Matokeo ya mikopo ya elimu ya juu 2023/2024 na changamoto zake

Sep 27, 2023
9
28
Naitwa Abdul-Aziz Ally Carter Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam( UDSM), Jana Octoba 20,2023 matokeo ya awamu ya 1 ya mkopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu yalitoka.

Kuna idadi kubwa ya wanafunzi wamepata mkopo chini ya 20% na walikuwa na sifa na vigezo vya kupata mkopo, wengi wao hawajapata aidha pesa za vitabu (books and stationary), wala pesa za mafunzo kwa vitendo (training practice),

Miongoni mwa wanafunzi niliowasiliana nao anakuja kusoma UDSM, kwa kozi anayotaka kusoma sociology Ada ni 1,300,000 , Bodi ya mikopo imempatia 230,000 sawa na 17% kwa msingi huo huyu mwanafunzi anapaswa kulipa 1,070,000 .

Swali je ni wazazi au walezi wangapi Tanzania wataweza kulipia kiasi hiki cha ada? Wanafunzi wangapi wa Elimu ya juu watashindwa kuendelea na masomo kwa kigezo cha Ada?
Nashauri mosi, TAHLISO wazungumzie hii changamoto mana wao ndio wenye Wajibu wa kupigania haki za Wanafunzi.

Pili bodi ya mikopo itoe taarifa sahihi ya mikopo na tatu wizara ya Elimu na serikali vitatue changamoto hii mapema iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom