Ligi kichelewa kuisha tatizo ni nini??

Black poison The Factor

JF-Expert Member
May 31, 2020
852
1,257
Hope mko poa wakuu na weekend hii.

Moja kati ya tatizo la kudumu sana kwenye league yetu NBC premier league ni pamoja na ratiba ya kumaliza msimbmapema.

Ukiuliza ni kwanini wanasema makombe ni mengi kwahiyo ratiba inabana,, lakini ukiangalia kwa wenzetu mfano Epl kwanza wao wana team 20 ambazo ni sawa na mechi 38. Lakini pia makombe wanayo mengi tu ila league yao inaisha mapema kuliko yetu sijui tatizo lipo wapi.

Haya ni makombe ambayo team za EPL zinashiriki.
1 EPL yenyewe
2 FA
3 carabao cup
4 UEFA champions league
5 UEROPA

Ila huwezi kukuta team ina viporo vya ajabuajabu.

ila hapa Tanzania makombe ni kama EPL ila viporo sasa ni balaa. kuna kipindi timu ziliwahi kua na viporo mpaka vitano.

Lakini pia kisimamisha michezo bila sababu maalum nayo inachangia pakubwa sana. tena kwa kigezo Cha mapumziko.

Pia Caf nao inabidi wateue siku maalum kwa ajili ya michezo ya club bingwa pamoja na shirikisho. Kama walivyofanya wenzao UEFA. Jumanne na jumatano ni UEFA champions league na alhamisi ni UEFA Europa league ingesaidia sana.

Haya ni makombe ambayo zinashiriki team za Tanzania.
1 NBC premier league
2 ASFC (FA)
3 Mapinduzi cup
4 Caf champions league
5 Caf confederation cup

ila viporo kwenye fridge havikauki. Mpaka Sasa kuna team zina michezo 21 huku zingine zikiwa na 19 ni aibu sana kwakweli.


TFF waache huruma badala yake kanuni ifuatwe.
 
Back
Top Bottom