Hata Ulaya, fainali ya Champions League huwa haichezwi neutral ground

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,713
20,472
Kuna watu wanadhani kuufuata mfumo wa Ulaya kutawezesha fainali ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kuchezwa katika uwanja ambao mojawapo ya timu husika haitakuwa mwenyeji.

Ukweli ni kwamba wenzetu wa Ulaya huwa wanakuwa wameshauchagua mji ambao fainali itachezwa, bila kujali mojawapo ya timu zitakazoingia fainali itakuwa ni ya nchi yenye mji huo au la. Mfano mzuri ni kwamba fainali ya UEFA Champions League ijayo (2024) tayari imeshapangwa kuchezwa Wembley Stadium, London bila kujali itakutanisha Arsenal (ya London, Uingereza) vs Barcelona (ya Barcelona, Uhispania), au itakutanisha timu zote mbili zisizo za Uingereza

The 2024 UEFA Champions League final will be the final match of the 2023–24 UEFA Champions League, the 69th season of Europe's premier club football tournament organised by UEFA, and the 32nd season since it was renamed from the European Champion Clubs' Cup to the UEFA Champions League. It will be played at Wembley Stadium in London, England, on 1 June 2024

The 2024 UEFA Europa League Final will be the final match of the 2023–24 UEFA Europa League, the 53rd season of Europe's secondary club football tournament organised by UEFA, and the 15th season since it was renamed from the UEFA Cup to the UEFA Europa League. The match will be played at the Aviva Stadium in Dublin, Republic of Ireland, on 22 May 2024
 
Fainali moja Ni utaratibu sahihi. Mchezo unavutia zaidi, kombe linakuwa uwanjani, mashabiki 50-50, Mshindi anafurahi kufurahia ushindi kwa uhuru. Sio unapewa kombe wamejaa mashabiki wa upinzani sababu upo kwao.
 
Siku fainali ikiwa moja tu, tutegemee nchi za kusini, kati na magharibi wakibadilishana kunyanyua ndoo
 
Africa sio Ulaya, fainali moja kwa africa lazima uwanja utakuwa ni mtupu. Tuache kukariri, sio kila cha ulaya tukifuate lazima tuangalie na mazingira ya kwetu yalivyo.
 
Siku fainali ikiwa moja tu, tutegemee nchi za kusini, kati na magharibi wakibadilishana kunyanyua ndoo

hebu tutajie adavantage waliyonayo nchi za Kaskazini ffainali zinapokuwa mbili.

Kwanini hamutaki kukubali kuwa jamaa wanaupiga mwingi? Kila mwaka mabingwa ni wao tu.
 
Wa africa tunahali ngumu za maisha. Huwez amini mechi ya Yanga na malumo kule bondeni kwa madiba washabiki wa Yanga walikuwa wengi kuliko wa Malumo kingali kiingilio kule kilikuwa bure. Kuna sehemu ukipeleka fainali za CAF hata kwa buku kuna wanainchi watashindwa kulipa.
 
Ni kweli venue inapangwa kabla ya mashindano kuanza. Ila hata ikitokea kwa mfano venue ni Wembley stadium halafu final ikawa kati ya Arsenal na Juventus, haimaanishi kwamba mashabiki wa Arsenal ndo watakua wengi kwa sababu wapo kwao.
Kinachofanyika ni UEFA wanafanya equal allocation of tickets kwa timu zote mbili. Utofauti na Africa ni kwamba sisi hatuwezi kusafiri na kwenda hata watu elfu 5 kushangilia timu huko Dakar.
Ila wenzetu wanasafiri na wanajaza uwanja. Na pia usafiri wao ni mzuri ikiwemo trains za umeme.
 
Back
Top Bottom