Ufisadi hasa ni nini?

Umenena Askofu! Mabadiliko ni sasa... ushirikina ni dalili ya umasikini uliokithiri...
 
Aibu ( Shame)
Mafisadi (Mambo ya aibu)

Unaweza kuitwa fisadi kwa

1:Kushiriki '/Kutenda'
2:Kuwezesha
3:Kunyamazia

MTU hatari anayenyamazia ufisadi huku wengine wakiumizwa' hafai Nimeandika haya baada ya kuona Magufuli anawaambia watu wawazomee Mafisadi

Nikajiuliza ni wale waliokata majina ya wengine na kumpitisha yeye awe Mgombea ili akipata Urais kawalinde wao kwa ufisadi walioufanya wakati
Magufuli akinyamazia kwa miaka 22 serikalini ?

Hata Kama Ana nia nzuri atawezaje ndani ya (Mfumo) Ccm ambalo ndilo tatizo LA msingi LA umasikini wa Tanzania ?

Toka Kampeni Hakuna Mahali popote Magufuli ameahidi kupambaba Na ufisadi Unaowatesa watanzania wa Richmond 'Epa' Meremeta'Buzwagi uuzwaji wa Nyumba zaWananchi ;Dawa za kulevya Na Nyara za maliasili kama tembo nk

Anachofanya ni kuungaunga MANENO ya ufisadi wa wizi wa kuku Na vibaka kwenye Halimashauri ambako anajua atakamata dagaa Na wala Sio wale

Watuhumiwa wakubwa waliomuwezesha kufikia hapo alipo !!

Kubwa zaidi aliyebebwa hajui mwendo wa Safari !!

Kwa maoni yangu Mimi Leo Ni kujidanganya mwenyewe kudhani Kila Meneja anaweza kuwa Msimamizi Na kiongozi ?
 
Ninaomba kwa wenye ufahamu mpana watupe tafsiri sahihi ya neno "FISADI" Tafsiri hiyo itatusaidia watanzania kujua maana sahihi kuliko sasa kwani neno hili limekuwa linatumika isivyo sahihi.
 
Ndugu wana jamii nimekuwa nafuatilia sana matamko ya watu Juu ya neno fisadi lakika sijapata maana take sahihi naomba nifahamishwe pamoja Na wengine.Pia nimekuwa nasikia Fulani fisadi au hao ni mafisadi je ili uitwe fisadi unatakiwa uwe Na sifa zipi au umefanya nini?Naomba ufafanuzi wenu.
 
Wadau naomba nipatiwe tafsiri ya neno Fisadi.Na je ili uwe au uitwe Fisadi unatakiwa uwe na sifa zipi. Nadhani tukipata hiyo tafsiri tutajua fisadi ni nani tofauti na sasa mtu akiamua kukuita fisadi anakuita hata kama huna sifa za kuwa Fisadi.
 
Sina uhakika hasa na maana ya hili neno hasa linapotumiwa na wanasiasa. Nadhani ni sifa ya kisiasa anayopachikwa mtu anapoonekana kukinzana kimtazamo na wanasiasa wenzake.
 
Kwa anayejua maana ya neno UFISADI atufahamishe Kwa watanzania walio wengi hawajui maana ya neno hilo hali ambayo inawafanya walitumie hata pasipo stahiri.
 
Back
Top Bottom