UEFA Champions League, Special Thread

UEFA Champions League, Special Thread

Status
Not open for further replies.
Ana miaka 25 tayari amesha vunja record nyingi zinazohusiana na football una maoni gani kuhusu huyu jamaa {lionel messi}
 
Jee c.ronaldo atamfikia? images (1).jpg
 
When you go through a
night like this all of the bad
days are forgotten, we do
not care who we get in the
quarter-finals
”
Barcelona striker David Villa
 
Barcelona hawana plan B, ndo maana hawashindi na wanatolewa kirahisi
 
Jana,mabingwa mara saba wa UCL,AC Milan waliingia uwanja wa ugenini kupambana na mabingwa mara nne wa kombe hilo,FC Barcelona. Wengi waliiona mechi hii iliyokuwa ya kukata na shoka. Matokeo ya mwisho yalikuwa ni Milan kufungwa mabao 4-0 hivyo kupigwa kumbo nje ya UCL huku Barcelona ikitinga hatua ya robo fainali.

Barcelona wakicheza nyumbani na wakiwa na kikosi imara,waliutawala mchezo wa jana hasa sehemu ya kiungo iliyokuwa ikiwashirikisha akina Xavi,Sergio na Iniesta. Dimba lilikamatwa na Barcelona.Viungo wa Milan akina Ambrosini,Montolivo na Boateng walifunikwa.Hata alipoingia Suley Muntari katika kiungo,hakuwa msaada mkubwa na tofauti katika sehemu ya kiungo ya AC Milan.

Katika ushambuliaji,Lionel Messi alituchachafya vya kutosha. Alifunga mabao mawili ya mwanzo kabla ya la David Villa na Jordi Alba lile la lala salama. Messi alikuwa akifanya atakavyo jana. Akichagizwa na washangiliaji wa uwanja wa nyumbani,Messi-mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo,alionesha kuwa bado wamo.

Mabeki wa pembeni wa Barcelona,Dany Alves na Jordi Alba,walicheza vizuri jana.Walipeleka mashambulizi makali langoni mwa Milan na kuwafanya mabeki wetu wa pembeni,Kelvin Constant na Ignazio Abate,wasiweze kupanda kwa kushambulia. Mabeki hao wa pembeni wa Milan walibaki nyuma na kushindwa kupeleka mashambulizi ya maana kwa Barcelona.

Walinzi wa kati wa Barcelona,Masherano na Pique-baadaye Puyol na Pique walicheza vyema. Waliwadhibiti washambuliaji wetu akina El Shaarawy,Robinho,Bojan na Mbaye Niang. Nao walitimiza wajibu wao ipasavyo. Milan hatukufua dafu jana.

Barcelona,wakicheza mchezo vutizi wa pasi,chenga na kujipanga,waliwapoteza kabisa Milan. Ifahamike kuwa,Barcelona ya Messi hukolezwa na ushindi wa Real Madrid ya Christiano Ronaldo. Kimsingi,akina Ronaldo ndio waliotuponza baada ya kuifurusha Man United kwenye mashindano haya haya. Messi afunikwe na Ronaldo? Ronaldo aende robo fainali na Messi abaki? Haiwezekani.

Messi ameonesha ubora wake.Barcelona wakashinda. Hongera zao.Sina mengi,kila mtu ni shahidi wa ubora wa Barcelona na hata Milan. Naweza kutamka kuwa Barcelona watalibeba kombe hili la UEFA

cc Gang Chomba gutierez LIVEPOOLfc Mourinho na wengineo wote
 
bora sie tulifungwa 2-1 na madrid....hao wanaojiita the most successful team in europe wamechezea kichapo cha mbwa...goli nne kulalekiiii :biggrin1:
 
"Barcelona hawana plan B,

Plan B ya nini wakati plan A inafaa!

ndo maana hawashindi na wanatolewa kirahisi"

Really?
 
wewe hebu acha ulevi.. barca wanatoka kirahisi? hawashindi?..lini hiyo ilitokea?..tuondolee ulevi wako maeneo haya...
uyo jamaa anonyesha pombe ndio maji yake anaongea pasi na kujua ameongea nini
 
tatizo la ACM ni kocha wao kuchelewesha plan B lasivyo barca wangeona cha moto
 
Jana,mabingwa mara saba wa UCL,AC Milan waliingia uwanja wa ugenini kupambana na mabingwa mara nne wa kombe hilo,FC Barcelona. Wengi waliiona mechi hii iliyokuwa ya kukata na shoka. Matokeo ya mwisho yalikuwa ni Milan kufungwa mabao 4-0 hivyo kupigwa kumbo nje ya UCL huku Barcelona ikitinga hatua ya robo fainali.

Barcelona wakicheza nyumbani na wakiwa na kikosi imara,waliutawala mchezo wa jana hasa sehemu ya kiungo iliyokuwa ikiwashirikisha akina Xavi,Sergio na Iniesta. Dimba lilikamatwa na Barcelona.Viungo wa Milan akina Ambrosini,Montolivo na Boateng walifunikwa.Hata alipoingia Suley Muntari katika kiungo,hakuwa msaada mkubwa na tofauti katika sehemu ya kiungo ya AC Milan.

Katika ushambuliaji,Lionel Messi alituchachafya vya kutosha. Alifunga mabao mawili ya mwanzo kabla ya la David Villa na Jordi Alba lile la lala salama. Messi alikuwa akifanya atakavyo jana. Akichagizwa na washangiliaji wa uwanja wa nyumbani,Messi-mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo,alionesha kuwa bado wamo.

Mabeki wa pembeni wa Barcelona,Dany Alves na Jordi Alba,walicheza vizuri jana.Walipeleka mashambulizi makali langoni mwa Milan na kuwafanya mabeki wetu wa pembeni,Kelvin Constant na Ignazio Abate,wasiweze kupanda kwa kushambulia. Mabeki hao wa pembeni wa Milan walibaki nyuma na kushindwa kupeleka mashambulizi ya maana kwa Barcelona.

Walinzi wa kati wa Barcelona,Masherano na Pique-baadaye Puyol na Pique walicheza vyema. Waliwadhibiti washambuliaji wetu akina El Shaarawy,Robinho,Bojan na Mbaye Niang. Nao walitimiza wajibu wao ipasavyo. Milan hatukufua dafu jana.

Barcelona,wakicheza mchezo vutizi wa pasi,chenga na kujipanga,waliwapoteza kabisa Milan. Ifahamike kuwa,Barcelona ya Messi hukolezwa na ushindi wa Real Madrid ya Christiano Ronaldo. Kimsingi,akina Ronaldo ndio waliotuponza baada ya kuifurusha Man United kwenye mashindano haya haya. Messi afunikwe na Ronaldo? Ronaldo aende robo fainali na Messi abaki? Haiwezekani.

Messi ameonesha ubora wake.Barcelona wakashinda. Hongera zao.Sina mengi,kila mtu ni shahidi wa ubora wa Barcelona na hata Milan. Naweza kutamka kuwa Barcelona watalibeba kombe hili la UEFA

cc Gang Chomba gutierez LIVEPOOLfc Mourinho na wengineo wote
Nimeamini methali isemayo kutangulia sio kufika,sina mengi poleni sana AC Milan na anti Barcelona wote,hata mimi nilikuwa hivyo kule Turati,usilie kwa uchungu sasa imewatachi sana mimi leo robo fainali :rockon:
 
Ushindi wa FC Barcelona jana wa goli 4 kwa 0 dhidi ya AC Milan ki ukweli ulikuwa kama dhidi ya dunia. Wenye mdomo mrefu wote sasa kimya na hata baadhi ya vyombo vyetu vya habari hapa nchini hawaipi uzito sana habari hii na kujikita kwenye mechi ya leo kati ya Bayern Munchen na Arsenal!
Sie hatufurahii kumfunga AC Milan (kushinda ni jadi yetu) bali tunafurahia kuwaziba midomo wote waliokuwa hawatutakii mema.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom