Ufisadi wa Kinana na Trans African Logistics Limited (TALL)

Ufisadi wa Kinana na Trans African Logistics Limited (TALL)

Status
Not open for further replies.
Hivi Mwakyembe ni mwanachama humu? kama siyo basi tumtumie SMS alishughulikie hili?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM AGOSTI 12, 2013
​


Mnamo tarehe 09/08/2013 majira ya saa 20:30 usiku Mbezi Beach, jiji ni Dar es Salaam, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama pamoja na Maafisa wa Idara ya Wanyama Pori lilimkamata Robert Dewar Umri Miaka 64, Raia wa Uingereza ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikans Logistics (TALL) Limited akiwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na nyara mbalimbali zikiwemo vipande nane (8) vya meno ya Tembo, vinyago 11 vya meno ya Tembo, meno 20 ya Simba, kucha 22 za Simba, shanga mbalimbali 15 zilizotengenezwa kwa meno ya Tembo, Ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya Mpingo na Idadi Kubwa ya vinyago ambavyo haviruhusiwi Mtu yeyote kimiliki bila Kibali cha Idara ya misitu. Jumla ya uzito aw nyara zilizokamatwa ni kilogramu 24, zenye Thamani ya shilingi milioni 118,314,900.

Vile vile alikamatwa akiwa na Mawe mbalimbali yanayodhaniwa kuwa ni Madini pamoja na Ganda moja la Bomu lenye ukubwa wa milimita 130 (cartridge artilary 130 mm).

Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano mzuri toka kwa wananchi ambao walitupatia taarifa zake kuwa anamiliki nyara nyingi za serikali nyumbani kwake na huwa anazisafirisha katika sehemu mbalimbali duniani. Baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifuatilia mwenendo mzima aw Raia huyo na hatimaye kumtia mbaroni.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani Mara baada ya upelelezi na utaratibu wa kisheria kukamilika.

Aidha, Jeshi la Polisi linawapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa walioutoa na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa, na linawaomba kuendelea na kuongeza kasi ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kukomesha biashara hii haramu ya usafirishaji wa nyara za serikali.
 
kwani jina la huyo jamaa, ni kinana, au ni msomali? au ndo yule kiongozi wa wasomali tz?

Usomali ni Taifa, kama mtanzania, somalia kuna makabila mengi kama hapa kwetu. Kumuita mtanzania msomali ni kosa, au mbaniani/bohora/khoja mwenye uraia wa tz, ukamuita mhindi ni kosa na kutokujua geography.


Nina ragiki yangu wakisomali ( mzaliwa mbeya )ambaye katika miaka ya 80 alipata fursa ya kumtembelea Hayati Nyerere," basi mwalimu akamuuliza wewe kabila gani, jamaa akajibu Msomali. Nwalimu akacheka akasema sijakuuliza taifa lako, au wewe ni raia wa somalia. Nilikuwa nataka kujua kama wewe ni Hawiya/Isihakia au Darood." ambayo ndio makabila makibwa nchini somalia.

Wengi hapa tz tunakosea sana kuwatambulisha watu kwa mataifa ambayo vizazi vyao vya miaka zaidi ya 100 yalitoka huko, wengine kama waarabu waliingia tanganyika kabla hata ya mgoni hajakimbia Afrika ya kusini haada chaka kudhulumiwa na makaburu. Lakini utaona leo mgoni ni mtanzania na wengine bado ni waarabu nk. huu ni ubaguzi wa rangi.
 
Mwingereza adakwa na nyara za serikali


na Bilal Soud




RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.

Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.

Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.

Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.

Kamishna Kova alisema kuwa matukio hayo yamekithiri nchini, ikiwamo tukio la raia wa Lebanon ambaye ni Mkurugenzi wa Home Shopping Centre jijini Dar es Salaam kumwagiwa kemikali iliyomletea madhara makubwa.

Katika hatua nyingine, watu wawili wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala wakikabiliwa na tuhuma za wizi wa kutumia silaha.

Washtakiwa hao, Abdalla Shamte (30) na Mussa Hassan (40) wanadaiwa kuiba mabati 47 na vipande 11 vya mbao, vyenye thamani ya sh 3,084,000 mali ya Dk. Justine Paul.

Washtakiwa wote walikana kosa hilo lilisomwa na Mwendesha Mashtaka, Munde Hamisi, mbele ya Hakimu Joyce Minde.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 26, mwaka huu na washtakiwa walipelekwa rumande.
 
Usomali ni Taifa, kama mtanzania, somalia kuna makabila mengi kama hapa kwetu. Kumuita mtanzania msomali ni kosa, au mbaniani/bohora/khoja mwenye uraia wa tz, ukamuita mhindi ni kosa na kutokujua geography.


Nina ragiki yangu wakisomali ( mzaliwa mbeya )ambaye katika miaka ya 80 alipata fursa ya kumtembelea Hayati Nyerere," basi mwalimu akamuuliza wewe kabila gani, jamaa akajibu Msomali. Nwalimu akacheka akasema sijakuuliza taifa lako, au wewe ni raia wa somalia. Nilikuwa nataka kujua kama wewe ni Hawiya/Isihakia au Darood." ambayo ndio makabila makibwa nchini somalia.

Wengi hapa tz tunakosea sana kuwatambulisha watu kwa mataifa ambayo vizazi vyao vya miaka zaidi ya 100 yalitoka huko, wengine kama waarabu waliingia tanganyika kabla hata ya mgoni hajakimbia Afrika ya kusini haada chaka kudhulumiwa na makaburu. Lakini utaona leo mgoni ni mtanzania na wengine bado ni waarabu nk. huu ni ubaguzi wa rangi.
somalia kuna kabila moja tu acha uongo wewe kama hujui kaa kimya. hayo uliyotaja hapo ni koo hizo sio makabila
 
Ni zaidi ya wiki sasa toka meli iiitwayo HOJIN V08 ifike na kushusha magari kwenye bandari kkavu inayomilikiwa na Katibu mkuu Kinana.Meli hii ilifika tarehe 24/12/2012. Kinachangaza wengi ni kuwa mpaka sasa hakuna release order zinazotoka ukiulizwa unaambiwa custom officer anayetoa release ni mmoja tu. bandari hii imekuwa na tabia ya kuchelewesha magari ya watu ili wanufaike na gharama za storage ambazo kwa gari za local hulipwa baada ya siku 7 na transit siku 14.

Tunaomba wahusika wa bandari walifuatilie suala hili kwa haraka iwezekananvyo. pia custom officer aitwaye ANNA kwenye bandari hii ni kikwazo hii ni kutokana na jeuri aliyo nayo kwa vile Mmme wake ni bosi TRA.

Naomba kuwasilisha.

labda magari yaliingiliana na sembe
 
Usomali ni Taifa, kama mtanzania, somalia kuna makabila mengi kama hapa kwetu. Kumuita mtanzania msomali ni kosa, au mbaniani/bohora/khoja mwenye uraia wa tz, ukamuita mhindi ni kosa na kutokujua geography.


Nina ragiki yangu wakisomali ( mzaliwa mbeya )ambaye katika miaka ya 80 alipata fursa ya kumtembelea Hayati Nyerere," basi mwalimu akamuuliza wewe kabila gani, jamaa akajibu Msomali. Nwalimu akacheka akasema sijakuuliza taifa lako, au wewe ni raia wa somalia. Nilikuwa nataka kujua kama wewe ni Hawiya/Isihakia au Darood." ambayo ndio makabila makibwa nchini somalia.

Wengi hapa tz tunakosea sana kuwatambulisha watu kwa mataifa ambayo vizazi vyao vya miaka zaidi ya 100 yalitoka huko, wengine kama waarabu waliingia tanganyika kabla hata ya mgoni hajakimbia Afrika ya kusini haada chaka kudhulumiwa na makaburu. Lakini utaona leo mgoni ni mtanzania na wengine bado ni waarabu nk. huu ni ubaguzi wa rangi.

hasira za kwa wasomali zinatokana na watu kama kinana na rage

sidhani kama watz wa chuki na kila msomali wanayemwona..
 
Kilichoandikwa mwezi Januari kimetokea August ingawa hapo katikati kuna mengi sana yametokea! Ahsante KIBANGA Ampiga Mkoloni kwa kuuzimua uzi huu. CCM hawahusiki kabisa na kadhia hii, wala katibu wao hahusikiki wala mbunge Azan hahusiki na madawa !!
 
Last edited by a moderator:
Hata kama Kinana ni mchafu sijaona maana ya kumtaja katika hili

Haya yalikuwa maoni yako ya mwezi Januari, je ina maana sasa kumtaja katika kadhia hii au bado unasimamia msimamo wako wa awali?
 
Kilichoandikwa mwezi Januari kimetokea August ingawa hapo katikati kuna mengi sana yametokea! Ahsante KIBANGA Ampiga Mkoloni kwa kuuzimua uzi huu. CCM hawahusiki kabisa na kadhia hii, wala katibu wao hahusikiki wala mbunge Azan hahusiki na madawa !!

Nadhani sasa hili tukio linatupa picha nzuri zaidi kuhusu huyu mtu anaitwa Abdulrahman Kinana. matukio haya yanatokea kuzunguka kampuni yake, kuanzia lile la meli iliyoshugulikiwa na kampuni hii kukutwa imebeba meno ya tembo, utetezi wa Serikali ukawa kwamba ile ni kampuni tu haihusiki na kilichobebwa na mteja! sasa CEO mwenyewe wa kampuni amekamatwa live. tunazidi kusogea kwa mmiliki...
 
hakika haya ni majanga kwel kwel mambo ya kinana hayo kaama wafanya kazi wanafanya haya si inamaana bosi wao ndo kabisa mpiga dili mkubwa
 
eeeh,muhudummu naomba kinana mbili baridi tafadhali
 
Haya yalikuwa maoni yako ya mwezi Januari, je ina maana sasa kumtaja katika kadhia hii au bado unasimamia msimamo wako wa awali?

Mkuu sisi mitanzania mijinga sana. Kuna watu na akili zao ndogo wanafikiri Kinana yuko pale CCM kama katibu mkuu. Huyu Msomali yuko pale kwa ajili ya biashara yake ya Pembe za Ndovu. Tuliishaambiwa na wabunge wa CHADEMA kuwa kuna Kiwanda cha kuchakata meno ya Tembo, serikali hata haikufanya uchunguzi, lakini huyu mzungu wa Kinana amekuta na pembe na meno ya Tembo ambayo ni PROCESSED. Still serikali ya CCM inakaa kimya haifanyi uchunguzi...

Msione Kinana yuko majukwaani anawaambia watanzania muikatae CHADEMA, pale anakuwa analinda maslahi yake binafsi kwa kuwa chama makini kikiingia madarakani watu kama huyu Kinana ndio watakuwa wa Kwanza kuonja utamu wa magereza. Kinana anamaliza tembo wetu hivi hivi, na sasa amehamia kwenye Simba lakini serikali inamtazama tu...
 
Ni zaidi ya wiki sasa toka meli iiitwayo HOJIN V08 ifike na kushusha magari kwenye bandari kkavu inayomilikiwa na Katibu mkuu Kinana.

Meli hii ilifika tarehe 24/12/2012. Kinachangaza wengi ni kuwa mpaka sasa hakuna release order zinazotoka ukiulizwa unaambiwa custom officer anayetoa release ni mmoja tu. Bandari hii imekuwa na tabia ya kuchelewesha magari ya watu ili wanufaike na gharama za storage ambazo kwa gari za local hulipwa baada ya siku 7 na transit siku 14.

Tunaomba wahusika wa bandari walifuatilie suala hili kwa haraka iwezekananvyo. Pia custom officer aitwaye ANNA kwenye bandari hii ni kikwazo hii ni kutokana na jeuri aliyo nayo kwa vile Mme wake ni bosi TRA.

Naomba kuwasilisha.

activist,

Are you new in this country? Hivi hujawahi kumsikia Waziri wa Uchukuzi Mhe.Harrison Mwakyembe(jembe) anavyowatia tumbo moto mafisadi wa Bandari ya Dar?

Nakushauri kama una matatizo genuine ukamwone. Your issues will be sorted out.
 
Nadhani sasa hili tukio linatupa picha nzuri zaidi kuhusu huyu mtu anaitwa Abdulrahman Kinana. matukio haya yanatokea kuzunguka kampuni yake, kuanzia lile la meli iliyoshugulikiwa na kampuni hii kukutwa imebeba meno ya tembo, utetezi wa Serikali ukawa kwamba ile ni kampuni tu haihusiki na kilichobebwa na mteja! sasa CEO mwenyewe wa kampuni amekamatwa live. tunazidi kusogea kwa mmiliki...
Kesi yake na Msigwa sijui imefikia wapi!
 
Usomali ni Taifa, kama mtanzania, somalia kuna makabila mengi kama hapa kwetu. Kumuita mtanzania msomali ni kosa, au mbaniani/bohora/khoja mwenye uraia wa tz, ukamuita mhindi ni kosa na kutokujua geography.


Nina ragiki yangu wakisomali ( mzaliwa mbeya )ambaye katika miaka ya 80 alipata fursa ya kumtembelea Hayati Nyerere," basi mwalimu akamuuliza wewe kabila gani, jamaa akajibu Msomali. Nwalimu akacheka akasema sijakuuliza taifa lako, au wewe ni raia wa somalia. Nilikuwa nataka kujua kama wewe ni Hawiya/Isihakia au Darood." ambayo ndio makabila makibwa nchini somalia.

Wengi hapa tz tunakosea sana kuwatambulisha watu kwa mataifa ambayo vizazi vyao vya miaka zaidi ya 100 yalitoka huko, wengine kama waarabu waliingia tanganyika kabla hata ya mgoni hajakimbia Afrika ya kusini haada chaka kudhulumiwa na makaburu. Lakini utaona leo mgoni ni mtanzania na wengine bado ni waarabu nk. huu ni ubaguzi wa rangi.

Ukiwa NJE ya nchi ya asili unatambulika kwa utaifa wako sio kabila
 
Msomali Kanali Abdulrahman Kinena katibu mkuu wa Chama Cha Majangili (CCM) ni jangili sugu, tishio, lililokomaa, lililokubuhu na lililoshindikana na sirikali hii dhaifu ya dhaifu baba Ritz 1
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom