Sijaridhishwa na uthaminishwaji uliofanywa eneo langu; Huu utwaaji wa ardhi unaofanywa na taasisi za Serikali tukimbilie wapi?

LugaMika

Member
Mar 13, 2024
38
53
Hivi hizi taasisi za Serikali zinazotapeli watu mali zao haswa Ardhi tuzilalamikie wapi?

Nina kesi ya Ardhi mwaka wa tatu sasa mahakama ya mwanzo Dodoma na haijawahi sikilizwa.

Eneo langu lipo Dodoma mjini, Mtuma lina hekari 3, na Nyumba 2 zenye thamani ya Milioni 82 na kisima 1 Thamani yake ni Molion 6.

Pia ni eneo lililoendelezwa kwa kupandwa mikorosho .

Lakini bado TBC na mthamini wa Serikali wanaungana na kuja na hoja ya kututaka tupokee milioni 100 kama fidia na wakati ujenzi wa nyumba kama hizo sasa hivi ni una gharimu milion 103.2.

Kweli huu ni uungwana?
 
Back
Top Bottom