SoC03 Ufanisi mzuri katika huduma za afya

Stories of Change - 2023 Competition

King Muchachu

Member
Jun 8, 2023
6
7
Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha huduma za afya ikiwemo kuja na sera mbalimbali zinazohusu huduma za Afya lakini bado imeonekana kuna changamoto ambazo hazijapatiwa ufumbuzi ambazo zinaendelea kuathiri wagonjwa ambao wengi hali zao za kipato ni duni. Upatikanaji wa huduma bora za Afya zinatakiwa kuwalenga watu wote kwa ubora unaotakiwa bila kutazama heshima, muonekano, hitikadi za kisiasa au hali ya kifedha bila kuathiri makundi maalumu.

Kumekuwa na huduma zisizo ridhisha katika hosipitali nyingi za serikali na baadhi ya hosipitali binafsi. Hosipitali nyingi za binafsi zimekuwa zikifanya vizuri kwasababu ya kuogopa kuwajibishwa na serikali na pia kujiweka vizuri katika ushindani wa utoaji wa huduma ili kuvutia wateja {wagonjwa} hali inayo sababisha hosipitali nyingi za binafsi kutoa huduma nzuri ukilinganisha na zile za serikali. Pia hosipitali binafsi zimekuwa zikifuatilia kwa karibu mienendo ya wafanyakazi wake ili kuhakikisha kunakuwa na ubora wa huduma zitolewazo na kituo husika ili kuendelea kuvutia wateja {wagonjwa} katika kituo husika.

Wanatambua kuwa wasipofanya hivyo watashindwa kuendesha kituo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara lakini hii ni tofauti kwa vituo vingi vya serikali ambavyo utoaji wa huduma umekuwa kama hisani badala ya wajibu kwani ni mahali pekee ambapo mgonjwa anatakiwa kunyenyekea muda wote kutokana na maudhi ya baadhi wa wahudumu wa Afya na pia muda mwingine hakuna lugha nzuri kwa wagonjwa hii inaweza kusababishwa na kutokuwa na usimamizi wa karibu kwa wafanya kazi au pengine wanaona serikali itawajibika kuwalipa kila mwisho wa mwezi sababu mishahara yao haitegemei mapato ya kituo husika kama ilivyo kwa hosipitali binafsi. Je, tunawezaje kuboresha huduma za Afya serikalini?

Serikali inatakiwa kuboresha mazingira ya wahudumu wa Afya ili kuwapa motisha ya utendaji mzuri wa kazi. Hii itasaidia pia wahudumu wa Afya kuipenda kazi nakufanya kazi kwa bidii hivyo kuvutia wagonjwa kutibiwa katika hosipitali za serikali sababu ya huduma nzuri na wala sii kwasababu ya unafuu wa gharama kama ilivyo kwa vituo vingi vya serikali.

Serikali inatakiwa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi wanaopata huduma katika kituo chochote cha serikali (kitakacho chaguliwa) ili kupima ufanisi katika huduma za Afya zinazotolewa na hosipitali za wilaya, vituo vya Afya au zahanati zitakazo chaguliwa, kupitia wananchi ambao ndio walengwa/wahanga wakubwa serikali inaweza kutambua kwa haraka zaidi maeneo ambayo yanahitaji maboresho, pia itakuwa rahisi kuwawajibisha viongozi ambao hawakutimiza wajibu wao katika kuwatumikia wananchi.

Serikali inatakiwa kuajiri wataalamu sahihi katika kila idara ya Afya na kwamba kila mtaalamu wa Afya atatakiwa kufanya kazi kulingana na ujuzi wa fani husika aliyoisomea. Mfano kwasasa serikali imekuwa ikiwatumia wauguzi kufanya shuhuli za Maabara katika baadhi ya vituo vya serikali hali ambayo inashusha ufanisi katika matibabu ya mgonjwa, zaidi ya asilimia sabini 70% ya matibabu ya wagonjwa yanategemea uchunguzi wa maabara hivyo kuwepo kwa watu wasio husika katika fani hiyo kunachangia kudumaza huduma za Afya nchini, madhara yanayo weza kujitokeza ni pamoja na kuchelewa kupona kwa wagonjwa au kutokupona kabisa sababu ya kupatiwa majibu yasio sahihi, usugu wa dawa utokanao na majibu yasiyo sahihi yanayo pelekea matibabu ya ugonjwa usio sahihi hali hii pia hupelekea gharama za matibabu kuongezeka kwa wagonjwa na wakati mwingine wagonjwa huweza kupoteza maisha.

Ikumbukwe mapema tarehe 22/10/2022 Jamii Forums kupitia mitandao yake ya kijamii waliweza kuandika taarifa yenye kichwa cha habari kilicho someka “WAGONJWA WASIOTIBIKA KUTOKANA NA USUGU WA DAWA NI 59.8% NCHINI.

_20230715_154256.JPG


Na waliainisha kwa undani mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha usugu wa dawa yakiwemo matumizi holela ya dawa, upungufu wa wahudumu wa Afya hali inayo pelekea wahudumu wa Afya kulemewa, wagonjwa kukosa taarifa sahihi juu ya matumizi sahihi ya dawa kama alivyo nukuliwa akisema mfamasia mkuu wa serikali Daud Msasi.

Pamoja na sababu hizo kutoka kwa mfamasia mkuu wa serikali sababu nyingine inayo weza kupelekea tatizo hilo la usugu wa dawa kutokea ni matumizi ya wauguzi na wasiokuwa Wataalamu wa Maabara (NON LABORATORY TESTERS) katika shughuli za vipimo vya maabara.

Hali hii huweza kuchangia kwa kiasi kikubwa tatizo hilo sababu matibabu ya mgonjwa yanategemea majibu sahihi kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara, Mtaalamu wa Maabara anajukumu la kuhakikisha anatoa majibu sahihi kulingana miongozo ya taaluma yake.

Serikali inatakiwa kuainisha gharama za matibabu katika hosipitali, vituo vya Afya na zahanati zake zote zilizopo chini yake na kuzibandika katika maeneo maalumu yanayoweza kufikiwa na kusomwa na wagonjwa hali hii itasaidia kupunguza mianya ya rushwa na pia kusaidia wagonjwa kutozwa gharama sahihi za matibabu waliyopatiwa, Mfano wa huduma hizo nikama x-ray, vipimo vya Maabara huduma za kumuona Daktari pamoja na huduma nyingine zinazopatikana katika hosipitali husika, huduma hizi zikiwekwa wazi huweza kumsaidia pia mgonjwa kujipanga na kuweka bajeti nzuri kwaajili ya kupata matibabu, suala hili linaweza kuratibiwa na wakuu wa idara katika hosipitali husika.

Serikali inapaswa kuratibu mafunzo yote yahusuyo afya kwa usawa bila kuacha sekta binafsi na watu wenye taaluma husika nyuma, mara nyingi kumekuwa na ubaguzi kwenye mafunzo yanayotolewa kwa wataalamu wa Afya, simaanishi wote wapewe nafasi, ninachomaanisha hapa ni kwamba hata wale wanaopata mafunzo hayo {watumishi wa serikali} hawaleti mrejesho katika sekta binafsi ili kuhakikisha huduma za Afya zinakwenda kwa hali yakufanana (ubora) badala yake sekta binafsi zimekuwa zikijua baadhi ya mambo wakati wa ukaguzi jambo ambalo sii sawa.

Pia katika hosipitali za kiserikali kumekuwa na changamoto ya kutuma wawakilishi ambao hawatoki katika fani husika, mfano Daktari anamuwakilisha mtaalamu wa Maabara au Mtaalamu wa maabara anamuwakilisha mtaalamu wa mionzi jambo hili linapelekea kutokuwa na mrejesho sahihi wa taarifa zinazopatikana hivyo kupunguza ufanisi katika sekta ya Afya.

Serikali isisitize utoaji wa risiti katika hosipitali binafsi na za serikali hii itasaidia kukuza huduma za Afya na kuongeza ufanisi sababu fedha zitakazo kusanywa zitatumika kuboresha huduma za Afya. Serikali ianzishe kampeni zitakazo kuza uelewa kwa wananchi juu ya kudai risiti na kwamba risiti ni haki yake.

Serikali iondoe urasimu katika vitendanishi mfano vinavyo husika katika upimaji wa maambukizi hasa kwa sekta binafsi ili kuhakikisha wanavipata kwa urahisi na pia kwa wakati.

Mwisho Wananchi tunajukumu la kuhahkikisha tunatoa taarifa sahihi zitakazo saidia upatikanaji wa huduma bora hili litawezekana kwakushirikiana na viongozi wa kiserikali ambao wanapatikana maeneo yote tunayo ishi.
 
Back
Top Bottom