UDSM ndio chanzo cha mfubao wa Elimu Tz

Nimekupata ndugu yangu.
Sasa basi tuingie katika mjadala wa uboreshaji wa elimu yetu ya juu, tafadhali ingia katika Jukwaa la Elimu na tuendeleze mada. Mchango wako unahitajika sana.

Ni ngumu kuongelea jinsi ya kuboresha elimu wakati bado ndani ya hiyo elimu kuna watu wenyejitihada za kuididimiza hiyo elimu,watu wasiokubali ukweli,watu wenye mentality zilizopitwa na wakati na hawataki kwenda na wakati.

Kwanza kitu cha kwanza ni watu wakubali kubadili hiyo mentality na wakubali kuelimika si lazima udsm ama DIT ama MZUMBE hata kwa njia ya internet mtu una elimika.
 
Mkamap,
Hapa Jf ndio jukwaa la kuwaelimisha watu kama hao. Usikate tamaa ndugu yangu. Hapa ndio pa kuwaambia hao jamaa wasiobadilika wabadilike. Weka kasoro zao zote hapa, kero zako zote, wataziona, watazisoma na kuzielewa na ninaamini watazifanyia kazi. Sina uhakika na vyuo vingine, ila Udsm kuna programu ya elimu kwa njia ya mtandao inayojulikana kama "TEIL".
Kila kitu kinawezekana, tutimize wajibu wetu.
 
Mkamap,

Pole sana ndugu, inaoneka huna cha maana cha kujadili zaidi ya kujielekeza kwenye kuilaumu UDSM, hasa hasa Prof. J.R. Masuha, Ing.Grad. Dipl.Ing., Dr.Ing.(West Berlin)

Maelezo yako yote yananishwishi kuamini wewe uliwahi kupitia pale UDSM upande wa Faculty of Egineering(enzi zile), maana hata mifano yako ya kozi unatoa ya Engineering. Upo uwezekano mkubwa wewe pia ulikuwa mmoja wa wale mafresher walionyakwa..halafu baadaye ukajiunga na DIT. Kwa hiyo ulipoona Prof Masuha pia huko yupo na mambo hayakuenda ulivyotarajia ikawa ni kumlaumu huyo mtaalamu mkongwe!. Japo sina details za huo mgogoro wa DIT, lakini naweza hisi kwamba kwa kuwa Prof ni mtaaluma wa siku nyingi aliyebobea, then alikuwa akitoa mchango wake katika kuiweka hiyo institute mahali pake; mkashindwa muelewa. Kama ni mambo ya technology huyo Prof kabobea, believe me. Asingekubali kushiriki katika kuunda chombo cha ubabaishaji katika fani yake. Si mtu wa masihara, in short. Hivi ni akina nani waliochoma gari lake? Wanachuo? si dhani kama malecturers wenu walifanya hivyo. Kama ni wanachuo, hilo linaeleweka, kwani wakati mwingine wakipotoshwa hufanya vitu bila kufikiri mara mbili.
Ushauri:
kama kweli uli disco pale UDSM(Engineering) na sasa umesoma DIT..bado unayo nafasi ya kupata "Bachala" yako popote pale ili mradi ulifanya vema DIT. Conquer that hatred against USDM, it seems to be haunting you so severely!
 
Hawa watu hawa
yani pamoja nakupita hapo udsm bado hujaelewa mantiki ya hesabu hiyo???
Mie haswa nilitaka kukuambia hiyo namba kubwa ya ma phd hapo udsm mliokua mnaipambamba kwa bwebwe si kawaida ya msomi kuangalia namba kubwa na kushabikia ,hayo ya kuangalia namba yanafanywa na watu ambao hata darasa la tano hawakufika maana ndipo hesabu za sehemu na asilimia zinapoonza.

Nilitaka kukuonyesha jinsi ya kupata chuo chenye ma phd wengi ni kwa njia ya uwiano kati ya ma phd na wanafunzi.

Ama ulitaka niweke kila kitu ktk DESA ili wewe uje umeze tu?? Vingine ni mifupa ndugu yangu.

Nilitaka kukujibu naona TzPride kaniwahi.........................hivi wewe ulisomea wapi hesabu???.................no mathematician will agree from what you displayed......even from the moon trust me...........worse stil unakuja kutetea..............aliyosema TzPride yaweza kuwa sahihi kabisa........mlinganisho haufanywi kirahisi rahisi namna hiyo especally kwa route uliyoamua kuitumia ktk mambo ya elimu iliyo diverse
 
Ogah and TzPride,

nadhani mnaufahamau fika ule usemi

"do not argue with a fool because when people see you they ill not know the difference" I guess you get my drift,.............

Mkamap,

I am sorry maelezo yako toka mwanzo ni hafifu kitaaluma, kihoja, hata katika kujieleza haujatulia kabisa. Details zako na heading uliyoweka havilingani. Kama unataka kutoa changamoto ya kuendeleza elimu basi spend less time hating and more time contributing, Masua is a well respected Professor, be a better professor than him then challenge his choices and decisions that he once made there you will make a difference rather than spending time insulting people.

This is my last post to you. I need this energy more than you know!

PEACE
 
Mada hii inanikumbusha gazeti moja lilivyoelezea vita ya visiwa vya Malvina kuwa ni vipara wawili wakigombea chanuo!

Kwa nini tunakuwa sensitive mno na criticism? Kwa nini tuna personalise kila kitu? Mtu kusema UDSM kuna matatizo hakuna maana kuwa wote waliosoma au wanaofundisha pale wana matatizo! Tunabaki kushindaniana namba za PH.Ds kama vile Ph.D ndiyo kigezi pekee! Katika walimu waliokuwa na impact kubwa kwangu ni wachache sana, if any, waliokuwa na Ph.D. Kilichowatofautisha hawa na walimu wengine ni mapenzi yao na elimu, uwezo wao wa ku'inspire' mwanafunzi ili ajione nae anaweza kufanikiwa akifanya juhudi. Bahati mbaya kwetu bado kuna walimu wanaoona ni sifa kufelisha na si kuwezesha. Ndiyo maana tunashinda kuwabeza walio'disko' badala ya kuona uchungu kwa nini mtu anadisko! Tunaona elimu ni exclusive na tunaona sifa kuwa tuliweza kumudu boot camp ili na sisi tuingie kwenye hiyo exclusive club. Hivi hakuna njia mbadala ya bootcamp ili wote nasi tuelimike? Chuo alichofundisha Walter Rodney deserves better!
 
Mkamap,

Pole sana ndugu, inaoneka huna cha maana cha kujadili zaidi ya kujielekeza kwenye kuilaumu UDSM, hasa hasa Prof. J.R. Masuha, Ing.Grad. Dipl.Ing., Dr.Ing.(West Berlin)

Maelezo yako yote yananishwishi kuamini wewe uliwahi kupitia pale UDSM upande wa Faculty of Egineering(enzi zile), maana hata mifano yako ya kozi unatoa ya Engineering. Upo uwezekano mkubwa wewe pia ulikuwa mmoja wa wale mafresher walionyakwa..halafu baadaye ukajiunga na DIT. Kwa hiyo ulipoona Prof Masuha pia huko yupo na mambo hayakuenda ulivyotarajia ikawa ni kumlaumu huyo mtaalamu mkongwe!. Japo sina details za huo mgogoro wa DIT, lakini naweza hisi kwamba kwa kuwa Prof ni mtaaluma wa siku nyingi aliyebobea, then alikuwa akitoa mchango wake katika kuiweka hiyo institute mahali pake; mkashindwa muelewa. Kama ni mambo ya technology huyo Prof kabobea, believe me. Asingekubali kushiriki katika kuunda chombo cha ubabaishaji katika fani yake. Si mtu wa masihara, in short. Hivi ni akina nani waliochoma gari lake? Wanachuo? si dhani kama malecturers wenu walifanya hivyo. Kama ni wanachuo, hilo linaeleweka, kwani wakati mwingine wakipotoshwa hufanya vitu bila kufikiri mara mbili.
Ushauri:
kama kweli uli disco pale UDSM(Engineering) na sasa umesoma DIT..bado unayo nafasi ya kupata "Bachala" yako popote pale ili mradi ulifanya vema DIT. Conquer that hatred against USDM, it seems to be haunting you so severely!

MIMI SIKUELEWA MMEANDIKA NINI.

KIJANA AMELETA MAMBO MAZURI TU NINYI MNATUMIA JANJA JANJA ZENU KUMKATISHA TAMAA. WENGINE WANAKIMBILIA KUFUNGUA THREADS NYINGINE. KAMA ULIONA INAFAA SI UNGEANZISHA MAPEMA. MMENIPA WASIWASI.

OGAH huwa ninadout sana reasonability yako, hivi hesabu aliyoweka huyo bwana unaiona ina kasoro na kwa vigezo gani? ungekuwa hujajieleza kwamba hukutokea UDSM ningedout ila sasa ninadhani hata undergraduate hujapitia maana mapenzi yako ya kuarge yamenipa wasiwasi.

ikumbukwe kuwa hii threads haisomwi na sisi tu bali hata wale malecturers wa UDSM hivyo basi tunapoargue tunaargue kwa nguvu zote ili wabadilike. kile chuo sio cha chao peke yao bali ni cha umma. pia vyuo vyote vinavyoanzishwa sio vya UDSm ni vya umma. mgawo inabidi uwe sawa.

mimi ni mwanasheria ila nimependelea yule bwana alivyoargue, unajua katika sheria ukiombwa ushahidi na ukautoa, tayari ni maksi. lakini ukiombwa ushahidi ukaanza, ohoo akimu unajua mbona yule hujamuomba wewe unaupendeleo.tayari huna lolote. hiyo ndivyo inavyoonekana kwa wale waliojitambulisha kama graduates wa udsm hapa hapa. eti hoo inaonekana wewe ulipita udsm ukakamatwa, it is imaterial ab initio. tunachotaka ni kujibu tuhuma au kukaa kimya. tunasema evasive countreclaim or evasive defence is not credited.

kama hujui inchi hii inavyokwenda kaa kimya vinginevyo tutakuona na wewe fisadi. unajua fisadi sio mpaka aibe elatu hata rushwa maonevu na kutowajibika ni mfisadi tu. sasa sisi tunajua vyuo vyetu vizuri. OGAH tafadhari ukae kimya kama huwezi kujibu tuhuma.

UDSM kuna course inaitwa PL yaani critical thinking and argumentation. nilikuwa sheria ila nilikuwa ninaingia FASS kuangalia na kujifunza chochote, sasa inamaana hapa wote zile products hazikupitia hilo somo.

mfano hesabu aliyoitoa mwanzilishi wa hii mada haina kasoro yoyote, na ninadhani yule aliyejitambulisha kama anachukua masters inabidi akubali ili kuonyesha huma kuwa kweli anachukua masters.

hapa hatuuani ila arguments ndizo zitakazomfanya mtu ajue kuwa yeye ni nani.

kwamba chuo kimefundishwa na walter rodney ni upumbavu ambao ninadiriki kuutoa hadharani kama liwalo na liwe. nijibu hivi chuo kilichomnyima WALTER RODNEY uprofessor mpaka akafariki ndio baada ya aibu wakaja kumpa ni chuo. kama unamkubari huyo Rodney mbona wao walikataa kumpa. basi rodney sio kitu. unajua kuna mambo mengi ambayo kama vyuo vingine vitakuwa empowered tutapata unafuu.

mimi ni product ya UDSM, mdogo wangu yuko sheria pia mwaka wa mwisho MZUMBE UNIVERSITY, na mdogo wangu wa mwisho yuko sheria UDSM mwaka wa kwanza, pia nina mtoto wa kaka yangu yuko UDSM mwaka wa nne. wote huja na rafiki zao either kwenye fields au kwenye holidays kufanya kazi kwenye firm yangu. mimi ndiyo ninayefahamu ninachokisema katika uwiano wa hizo elimu za vyuo tofauti. tusipayuke kama hujui unyamaze au angalia vyuo vyote kwa makini. inatia hasira watu kugangania upumbavu pasipo sababu.

tuwe wakweli na wazalendo. tuone kama nchi tutaifikisha panapohusika. tuache ubinafsi na kiburi.
 
Ni ngumu kuongelea jinsi ya kuboresha elimu wakati bado ndani ya hiyo elimu kuna watu wenyejitihada za kuididimiza hiyo elimu,watu wasiokubali ukweli,watu wenye mentality zilizopitwa na wakati na hawataki kwenda na wakati.

Kwanza kitu cha kwanza ni watu wakubali kubadili hiyo mentality na wakubali kuelimika si lazima udsm ama DIT ama MZUMBE hata kwa njia ya internet mtu una elimika.

pole sana na ongera kwa kazi unayoifanya unajua ni heri kukubali kutokuburuzwa na mawazo mgando, yale yanayotetea ufisadi kuliko kunyamazia kutokubali kuburuzwa na mawazo hayo. kazi uliyoianza ni kali sababu ilishaenea kuwa the only university in tanzani is udsm. ila kama ccm inakili kwa sasa jitihada zako zitawafanya hata udsm kukubali pia. mimi ni mmoja wa wale wanaokuunga mkono. na minavyomjua Maghembe yuko upande wetu.
 
Ogah and TzPride,

nadhani mnaufahamau fika ule usemi

"do not argue with a fool because when people see you they ill not know the difference" I guess you get my drift,.............

Mkamap,

I am sorry maelezo yako toka mwanzo ni hafifu kitaaluma, kihoja, hata katika kujieleza haujatulia kabisa. Details zako na heading uliyoweka havilingani. Kama unataka kutoa changamoto ya kuendeleza elimu basi spend less time hating and more time contributing, Masua is a well respected Professor, be a better professor than him then challenge his choices and decisions that he once made there you will make a difference rather than spending time insulting people.

This is my last post to you. I need this energy more than you know!

PEACE

Bi Mkubwa:

Pamoja na aliyosema Mkamap ni hoja dhahifu kwa maoni yako na wengine. Kuna ukweli fulani ambao ni lazima tuuweke bayana. Tanzania ni nchi kubwa na UDSM haijatosheleza miaka iliyopita, haijatosheleza sasa na haitatosheleza miaka inayokuja kukidhi mahitaji ya kitaaluma kwa taifa.

Inawezekana Masua ni professor mzuri akiwa katika viwanja vya UDSM, lakini kuna uwezekano wa yeye kuashindwa kuzipeleka nje ya jumuia ya UDSM. Na kwa sisi tuliosoma nje ya nchi, uzuri wa professor hauko katika kufundisha tu. Uzuri hupo katika to think outside the box. Je kuna paper ngapi za original research work professor ametoa?

Baada ya masomo ya form 4 nilikwenda Dar. Tech. kuchukua FTC (Fundi Mchundo). Vitabu nilivyotumia ni vile vile vinavyotumika kwa wanafunzi wa Advance Diploma na wanaochukua BSc. Kwa kawaida baada ya masomo, tulikuwa na tabia ya kukaa nje chuo (Kando ya Morogoro road) kupumzika. Kuna siku tukiwa nje kama kawaida yetu professor mmoja wa UDSM alikuwa anapita barabara ya Morogoro na akasimama kuongea na sisi. Alituuliza vijana mnasomea nini? Tukamwambia FTC in Electrical Engineering. Professor aliposikia neno Engineering alianza kututukana na kukandia Dar. Tech. kwamba haiwezi kutoa Engineer.

Maoni ya professor huyo ni ya kwake na hayawakilishi jumuia nzima. Lakini ukweli wa kuwa watu waliomaliza UDSM kufikiri kuwa superior hupo. Ukweli huu hauwakilishi jumuia nzima na hausaidii maendeleo ya nchi.

Mwalimu wangu mmoja pale Dar Tech. ambaye alichukua BSc yake UDSM na Master yake Berlin Ujerumani, alituambia wakati anakwenda ku-defend thesis yake huko Berlin alisindikizwa na professor mmoja kutoka UDSM kama supervisor wake. Walipofika Berlin huyu professor alimwambia mwalimu wetu aache kutumia title ya professor na amwite Dr. Kwanini u-professor utumike Tanzania na nje ya Tanzania usitumike. Na anakuwa mkali kutambua vyuo vingine vya Tanzania wakati yeye mwenyewe hana uhakika na u-professor wake akiwa kwa ma-professor kamili.

Kama sehemu zingine za kazi, katika masuala ya elimu kuna talent na knowledge. Knowledge unaipata kwa kufundishwa au kujifundisha. Talent unazaliwa nayo. Na ni watu wenye talent wanaobadilisha mchanga kuwa sambusa. UDSM na vyuo vingine vimetoa wasomi wengi tu kwa taifa ambao wangeweza kubadilisha taifa. Wengi wa wasomi hawa wana maarifa ya vitu walivyosomea lakini hawako talented katika vitu hivyo. Na hii inafanya elimu yao kutoleta mabadiliko ya maana katika jamii.

Na tukikazania talent basi mtu mwenye average ya A ya DIT, IFM au Mzumbe awe na A akiwa UDSM, MIT, Harvard au Cambridge. Na mtu mwenye average ya C akiwa UDSM asiifanya kuwa ni A ya vyuo vingine vya Tanzania.
 
Ni kama mnaochangia humu labda hamjawai ishi Tz na kusoma aya mambo Tz.
Ni obvious mara nyingi UDSM wamekuwa wakiweka nguma the rising of new universities kama MU nakumbuka akina Warioba walipata shida mno kumbe ishu ni fungu!Thanks to mama Mary Nagu yeye alisimamia kidete ilo naona bse mme wake ni lecturer pale.
Atleast nina ya kuongea kuhusu MU but little on DIT ingawa nasikia it is the same to MU.
Unajua msomi anaeogopa challenges to me is hopeless.Lets have as many universities as possible as long as zinameet standards za kuwa vyuo na si kauzibe vya apa na pale.
Na nilishawai sikia mtu kazini akisema C ya UDSM ni A ya MU na kwingineko.Mara nyingi hayo ni maneno ya watu ambao sio competent kabsa tena alikuwa graduate from that day nikaanza kumzarau bahati mbaya baada ya mda alitimuliwa kazi bse alikuwa kitengo cha uhasibu kutokana na ukilaza wake uku akijifanya mjuaji akafanya mambo ndivyo sivyo.
 
Ni kama mnaochangia humu labda hamjawai ishi Tz na kusoma aya mambo Tz.
Kwa mtu aliyesoma na kukulia ktk elimu ya tz,Ni obvious mara nyingi UDSM wamekuwa wakiweka nguma the rising of new universities kisa Fungu, kama MU nakumbuka akina Warioba walipata shida mno kumbe ishu ni fungu!Thanks to mama Mary Nagu yeye alisimamia kidete ilo naona bse mme wake ni lecturer pale.
Atleast nina ya kuongea kuhusu MU but little on DIT ingawa nasikia it is the same to MU as informed by my young brother who once persued some studies there
Unajua msomi anaeogopa challenges to me is hopeless.Lets have as many universities as possible as long as zinameet standards za kuwa vyuo na si kauzibe vya apa na pale.
Na nilishawai sikia mtu kazini akisema C ya UDSM ni A ya MU na kwingineko.Mara nyingi hayo ni maneno ya watu ambao sio competent kabsa tena alikuwa graduate from that day nikaanza kumzarau bahati mbaya baada ya mda alitimuliwa kazi bse alikuwa kitengo cha uhasibu kutokana na ukilaza wake uku akijifanya mjuaji akafanya mambo ndivyo sivyo.
 
Mkamap,

Pole sana ndugu, inaoneka huna cha maana cha kujadili zaidi ya kujielekeza kwenye kuilaumu UDSM, hasa hasa Prof. J.R. Masuha, Ing.Grad. Dipl.Ing., Dr.Ing.(West Berlin)

Maelezo yako yote yananishwishi kuamini wewe uliwahi kupitia pale UDSM upande wa Faculty of Egineering(enzi zile), maana hata mifano yako ya kozi unatoa ya Engineering. Upo uwezekano mkubwa wewe pia ulikuwa mmoja wa wale mafresher walionyakwa..halafu baadaye ukajiunga na DIT. Kwa hiyo ulipoona Prof Masuha pia huko yupo na mambo hayakuenda ulivyotarajia ikawa ni kumlaumu huyo mtaalamu mkongwe!. Japo sina details za huo mgogoro wa DIT, lakini naweza hisi kwamba kwa kuwa Prof ni mtaaluma wa siku nyingi aliyebobea, then alikuwa akitoa mchango wake katika kuiweka hiyo institute mahali pake; mkashindwa muelewa. Kama ni mambo ya technology huyo Prof kabobea, believe me. Asingekubali kushiriki katika kuunda chombo cha ubabaishaji katika fani yake. Si mtu wa masihara, in short. Hivi ni akina nani waliochoma gari lake? Wanachuo? si dhani kama malecturers wenu walifanya hivyo. Kama ni wanachuo, hilo linaeleweka, kwani wakati mwingine wakipotoshwa hufanya vitu bila kufikiri mara mbili.
Ushauri:
kama kweli uli disco pale UDSM(Engineering) na sasa umesoma DIT..bado unayo nafasi ya kupata "Bachala" yako popote pale ili mradi ulifanya vema DIT. Conquer that hatred against USDM, it seems to be haunting you so severely!

Rafiki yangu wewe sasa hapa unataka NIKUSAIDIE JE?
nijitamburishe au unataka nini? ila kwa kawaida ilipaswa nisikujibu.
Mie sijawahi kusoma elimu ya juu nchini tz ,bachala yangu nimechukua hapahapa na nikaunganisha masters nipo karibu kuhitimu hapahapa ,nafanya DIGITAL NETWORKING SYSTEM.ktk chuo kimoja kinaitwa UNIVERSITY OF TECHNOLOGY AND LIFE SCIENCE.

Yani wewe kuona napingana na baadhi ya mambo hapo udsm kufikiria kwako kote ndiko kumekupa soln hiyo uliyokuja nayo POLE SANA NDUGU YANGU.Sitokulaumu wenda ndiyo matunda menyewe hayo uliyochuma ila siwezi kukuacha hivi hivi ningependa kukushauri hivi kama una bachala ya udsm basi jitahidi ufanye masters chuo chochote kile duniani isipokua udsm na kama una masters ya hapo udsm kama hupendi kuendelea zaidi na phd basi fanya hata vijikozi vya miezi kadhaa nje ya udsm.
 
Nilitaka kukujibu naona TzPride kaniwahi.........................hivi wewe ulisomea wapi hesabu???.................no mathematician will agree from what you displayed......even from the moon trust me...........worse stil unakuja kutetea..............aliyosema TzPride yaweza kuwa sahihi kabisa........mlinganisho haufanywi kirahisi rahisi namna hiyo especally kwa route uliyoamua kuitumia ktk mambo ya elimu iliyo diverse

Huruma !!!!

Sina jinsi tena ya kukusaidia .
sasa kama unashindwa kuielewa mantiki ya hesabu ndogo namna hiyo duuu!!!!!!!!!!!

Ili watu wapate pa kuanzia naomba tu useme wapi kunamakosa tkt hesabu hiyo ??
Na wewe ungeonelea kuwe vipi ili kupata chuo chenye uwiano mzuri wa ma phd na wanafunzi??? Je kwa kuchukua namba kubwa kama mlivyokua mnashabikia ??
 
Ogah and TzPride,

nadhani mnaufahamau fika ule usemi

"do not argue with a fool because when people see you they ill not know the difference" I guess you get my drift,.............

Mkamap,

I am sorry maelezo yako toka mwanzo ni hafifu kitaaluma, kihoja, hata katika kujieleza haujatulia kabisa. Details zako na heading uliyoweka havilingani. Kama unataka kutoa changamoto ya kuendeleza elimu basi spend less time hating and more time contributing, Masua is a well respected Professor, be a better professor than him then challenge his choices and decisions that he once made there you will make a difference rather than spending time insulting people.

This is my last post to you. I need this energy more than you know!

PEACE

Something here to be revealed

bimkubwa mhhhh
Masua yawezekana well respected kwa kukamata watu pale udsm.

BUT ninachokuambia kuhusu mtu huyu ni 100% ndicho alichokifanya.
usifanye mentality yako kua ngumu na
kama unamtetea kwa hilo watu watakuhoji shauri lako mie simo.
UDSM ni chuo kinachofubaisha elimu tz
 
pole sana na ongera kwa kazi unayoifanya unajua ni heri kukubali kutokuburuzwa na mawazo mgando, yale yanayotetea ufisadi kuliko kunyamazia kutokubali kuburuzwa na mawazo hayo. kazi uliyoianza ni kali sababu ilishaenea kuwa the only university in tanzani is udsm. ila kama ccm inakili kwa sasa jitihada zako zitawafanya hata udsm kukubali pia. mimi ni mmoja wa wale wanaokuunga mkono. na minavyomjua Maghembe yuko upande wetu.

ukweli tutawaambia hatutachoka mpaka elimu bora ipatikane.
Unajua nini ,pamoja na tz kua tajiri kwa mali asili,ardhi bora ,madini,maziwa ,vivutio vya kila aina lakini cha kushangaza inaburuta mkia kwa umasiki.
watu hadi rais JK wanashindwa kuelewa kwa nini tz ni masikini maana hakuna sababu inayoonekana ya tz kua masikini.

Jibu lake ni UDSM ndio chuo kilichopewa mamlaka tangu awali kufyatua wataalamu na ma thinker amabao wangebadirisha hii malighafi nakua utajiri kwa tz.

UDSM imefeli na ndio kichocheo cha umasikini tz hakuna kitu kingine kilichosababisha kufeli kwa uchumi wetu.

Elimu ya juu ikifeli ktk nchi yoyote matokeo yake ni nchi kufubaa uchumi wake ,hata kama ktk nchi hiyo kunamiminika maziwa,asali dhahabu kila eneo almasi kila eneo,maeneo ya utalii kujazana But uchumi wa nchi hiyo utakua duni tu kama elimu ya juu ya nchi hiyo imefeli ,maana kufeli kwa elimu ya juu kunatoa nafasi ya wajanja kutoka nchi zingine kuja kujichotea hiyo asali na dhahabu na kuwaachia mizinga mitupu.

The same thing happening in tz.
Na. kama elimu ya juu yetu imefeli na uchumi wetu lazima ufeli na vivyo hivyo UDSM ndio imeufelisha.

Kwa yule anayejiuliza kuzorota kwa uchumi wetu kama hujui basi elewa chanzo ni udsm

Udsm ni ndio chazo cha mfubao wa elimu tz.
 
kwamba chuo kimefundishwa na walter rodney ni upumbavu ambao ninadiriki kuutoa hadharani kama liwalo na liwe. nijibu hivi chuo kilichomnyima WALTER RODNEY uprofessor mpaka akafariki ndio baada ya aibu wakaja kumpa ni chuo. kama unamkubari huyo Rodney mbona wao walikataa kumpa. basi rodney sio kitu. unajua kuna mambo mengi ambayo kama vyuo vingine vitakuwa empowered tutapata unafuu.

mimi ni product ya UDSM, mdogo wangu yuko sheria pia mwaka wa mwisho MZUMBE UNIVERSITY, na mdogo wangu wa mwisho yuko sheria UDSM mwaka wa kwanza, pia nina mtoto wa kaka yangu yuko UDSM mwaka wa nne. wote huja na rafiki zao either kwenye fields au kwenye holidays kufanya kazi kwenye firm yangu. mimi ndiyo ninayefahamu ninachokisema katika uwiano wa hizo elimu za vyuo tofauti. tusipayuke kama hujui unyamaze au angalia vyuo vyote kwa makini. inatia hasira watu kugangania upumbavu pasipo sababu.

tuwe wakweli na wazalendo. tuone kama nchi tutaifikisha panapohusika. tuache ubinafsi na kiburi.

Haya, learned friend! Unachotaka kusema hapa nini? Kuwa umetoka katika ukoo uliosoma? Kwamba una firm yako? Au ni wewe pekee yako mwenye haki ya kujadili mada hii maana ulisomea critical thinking na argumentation? Ungetusaidia sisi ambao hatukupata nafasi kupitia kwenye hizo hallowed grounds kama wewe mwenzetu kwa kusema kwa lugha nyepesi; huo upumbavu ni upi?

Aha, Walter Rodney si kitu? Kwa sababu gani, learned friend? Kwa vile,UDSM hawakumpa uprofesa? Au kwa vile wewe Mkuu unamuona ( ambayo ni haki yako) hivyo? Kwa mtu uliyesoma critical thinking na argumentation, you make a weak case. Kama usomi wenyewe ndio huu, namshukuru Mungu kuwa sikubahatika kuingia huko. Kusoma sana, ndugu yangu, si lazima iwe dalili ya kuelimika.
 
Ina semekana mfubao wa elimu nchi unasababishwa na wanaojiita wasomi wa UDSM kuwa na chuki za kipumbavu na mentality mfuu iliyojengeka vichwani mwao.

Mfano wasomi wa UDSM wamekuwa na tabia ya kuzibia vyuo vingi vilivyo nasababu pia nia ya kua vyuo vikuu mfano DIT, kutokana na kuwa na ma egineer wachache ilikuwa na nia siku nyingi ya kutoa digrii lakini ilipambana na mkono wa uzibe kutoka UDSM isipate wasaha huo mfano wa wazi ni pale kiongozi mwandamizi wa UDSM DR Masua alipoamua kusafiri mpaka ulaya ili kukisiriba chuo hicho kwa wadau ili kisipate hadhi hiyo.

Bado kuna mfano wa Mzumbe kikiandamwa na propaganda za wakuu wa adimizi wa UDSM.
SWALI LA KUJIULIZA!!! kwanini? UDSM ni wahasimu wakubwa wa vyuo vinavyotoa kozi zinazofanana na zile zinazotolewa UDSM.

Na juhudi zao zinapokwama hufanya kila mbinu ili chuo husika kiwe chuo kishiriki chao,habari zinapasha.

Na cha kusikitisha zaidi hawa wahadhiri wamekua mstari wa mbele kukebehi vyuo vingine mfano utasikia ukipata C udsm hii ni A mzumbe, na sivyo hivyo tu wamekua wakienda mbali kulaghai wanafunzi wao na kuwaaminisha vitu vya ajabu ajabu mfano hii digrii ya UDSM ni masters ya ulaya.

Cha ajabu wanafunzi hao nao wamekua wakiamini hayo bila kuhoji mbona hawa ma tutor wetu wengi wamezichukua hizo master ulaya? baada ya ya kuchukua digrii hapa kwanini hawakwenda moja kwa moja DR huko ulaya.habari zilizidi kupasha na kuongeza,

DESA za UDSM ndizo zimeua kabisa elimu ya Tanzania maana zimekuwa zikitoa wanafunzi mabigwa wa desa wasio na skills, chanzo kilipasha.

Na kama mfumo mzima wa elimu Tz kuangaliwa inabidi waanze na UDSM maana inasemekana ni chuo kiliojaa kinyongo, chuki ku-disco watu wenye uwezo kwa sababu za ma-prof binafsi, kupitisha wanafunzi wasio na uwezo kwa uwezo wao wa kuvua chupi.

Ndugu ndugu, chonde chonde, unaporopoka uwe makini. Kwa kuanza nenda kwenye thread moja iliyoandikwa kuhusiana na digrii au Phd feki za Mzumbe then urudi kwenye mada yako.

Mimi sio kwamba nasema hawajawahi kuzuia vyuo vingine visiwe vyuo vikuu but hata kama ni kweli tumewahi kujiuliza ni kwa nini. Na tumewahi kujiuliza maswali yafuatayo:-
- Je, vina wahadhiri wa kutosha wenye elimu inayotambulika na baraza la vyuo vikuu duniani..??
- Je, vina maabara za kutosha kiasi cha kuweza kubeba population size ya University. Manake utambue chuo kikibeba wanafunzi 20, sio University ni College, nenda kwenye standards za vyuo kwa ufafanuzi.
- Je, kina teknolojia ya kutosha kiasi cha kumeet viwango vya kimataifa..??

Mimi nafikiri hayo maswali ni ya msingi sana, then baada ya hapo ndio uanze kuongea. Je, DIT ina Phd ngapi..?? Je, hata huko Mzumbe umeona Phd zao..?? na je hata hizo zilizodaiwa kuwa feki ziko ngapi..??

Huyo binadamu aliyewahi kudai kuwa C ya Mlimani ni A ya mzumbe, mimi namkubalia, sio kwamba ni mdau/mshabiki wa mlimani, no plse. Ukweli ni kuwa, nenda Mzumbe kachukue mitihani ya masomo kama auditing, management accounting, financial accounting and tax. Kisha njoo nayo mlimani na ulinganishe na paper zao, kama ni kipanga, you will obviously detect the difference ya competence ya kimtihani. I have done that, na ndio maana najiamini kuongea hivyo.

Pia nimewahi kuambiwa na wanafunzi hao hao wa Mzumbe jinsi wanavyotungiwa mitihani. Mfano, kuna mwalimu mmoja wa auditing (jina kapuni, ingawa ukifuatilia utamjua), yeye huwa anawapa angles atakazochezea kwenye pepa, na ukichunguza wanafunzi kibao wa Mzumbe wana A kwenye auditing, but walete kwenye soko na tena usiende mbali, walete kwenye mitihani ya NBAA, lazima wale chaka. Sasa kachukue kijana wa mlimani ambaye kapikwa vizuri auditing na mtaalamu anayeitwa Dr. Temu, then uniambie ataifanya nini mitihani ya NBAA.

Swala la uwezo wa wanafunzi wa mlimani hilo napenda kukushauri tusilumbane sana, nenda kwenye big 4 auditing firms watakwambia wanapenda kuchukua wapi wafanyakazi...? Huko kumejaa mlimani tupu, kaangalie kama utakuta vyuo vyako. Mzumbe wameanza kuingia juzi juzi, na wengi wameprove in-efficiency. Kiasi kwamba, moja ya kampuni, jina kapuni, imekiri kutochukua tena vijana wa Mzumbe. Sasa niambie shekhe, huo uwezo unaouongelea ni upi..?? Pia kwenye uwezo, hebu nenda kwenye database ya NBAA kisha uangalie for the past 5 to 10 years, best students (top 3) katika kila somo na if possible overall huwa wanatoka chuo gani. Au kila matokeo ya NBAA yanapotoka, nenda kaangalie kwenye ubao wa kitivo cha biashara mlimani, utakuta tangazo toka bodi ya uhasibu (i.e. NBAA) la kukipongeza chuo kwa "kuendelea kutoa" na sio "kutoa tu" wanafunzi bora wa katika mitihani ya NBAA.

Mimi nafikiri hawa wazee wa Mzumbe, waache kuinvest kwenye kufaulisha, bali wawekeze kwenye kutoa vipaji.

Pia mheshimiwa, ukumbuke kuwa uwezo wa mtu, sio chuo tu, hata kipaji binafsi kinaweza fyatua kitu. So, hata mtu apikwe Havard, anaweza akaja bongo akapigwa bao na mtu mwenye kadiploma cha chuo cha uswazi. Ingawa, je, ni wangapi.?? Manake hizi hazitokei kila siku..!! Watu kama hawa ni wachache kwenye jamii, na ndio maana wataalamu wa viwango duniani, wanasema wanataka mtu anayetoka kwenye chuo kinachotambulika kimataifa, akiwa na mategemeo kuwa vipanga ndio wanaingia humo and not otherwise. Na ndio maana, mlimani kwa sasa, ukiwa na division II hukanyagi na hata I ikiwa ya wasiwasi hunusi majengo ya chuo. Ukikuta hivyo, ni wale ambao Mungu kawapa neema ya kipekee, na huwa ni rare vile vile.

Kwa kipindi cha miaka ya karibuni naweza kukukubalia kuwa mlimani imeshuka, ila haijafikia kiwango hicho unachokifikira au kiwango cha hivyo vyuo vyako. Hii yote ni kutokana na uzembe wa serikali yako ya URT (i.e. United Republic of Tanzania), kwa kuendekeza siasa mpaka kwenye elimu. Kwa sasa wameongeza enrollment kupita kiasi na nahisi hii inachangia hata uwezo wa walimu kumeet mahitaji ya kila mwanafunzi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Ila hili waheshimiwa wa Mlimani wameshataarifiwa walirekebishe na naamini wameanza kulifanyia kazi.

Kama una maoni, yanakaribishwa, inawezekana una jipya zaidi nisilolijua.
 
Bado vipara mnagombania chanuo? Bado mnalinganisha paper ili mjue nani mkali? Elimu si bling! Hivi kweli mnataka kusaidiana au kwa lugha yenu kuendeleza 'beef'? Naona nilikosea njia humu nikitegemea nitawakuta wasomi wakipanuana mawazo. Should have known better.
 
ukweli tutawaambia hatutachoka mpaka elimu bora ipatikane.
Unajua nini ,pamoja na tz kua tajiri kwa mali asili,ardhi bora ,madini,maziwa ,vivutio vya kila aina lakini cha kushangaza inaburuta mkia kwa umasiki.
watu hadi rais JK wanashindwa kuelewa kwa nini tz ni masikini maana hakuna sababu inayoonekana ya tz kua masikini.

Jibu lake ni UDSM ndio chuo kilichopewa mamlaka tangu awali kufyatua wataalamu na ma thinker amabao wangebadirisha hii malighafi nakua utajiri kwa tz.

UDSM imefeli na ndio kichocheo cha umasikini tz hakuna kitu kingine kilichosababisha kufeli kwa uchumi wetu.

Elimu ya juu ikifeli ktk nchi yoyote matokeo yake ni nchi kufubaa uchumi wake ,hata kama ktk nchi hiyo kunamiminika maziwa,asali dhahabu kila eneo almasi kila eneo,maeneo ya utalii kujazana But uchumi wa nchi hiyo utakua duni tu kama elimu ya juu ya nchi hiyo imefeli ,maana kufeli kwa elimu ya juu kunatoa nafasi ya wajanja kutoka nchi zingine kuja kujichotea hiyo asali na dhahabu na kuwaachia mizinga mitupu.

The same thing happening in tz.
Na. kama elimu ya juu yetu imefeli na uchumi wetu lazima ufeli na vivyo hivyo UDSM ndio imeufelisha.

Kwa yule anayejiuliza kuzorota kwa uchumi wetu kama hujui basi elewa chanzo ni udsm

Udsm ni ndio chazo cha mfubao wa elimu tz.

data tunazozijua ni kuwa WALTER RODNEY kafanya paper zake nyingi za kuwa professor, na kazibiwa na hao hao maprof. ila baada ya kufariki ndipo walipoona aibu na kumpa huo uprofessor. sio roho mbaya?. hii inatokea kwa wengi tu!.

kama mkuu wa nchi alienda kuomba wataalamu nje ya nchi akidai tanzania hamna wataalamu, wakati chuo kimeendelea kutoa sheria tandu miaka nenda rudi, hivi unataka jibu gani kuwa chuo hiki cha udsm hakijakidhi matatizo ya nchi.

all the efforts so made since independence have been futile na sasa tunahitaji njia nyingine ya watu kuja na mawazo mapya. hatusiti kuwashutumu hao wanaotetea ufisadi kuwa nao ni mafisadi. au tunahitaji kumtumia DR Slaa na mwakyembe autumie circumstancial evidence kuwaunganisha na hao mafisadi?

tusiuje na hoja moja tu ya degree feki kuover rule others. hii hoja imeisha kubalika na pande zote na hivyo it is not in dispute. sasa hoja nyingine je.......

mimi ninadhani kitendo cha Rais wetu kudai hatuna wataalam ni dhairi kuwa UDSM imefubaza elimu ya tanzania.
 
Ndugu ndugu, chonde chonde, unaporopoka uwe makini. Kwa kuanza nenda kwenye thread moja iliyoandikwa kuhusiana na digrii au Phd feki za Mzumbe then urudi kwenye mada yako.

Mimi sio kwamba nasema hawajawahi kuzuia vyuo vingine visiwe vyuo vikuu but hata kama ni kweli tumewahi kujiuliza ni kwa nini. Na tumewahi kujiuliza maswali yafuatayo:-
- Je, vina wahadhiri wa kutosha wenye elimu inayotambulika na baraza la vyuo vikuu duniani..??
- Je, vina maabara za kutosha kiasi cha kuweza kubeba population size ya University. Manake utambue chuo kikibeba wanafunzi 20, sio University ni College, nenda kwenye standards za vyuo kwa ufafanuzi.
- Je, kina teknolojia ya kutosha kiasi cha kumeet viwango vya kimataifa..??

Mimi nafikiri hayo maswali ni ya msingi sana, then baada ya hapo ndio uanze kuongea. Je, DIT ina Phd ngapi..?? Je, hata huko Mzumbe umeona Phd zao..?? na je hata hizo zilizodaiwa kuwa feki ziko ngapi..??

Huyo binadamu aliyewahi kudai kuwa C ya Mlimani ni A ya mzumbe, mimi namkubalia, sio kwamba ni mdau/mshabiki wa mlimani, no plse. Ukweli ni kuwa, nenda Mzumbe kachukue mitihani ya masomo kama auditing, management accounting, financial accounting and tax. Kisha njoo nayo mlimani na ulinganishe na paper zao, kama ni kipanga, you will obviously detect the difference ya competence ya kimtihani. I have done that, na ndio maana najiamini kuongea hivyo.

Pia nimewahi kuambiwa na wanafunzi hao hao wa Mzumbe jinsi wanavyotungiwa mitihani. Mfano, kuna mwalimu mmoja wa auditing (jina kapuni, ingawa ukifuatilia utamjua), yeye huwa anawapa angles atakazochezea kwenye pepa, na ukichunguza wanafunzi kibao wa Mzumbe wana A kwenye auditing, but walete kwenye soko na tena usiende mbali, walete kwenye mitihani ya NBAA, lazima wale chaka. Sasa kachukue kijana wa mlimani ambaye kapikwa vizuri auditing na mtaalamu anayeitwa Dr. Temu, then uniambie ataifanya nini mitihani ya NBAA.

Swala la uwezo wa wanafunzi wa mlimani hilo napenda kukushauri tusilumbane sana, nenda kwenye big 4 auditing firms watakwambia wanapenda kuchukua wapi wafanyakazi...? Huko kumejaa mlimani tupu, kaangalie kama utakuta vyuo vyako. Mzumbe wameanza kuingia juzi juzi, na wengi wameprove in-efficiency. Kiasi kwamba, moja ya kampuni, jina kapuni, imekiri kutochukua tena vijana wa Mzumbe. Sasa niambie shekhe, huo uwezo unaouongelea ni upi..?? Pia kwenye uwezo, hebu nenda kwenye database ya NBAA kisha uangalie for the past 5 to 10 years, best students (top 3) katika kila somo na if possible overall huwa wanatoka chuo gani. Au kila matokeo ya NBAA yanapotoka, nenda kaangalie kwenye ubao wa kitivo cha biashara mlimani, utakuta tangazo toka bodi ya uhasibu (i.e. NBAA) la kukipongeza chuo kwa "kuendelea kutoa" na sio "kutoa tu" wanafunzi bora wa katika mitihani ya NBAA.

Mimi nafikiri hawa wazee wa Mzumbe, waache kuinvest kwenye kufaulisha, bali wawekeze kwenye kutoa vipaji.

Pia mheshimiwa, ukumbuke kuwa uwezo wa mtu, sio chuo tu, hata kipaji binafsi kinaweza fyatua kitu. So, hata mtu apikwe Havard, anaweza akaja bongo akapigwa bao na mtu mwenye kadiploma cha chuo cha uswazi. Ingawa, je, ni wangapi.?? Manake hizi hazitokei kila siku..!! Watu kama hawa ni wachache kwenye jamii, na ndio maana wataalamu wa viwango duniani, wanasema wanataka mtu anayetoka kwenye chuo kinachotambulika kimataifa, akiwa na mategemeo kuwa vipanga ndio wanaingia humo and not otherwise. Na ndio maana, mlimani kwa sasa, ukiwa na division II hukanyagi na hata I ikiwa ya wasiwasi hunusi majengo ya chuo. Ukikuta hivyo, ni wale ambao Mungu kawapa neema ya kipekee, na huwa ni rare vile vile.

Kwa kipindi cha miaka ya karibuni naweza kukukubalia kuwa mlimani imeshuka, ila haijafikia kiwango hicho unachokifikira au kiwango cha hivyo vyuo vyako. Hii yote ni kutokana na uzembe wa serikali yako ya URT (i.e. United Republic of Tanzania), kwa kuendekeza siasa mpaka kwenye elimu. Kwa sasa wameongeza enrollment kupita kiasi na nahisi hii inachangia hata uwezo wa walimu kumeet mahitaji ya kila mwanafunzi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Ila hili waheshimiwa wa Mlimani wameshataarifiwa walirekebishe na naamini wameanza kulifanyia kazi.

Kama una maoni, yanakaribishwa, inawezekana una jipya zaidi nisilolijua.

nakuuliza wewe, nani anatoa pesa kwa ajiri ya kuongeza waadhiri wa UDSM si serikali. sasa kama ndiyo hiyo tunachotaka ni kufanya serikali itoe pesa kwa ajiri ya kuongeza waadhiri, maktaba n.k katika vyuo hivyo sio UDSM kutumia fursa ilio nayo kurob vyuo hivi visipewe. etc. pia pinda alipochaguliwa mtu wa kwanza kushukuriwa ni wazazi kwa kumlea vizuri, na mke wake na watoto pia, na pia akiboronga kama kuiba tutasema wazazi hawakumpa malezi mema.

hii inatumika hata kwa vyuo, ndio maana yule mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi kenya alipofanya vibaya UDSM ilifikia hatua ya kutaka kumkatia degree yake kuwa ameaibishwa. tukifanya hivyo kwa kila mmoja tukianzia kwa hao mafisadi tutabakiza wangapi waliopitia hapo?

tutalaumu kwa kuwa na mabogus wanaoshindwa kutrain watu wao. the education is to liberate one so as to liberate the sociate. if that fails we have all reasons and means to do so.

swala la area of concentration liko kila chuo duniani including UDSM na NINAKUOMBA WEWE MCHANGIAJI UACHE UNAFIKI. HIVI HAPO UDSM HAKUNA TIMED TEST ambapo wanafunzi wanapewa maswali kumi na kuambiwa yatatoka moja???? au kwenye paper ya mwisho mwalimu huwa wakati mwingine anasema kwenye maswali ya SEMINA yatakuwepo matatu, na timed test mawili n.k. kama unabishi niombe paper ya timed test niiscan hapa na uione ili nikuestop.

watanzania bwana ni wanafiki kwelikweli. utawaona utadhani tunafundishwa kudanganya hapo vyuoni. mbona sisi tumepitia hapo hapo. hatupingi kuwa UDSM sio chuo, maana hata wale walioendesha kampein za multipartism walikuwa CCM akiwepo nyerere, na hapa utaona magroup mawili consevatives, wale wanao sema kiwepo chuo kimoja, wasioona hali itakavyokuwa baada ya miaka 20 ijayo, na liberal, wale wanaoonelea vyuo vingi kuwa kula siku tutakuwa tunapiga hatua ili baada ya miaka 20tuwe katika level moja.
 
Back
Top Bottom