Ufisadi hasa ni nini?

Ufisadi hasa ni nini?

Ukichukua maelezo, kamusi zote mbili utagundua muafaka mmoja kuwa Mtu Fisadi;
Ni Mwanadamu aliyepoteza UTU wake!..."This is human disoder"

Muathirika huwa anajisikia mtupu na aliyefilisika kimwili na kiufahamu ...
Na atajitibu au atajikamilishaje kwa kile kilichopotea ndani yake..?

Atafanya yote yaliyoelezwa kwenye kamusi...corrupt, seducer, esp of women etc
Mh Speaker aelimike kuwa Fisadi ni tatizo la kiutu na kibinadamu lenye dalili zaidi ya moja...
 
Mfano halisi wa nchi iliyotafunwa kwa ufisadi ni TANZANIA......nani anabisha????????????????
 
Nimeipenda hii kutoka kwa Mwalimu Lwaitama

----- Reply message -----
From: "Azaveli Lwaitama"
To:
Subject: MPENDAZOE ASEMA NAPE ALISHIRIKI KUANZISHA CCJ
Date: Sun, May 15, 2011 11:21 am

Mimi nadhani ndugu zangu wanahabari tunasaidia kupindisha hoja juu ya dhana ya ufisadi...Kuwa na mshahara mkubwa au kuwa na kipato kikubwa ulichopata kwa makubaliano na waajiri wako au kwa juhudi zako halali au za ndugu zako si ufisadi...Kutembelea gari la kifahari ulilopewa au kuazimwa au kununua kwa kipato halali chako au ndugu yako... ilo pekee alikufanyanyi mtu kuwa fisadi...Ufisadi, kwa maana yenye mashiko kisiasa, ni kushiriki kwenye vitendo vya kupata kipato cha siri kama malipo kwa kutumia cheo chako serikalini au katika chama tawala kufanikisha malengo yakujitajirisha kinyume cha sheria ya mtu au kakundi ka watu..Sasa ndugu yangu Nape kusema eti Dr. Slaa naye ni fisadi maana yake ni nini kimantiki? Kama Dr. Slaa ni fisadi basi kwa vile tu Chadema wamempa mshahara mkubwa kwa cheo chake cha ukatibu wa chama taifa ( ambayo si sawa na kuwa mbunge wa jimbo moja!!!!) sasa CCM wanajivua gamba kwa nini yalabi? Kama hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape basi haina maana kusambabisha uwezekano wa mifarakano ndani ya CCM kwa kutaka mafisadi wake wajiuzuru....Wanyime tu mishahara mikubwa!!!!!Eti?!!!..

Maana sasa kumbe ufisadi ni kupokea milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya chama chako cha kisiasa kitaifa eti vile uliwai kusema wabunge wajimbo moja la watu wasiozidi milioni moja wasipate mshahara "mkubwa" wa milioni 7????!!! Hii inamantiki kweli??!!! Kashfa ya EPA, rada, Richmond...makashfa yenye harufu ya rushwa kubwa kubwa ya watu wenye madaraka makubwa makubwa serikalini, sasa yanalinganishwa na eti Dr. Slaa kulipwa mshahara wa milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya ukatibu wa chama kitaifa chenye Wabunge na Madiwani na wafuasi kibao nchi nzima????!!!...Kweli kabisa hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape???

Huyu ndiye Nape anayetaka mimi na wewe tumwamini kuwa anakisaidia chama cha wakulima na wafanyakazi cha CCM kijivue gamba??? Gamba la nini kama si matajiri wanaoajiri mamia ya wafanyakazi na hivyo ni wanyonyaji lakini wameteka chama cha wakulima na wafanyakazi badal ya kuanzisha chama chao cha liberal democratic union au republican??? Gamba la nini kama si wafanya biashara wakubwa wakubwa wenye kutuhumiwa ufisadi kama ule wa EPA, Richmondi na Rada??? ...Kumbe ndugu yangu Nape tafsiri yake ya ufisadi ni kule kuwa na mshara wa milioni 7 au hata 10...Ina maana Maximo aliye kuwa kocha wa TFF na Gavana wa Benki Kuu ni fisadi vile waanapokea/walipokea mshahara mkubwa tulio wapangia sie? Kweli ndugu huyu Nape anataka tumwamini kuwa ni mpambanaji dhidi ya ufisadi? Kwa nini tusiamini kuwa lengo la uteuzi wake ni kupotosha umma juu ya dhana mzima ya ufisadi ili baadaye kusiwepo hata mmoja hatayeondoka CCM kwa kutajwa kuwa fisadi??? Yaani ufisadi ndani ya CCM utaondoka kwa kuzunguka nchi nzima tukishutumu ufisadi wa Dr. Slaa wa Chadema??!!!Maana sasa CCM itakachoitaji kufanya ni kuchapisha nakala za malipo ya mishahara ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, eti? Hapo kweli sasa mafisadi watabaki akina Dr. Slaa na Gavana wa Benki Kuu, na Mkurugenzi Mkuu wa TRA, siyo?Tuache utani bwana!!!!Nape? Unatukatisha tamaa sisi CCM wafu!!! Tulidhani kumekucha kumbe bado giza totoro?!!
Wakatabahu,

Mwalimu Lwaitama
 
hoja nzito, Nape itabidi atafakari upya, vinginevyo, atazidi kujidhalilisha!
 
kama ana masikio na asikie.. somo/ufafanuzi/uchambuzi mzuri toka kwa mwalimu lwaitama!
 
Jamani msipoteze mda kuhusu huyu kilaza Nape hana jipya hata Makamba ana nafuu, juzi alikuwa Kijiji cha Ngamu Singida (v), hakuna cha maana alichoongea zaidi ya kumpaka Dr. SLAA eti Malaya, fisadi, ameasi kanisa, ooh aliba kura ndio maana ccm ilishuka....
Mi namshangaa kwanza uchaguzi umepita lakini inaonekana Nape ndo kwanza ameanza kampeni... Mi nafikiri kazi anayotakiwa kufanya ni kukijenga chama upya kwa maana ya kutoa SERA ambazo zitawashawishi Wananchi kurejesha Imani kwa chama chake na sio kutoa porojo na matusi yasi na tija kwa taifa.
 
Mwalimu Lwaitama,usihangaike na mwanaCCJ Nape. Uyu ni mtu mwenye uwezo mdogo sana kisiasa. Si mtu wa kulisumbua akili taifa. Bora mr makamba mpayukaji kuliko jasiri ujinga uyu.
 
ninakushukuru sana mwalimu wangu Azaveli Lwaitama. Kila wakati najivunia kupita kwenye mikono yako kitaaluma.
 
Elimu ya bure kwa nape.
Ni hiari yake kuipokea ama kuiachia mbali na kuukumbatia ujinga wake.
 
Wadau naomba kuuliza dr azaveli lwaitama anafundisha kozi gani udsm?

Kwasababu naona ni dokta wa ukweli kwasababu amekuwa akialikwa kwenye mdidahalo mbalimbali inayozungumzia changamoto za nchi yetu.
 
kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu
 
kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu

Tamaa na wivu wa nini au kuhusu nani? Lwaitama hata asingekuwa na PHD wengine tungemuita DK!!
 
kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu

Tuna wakina lwaitama wachache sana nchi hii'kumbuka wakati wa uchaguzi alivyokuwa akitoa analyist za siasa'ana akili timamu halafu ni msomi mzuri'
 
kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu

Una matatizo ya ubongo,huna uwezo wa kuhoji uwezo wa Dr Lwaitama hata kidogo na elimu yako ya shule ya msingi....nenda katibiwe kwanza ndio utoe comments hapa JF...
 

Una matatizo ya ubongo,huna uwezo wa kuhoji uwezo wa Dr Lwaitama hata kidogo na elimu yako ya shule ya msingi....nenda katibiwe kwanza ndio utoe comments hapa JF...
Umemaliza. Nilitaka nimjibu hivi hivi. Inawezekana hata shule ya msingi hakumaliza.
 
Afadhali mmenisaidia coz alishanitia hasira huyo anayedoubt elimu ya doct lwaitama!ana phd na amenifundisha commctn skills nikiwa first year UDSM. Ni m2 mwenye uchungu na hii nchi.
 
kualikwa kwenye midahalo haimaanishi eti wewe ni dr wa ukweli yule ni mtu mwenye tamaa na wivu wa umaarufu
Sio wewe ndio unamuonea wivu kwa kuwa ni Dr wa ukweli na ni timamu kuliko JK.

Dr Lwaitama is a senior lecturer, Philosophy Programme (Unit), University of Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom