..

Yule Mtu Hakujiuzulu Mwenyewe, Na Hata Kura Za Ccm Nec Hazikutosha, Ni Itifaki..he Is Very Rich But Very Unpopular Na He Was Creating The Ufisadi Atmoshpere Na Aliaanza Kampeni Ya Urais Akiwa Pm, Alitaka Kuwa Vice Chair Wa Ccm, Hakupewa Akawa Bitter...he Was In London Mkataba Wa Buzwagi Ukiwa Signed Na Karamagi Ingawa Alisema Kuwa Alikuwa London Shopping..he Is One Greedy Bastard..mr.president Wanted No New Mining Contract Signed, He Authorized Sababu Ya Arrogance Na Karamagi Went Down, Na Msabaha Went Down Because Of This No Good, Nyerere -rejecting Prime Minister Who Only Thought Of Himnself & No One Else But Himself...hayo Magari 500 Aliyopokelewa Arusha Ni His Money Na Anatabia Ya Kununua Wana-habari Na Hii Ni Mbinu Anaona Inafaa

Kosa Alilofanya Jk Ni Kumtumia Samwel 6 Kumfukuza El Kazi..sam 6 Na Lowassa Hawaelewani Hata Kidogo Sababu Wote Walitaka Kazi Ya U-pm Baada Ya Uchaguzi..

Sasa Wana Jf, Fungukeni Macho, Punguzeni Ushabiki, Na Mtegemeeni Bad News Kuhusu Your President Kikwete Kama Kisasi Cha Waziri Mkuu Ambaye Alizoea Kutembea Na Magazeti Muda Wote..sasa Anaenda Israel Kuhiji, Who Cares, Reall

He Is Making & Paying Tanzanian Media To Taint The Govt, Smear Because He Has Money, Na Rafiki Yake Rostam Ana-control Magazeti From Mtanzania, Raia, Raia Mwema Etc.. Ambao Hamjarudi Nyumbani Tanzania Mjitahidi Muende At Least Once Year Or Two Years, Pamebadilika Na People Have Become That Power..so Dont Use This Forum Kuendeleza Rumors Na Tabloids-..ufisadi Haukuanza Leo, Wakati Wa Nyerere Ulikuwepo, Ila Kama Kawawa Nae Angekuwa Na Resources Za Lowassa, Basi Nae Angelipa News Media Zim- Smear Nyerer Alipomuondosha Uwaziri Mkuu Au Msuya Pia..

Dont Be Fooled People, Hii Forum Sio Ufisadi Tu Na Sisi Amani Yetu Ni Kitu Cha Bure Ila Mafahari Wawili Wakigombana Na Majani Including Wana Jf Kama Amani Itapoea..this Is How Unrest Start, Utafikiri Unakomaa Kisiasa Kumbe Ni Siasa Za Chuki Na Chuki Tu..
 
Ngurdoto ,

Sijui unaongea kitu gani, Kama kweli JK na EL they don't have anything they share in common, why did he (JK) selected him to be the prime minister? That is the profound question you were supposed to ask yourself before instigating those childish tantrum. Your story does not pass the litmus test to make a long story short what you have proposed is absolutely absurd. Please if you don't have anything to contribute in this platform just keep quite instead of exposing your biasness. EL has nothing to do with this issue " Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni".
 
Back
Top Bottom