Ufisadi hasa ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi hasa ni nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 31, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Leo nimekaa na kuwaza kidogo kwa sababu katika pita pita yangu nimekutana na mfanyakazi mmoja wa ngazi ya juu ambaye anasema akiitwa fisadi ni kama "promotion" na hivyo kuandikwa magazetini ni sifa ya aina fulani.

  Hofu yangu ni kuwa mtu kuitwa "fisadi" kunaanza kuwa kama kumwambie mtu "duh, jamaa mshenzi sana".. kwa maana nzuri kwamba jamaa amechangamka sana katika mambo yake.

  Sasa naomba tuweke vitendo ambavyo tunaweza kuviita ni vya kifisadi? Je ni vitendo vya sifa kuwa fisadi?
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  1. Fisadi ni mtu anayewambia watanzania kula nyasi ili ndege mbovu ya rais inunuliwe - Mramba

  2. ....
   
 3. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #3
  Feb 1, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Wenyewe wameu-define hivi:

  "utapeli, udanganyifu mkubwa unaoleta hasara kubwa kwa nchi.."
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  MwK, hivyo fisadi anaweza kuwa wa maneno tu?

  Kitila, ina maana ufisadi lazima uhusiane na ulaghai wa aina fulani?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Feb 1, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Fisadi ni lijitu linalofuja mali za umma bila aibu wala huruma yoyote kwa wanyonge na watu wengi walio mafukara. Kama lijitu limejipatia mali kwa njia za udanganyifu halafu linaishi maisha ya hali ya juu bila kusutwa na dhamiri kila linapoona watu wakihangaika na maisha, hilo ni lifisadi.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  ....Na nini maana ya fisadi kiwembe
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Feb 1, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Kamwulize mamako atakwambia...
   
 8. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanakiji kazi unayo

  Kila mada unayoanzisha hazifiki post kumi lazima kuna a****s za namna fulani kulikoni wana JF
   
 9. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Fisadi ni neno la kiarabu(Fasad) ambalo maana yake ni,

  The Qur'anic term for corruption is al-Fasad. It means spoiling the order, disturbing the balance of justice by greed, self-interest, deception and double talk. The Qur'an has used this word about 50 times. Al-Fasad could be in morals, in values, in social system, in family system, in educational system, in economics, in politics or in human relations in general.

  Al-Fasad appears when people follow their lusts and vain desires, when they try to twist the truth and distort the facts. Instead of following the Truth and the Guidance from their Lord and Creator, they ignore and turn away from His message.

  http://www.isna.net/services/library/khutbahs/as-fasad.html

  Mkjj naona meya wenu ameomba msamaha na kukubali makosa, inakuwaje viongozi wetu hawana utamaduni huo?
   
 10. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #10
  Feb 1, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Nyani, vipi tena mbona huyo jamaa umemshukia hivyo?!
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Tafsiri yoyote ya ufisadi based on how we can describe kwetu watanzania ni lazima ijumuishe hayo hapo juu!
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nimekarabati maana kutoka kwenye neno asilia la Kiarabu.

  Al-Fasad(Fisadi) appears when Government official,using their position and power entrusted by people, follow their lusts and vain desires to twist the truth and distort the facts for personal benefit.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 1, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimeuliza hivyo kwa sababu kuna dalili kuwa tunapozungumzia ufisadi watawala wetu wanafikiri tunazungumzia rushwa tu. Ndio maana walipochunguza mara ya kwanza mkataba wa Richmond walikuja na majibu kuwa "hakukuwa na rushwa".

  Kumbe ufisadi ni zaidi ya kutoa na kupokea rushwa, je yawezekana kuwa ufisadi hutokana na mweleekeo wa mawazo ya mtu au attitude of the mind? Yawezekana mtu akakulia ndani ya ufisadi kiasi kwamba hajui njia nyingine ya kufunction?
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Feb 1, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Think about indifference...
  Think about lack of integrity...
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Ni sawa kabisa,inaonekana kama ni ideology ambayo inabidi tuanzishe vita dhidi yake!kwasababu ni kama ugaidi tu!Ni vita ambavyo kizazi hiki hakina budi kuanza kupambana!Ili kizazi kijacho kijue kwamba tulipigana vita dhidi ya ufisadi..na tulishinda vita hivyo!
   
 16. PainKiller

  PainKiller Content Manager Staff Member

  #16
  Feb 1, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 2,739
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Unnecessary comment. Please refrain!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  mimi namtaka mamako aniambie...
   
 18. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu sio ishu.au mmetumwa??
   
 19. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nimeamua kutoa darasa kuhusu hizi mnazoita kamusi ambazo kwa kiingereza huitwa "dictionary". Naamini wanopenda tujione hatuko sahihi kimbilio lao ni kamusi.

  Lakini wasidhani hizo kamusi sisi hatuzisomi na nitakapomaliza hii post ndipo tutaona kuwa Dr. Slaa alikuwa sahihi alioptumia msamiati huo na wanaotaka tuubadilishe ni wavivu wa kutafiti.

  Hapa nilipo nimeshikilia "Oxford Advanced Learner's Dictionary-New 7th Edition". Kwenye ukurasa wa vii utaona Proffessor Henry Widowson ameandika foreword akieleza mabadiliko ya maneno. Ameeleza kwamba first edition ya dictionary kama hii ilitoka miaka 250 iliyopita.

  Hivyo akawaasa wasomaji wa hii edition kwamba wasishingae kukuta edition hii maneno yana tafsiri tofauti na zile previous editions.

  Maana yake ni nini? Anakiri wazi jamii ndiyo yenye mamlaka ya kubadili maana na matumizi ya neno. Inaelekea mama Makinda hajui au hasomi vitu rahisi kama hivi.

  Tunajjijua watanzania ni wavivu kil sekta na huenda uvivu huu umewafanya hata walio-update kamusi kushindwa tafiti hizi ndogo.

  Wana-kiswahili wasingekuwa wavivu wa kutafiti leo hii neno "walokole" lingekuwa limeshaingizwa kwenye kamusi.

  Nimalizie kwa rejea nyingine ambayo ni "A standard Swahili-English Dictionary, Edition 2008" kwenye ukurasa wa 97. Humu neno fisadi limetafsiriwa kwenda kwenye kiingereza kama ifuatavyo:

  Fisadi: a corrupter, especially of women, seducer, immoral person.

  Wote tuchambue definiton hii.

  Maneno ya msingi ni yale niliyoyakolozea na rangi ya red. Hivyo neno corrupter, seducer, na immoral person ni maneno yanayojitosheleza kwa kutoa definition ya neno fisadi.

  Mbele ya neno corrupter kuna statement isemayo especially of women. Basi hapa ndipo wengi wanataka tukazanie kama ndiyo maana mpya ya neno fisadi lakini wanaofanya hivyo ni kwa mapenzi yao na si mapenzi ya dictionary.

  Ingekwa ni mapenzi ya dictionary basi hapa pangeandikwa {a corrupter of women}, lakini hapa ni wazi pameandikwa {a corrupter, especially of women}.

  Tofauti hapa ni kwamba neno ?? ni msisitizo unaoonyesha kwa mara nyingi fisadi inamaanisha ku-corrupt mwanamke. Hii ni tahadhari kwa mtumiaji kwamba asiishie kudhani fisadi ni corrupter tu bali kuna sehemu ataenda na kukuta fisadi ina maana ya kuchukua mwanamke. Na hapo ni kumchukua mwanamke yeyote, awe ameolewa au hakuolewa.

  HIvyo hii statement especially of women hata isingekuwepo isingefuta maana ya kwanza yaani fisadi ni corrupter. Ndiyo maana kwenye neno immoral hakuweka gender emphasisi yoyote kwani immoral ni mtu asiye muadilifu.

  Tukumbuke kwamba Dr. Slaa alitumia msamiati huo pale Mwembeyanga. Mnaotaka tuamini maana mpya ya ufuska basi watajwa wale walitakiwa kufungua mashtaka kwa kesi ya kusingiziwa ufuska kama waliona cha moto kufungua ya kukashifiwa kwa fedha za EPA.

  Kesi ingekuwa rahisi sana. Ni kiasi cha advocate kumuuliza Dr. Slaa ebu taja wanawake waliofanyiwa ufisadi na mafisadi unaowadai. hakuna aliyedokeza kushitaki kwa dai hilo badala yake waote walikazania kutishia kushtaki kuhusiana na fedha.

  Mimi nimefurahishwa na kauli ya Spika wa zamani Samwel Sitta alipomwambia Anna Makinda kwamba bunge la sasa hivi lina changamot kubwa. Moja ni kwamba sasa hivi watu wana uelewa mkubwa. Sitta alijua anamaanisha nini nadhani hakutaka tu lakini angeweza kusema yeye mwenyewe yalimkuta alipoletwa hoja ya EPA akaipga chini et kwa vile ni ushahidi wa internet.

  MImi naona hapa Sitta anakiri kabisa usidhani watu kushinda kwenye Jamii Forum au blogu hawana kazi. Hukohuko ndiko kwenye vyanzo vya uelewa na vyanzo vya kuumbuana.

  Haikupita masaa mama yetu (kimuri ni mama yangu) Anna Makinda hakuzingatia ushauri wa Sitta akaja na definition yake ya ufisadi. Inaelekea Anna Makinda haju mitandano ina-search haraka na haikupita siku nzima watu tayari wameshafukua hotuba yake ya mwaka juzi alipowakemea wanaowatetea mafisadi.

  (Link hii hapa: www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/7/habari3.php)

  Huyu mama yetu na wengine dada yenu huu ni mfano tosha kuwa akicheza ni kizazi chetu matokeo yake ataona jamii inamchukia wakati ni yeye mwenyewe anashindwa kuwa muangalifu.

  Hata waiosoma JF si lazime waje humu. Kauliza zake mbili ni rahisi kuzituma kwa marafiki walioko kwenye simu yako na kama hawaamini kuwa Makinda aliwahi kutaja vile basi waape na website kwenye simu zao ili wakienda internet cafe wakajionee na kama simu zao zina internet mchezo unaisha mapema.

  Na nyinyi mnaotete humu JF, mara ningine mnadanganyika na majibu ya mkato na utani au matusi yasiyo na hoja. Matokeo yake mnadhani JF ni mfuriko wa kigenge cha wasio na hoja.

  Zinapokuja data kama hizi sijui utetezi wenu unakuja kwa misingi gani.

  Narudia mama Makinda ajue kwamba dunia ya sasa hauwadanganyi watu hata kwa saa moja kama ulishawahi kutoa kauli tofauti hata miaka 10 iliyopita, na kusoma vitabu wapo tunasoma asivyodhani.
   
 20. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #20
  Nov 14, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Swahili to English - 10 results in 1.83s.
  5 suggested literal translations
  • corrupt person
  • libertine
  • seducer
  • destroyer
  • evil person

  5 definitions
  fisadi (fisadi) { corrupt person } noun detailed view
  fisadi (fisadi) { libertine } noun detailed view fisadi (fisadi) { seducer } noun detailed view fisadi (fisadi) { destroyer } Swahili: fisadi

  [​IMG]
  Noun Class/Verb Class 5/6an
  Part of Speech noun
  Terminology general
  English Plural corrupt people
  English Headword corrupt
  English Word corrupt person
  Regular Plural mafisadi

  [​IMG]ReviewedCite
  fisadi. . In Swahili. Retrieved 12:44 AM June 23rd, 2008, from fisadi - Swahili | fie.nipa Dictionary
   
Loading...