UEFA Champions League, Special Thread

Status
Not open for further replies.
Wataala na wachambuzi wa mpira wanasema kwavile beki wa kati, Thiago Silva, na washambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Ezequiel Lavezz, ambao wote walisajiliwa mwaka jana kwa gharama kubwa, wamekuwa mhimili kuisaidia PSG kupata mafanikio mpaka hatua ya sasa.

dalili za mvua ni mawingu, leo inaweza kuwa mwendelezo PSG ng'oa ng'oa kama walivyo wafanya Valencia ktk hatua ya 16 bora, na wanaamini leo ni wakati mzuri kwao kupata heshima ya kuwa miongoni mwa vigogo wa Ulaya.
 
Kuendelea kuwepo kwa Barca kwenye haya mashindano kunanikosesha amani sana mimi mnazi wa Madrid, nilipata nguvu ile timu ya Gang Chomba ilivyowapa wakati mgumu lakini mwisho wa siku wametepeta, sioni wa kuniepushia hiki kikombe labda kwa mapenzi ya Bwana.Wana
 
Kuna kila dalili kuwa Barcelona atafungwa leo, kwa sababu;

1/PSG watakuwa nyumbani.

2/PSG wana kocha mzuri sana kimbinu(Nakumbuka namna alivyomfanyia Pap Gardiola mwaka 2009 wakati huo Gus Hidink akiwa Chelsea)

3/PSG ilivyofanikiwa kupita hatua ya mtoano kwa kuitoa timu ngumu kwa mbinu bora za kocha.

4/PSG wana kocha mzoefu sana katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya(European Speciality)

.., nyota mpya wa PSG, David Beckham, aliyesajiliwa Janauari kwa mkataba wa miezi mitano, anaamini kwamba wanaweza kufanya vizuri, ingawa alikuwa anasema kwamba itakuwa mechi ngumu naya kuvutia' ngoja tuone utabiri wake.
 
... Update:
Vikosi vinavyotarajiwa leo ni kama ifuatavyo;-

PSG:
- Salvatore Sirigu
- Christophe Jallet
- Thiago Silva
- Alex, Maxwell, Lucas
- Marco Verratti,
- Blaise Matuidi
- Javier Pastore
- Zlatan' Ibrahimovic
- Ezequiel Lavezzi

======
BARCELONA:
- Victor Valdes
- Dani Alves
- Gerard Pique
- Javier Mascherano
- Jord Alba
- Sergio Busquets
- Xavi, Andres Iniesta
- Cesc Fabregas
- Lionel Messi, na
- David Villa.
 
Natamani nimrushie mneno usiofaa manager wa Tanesco Moro ila naogopa BAN tu, kila ikicheza Barca lazima akate umeme katikati ya Mechi sijui ni Madrid mwenzangu?
 
duu hawa psg ni noma..

Wana unoma gani hawa si kama chama lako la Chamazi tu, safari ndio imewadia hapo Camp Nou watapoteana hawa. Naombea Andunje awe ameumia sana kapumzike kidugo tupumue, kila mechi yumo utafikiri Kaseja.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom