UDSM-Law First Classes

Haya Mkuu, kunywa maji upumzike. Maana unaelekea kurukwa kwa mambo yasiyo na maana kwenye maisha yako. Ukiwa na jinai ndiyo utajua kama Mawakili ni vilaza au la. Siku njema!
Wakati naenda kunywa maji na wewe GO MEMORIZE mnatia aibu aisee ....katika zunguka zunguka yangu yote mahakama za mjini hapa ni wakili mmoja tu niliona yupo fiti ni Aisha Bade nadhani alikua mwenyekiti wa TAWLA....wengine wengi japo sio wotr ni waganga njaa aisee ...typical bush lawyers
 
Hivi hiyo sheria ina ugumu kiasi gani hadi watu wasifaulu na first class honors hapo UDSM?
Mimi nimepita pale kuna ubabe wa kutisha sana,
Utaratubu mbovu sana wa kufundisha kuna watu pale wana GPA nzuri sana kwenye makaratasi wakianza kufundisha ni kama standard seven leavers .
Wengine wanaingia darasani kusoma notes zao siyo kugundisha
Wengine wanafanya translation tu
Wakimaliza wanatoa vitisho vya kukamata watu.
 
Mkuu,ungesoma vyema mantiki ya jibu langu ungeelewa.Ni hivi,tangu zamani wanafunzi wa Sheria wamekuwa wakijisomea kwa juhudi na maarifa...kwelikweli. Sheria na Uhandisi ni kozi zenye wasongo wa kutosha. Lakini,perfomance ya wanafunzi huwa tofauti.Hapo ndipo hata mimi nisipoelewa. Wanafunzi wanahudhuria mihadhara na kujisomea kwa bidii,kwanini ufaulu usumbue?
Udsm kwa sasa kuna lecturers wachache sana wenye sifa za kuwa pale wengine wote ni sawa na wanafunzi tu
Wanakuja kusomea notes wanafunzi wakopi darasani badala ya kufanya lecturing.
 
Hapana nilikua naona ikitokea ishu ya sheria hapa JF...jamaa anaitwa atoe eti "ushauri wa kisheria" sasa ndo nikasema naomba aniambie case alizoshinda ili nizifuatilie nione kama sio bush lawyer kama wenzake.....
Maana ni kama yule kibatala ana jina kubwa...juzi kwenye case ya yule msanii anashindwa hata kuweka foundation ya documentary evidence.......
Acha ubishi mandazi hivi unaweza kutumia kigezo hicho tu kumdiscredit kibatala ?
Ana precedent ngapi mpaka sasa ambazo zina impact kwa jamii ?
 
Leo nimekumbuka historia hii kama kumbukumbu:
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM kilianzishwa mwaka 1961 kikiwa na kitivo kimoja tu cha Sheria. Kilianzia Lumumba na sasa Mwalimu Julius Nyerere Mlimani Campus kikiwa na Koleji na Shule Kuu mbalimbali.

Tangu kuanzishwa kwake,Kitivo cha Sheria kimetoa wahitimu wanne tu waliokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza(yaani First Class-GPA ya 4.4 hadi 5.0).

Hao ni Dr.Ringo William Tenga,Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro na Prof. Hamudi Ismail Majamba. Hawa wanastahili sifa.Wanastahili kuitwa 'the Big Four'.Tangu mwaka 1992,hakukuwa na Daraja la kwanza lingine.

Wengine tulijaribu lakini tukashindwa.Tukaishia na Daraja la Pili la Juu (Upper Second Class). Ikumbukwe kuwa,Kitivo cha Sheria ndicho kinachochukua wanafunzi wanaofaulu zaidi,'the Cream of the Nation' kwa masomo ya sanaa(lakini kwasasa TCU wanaleta hata daraja la pili).

Juhudi ziongezwe kwa wengine kupata Daraja la Kwanza kitivoni hapo.Wapo watakaoweza. Wajiunge na wastahili hao. Mazingira ya kujisomea UDSM yanaboreshwa kila kukicha. Inawezekana hata kwa wengine.
Sasa kama mlifaulu sana mbona wewe umaarufu wako hatuuoni kwenye practice?
 
Wemye first class huwaga ni vilaza afu mbwembwe nyingi.... mmoja wao ni huyo hasani majamba na palamagamba
Halafu huyu aliingizwa chaka kwenye mazungumzo ya makinikia na barrick! Akaambiwa economic profit tutagawana nusu kwa nusu halafu akadhani faida halisi ya fedha itokanayo na biashara ya dhahabu tutagawana nusu kwa nusu! Mkuu naye akaingizwa chaka! Kumbe wenyewe wanamaanisha win win situation! Yaani kila MTU ajisikie amepata! Profesa mzima akaamini kuwa pamoja na kuwa na hisa 16% lakini faida apate 50%! Hiyo haiwezekani popote! Hamsini zetu ni ule mrahaba, kutengeneza miundo mbinu, kuchangia shule pamoja na hiyo 16% na tozo mbali mbali kwa pamoja zinafanya win ya upande wetu! Vilivyobaki vyote ni win ya upande wao!
 
Udsm kwa sasa kuna lecturers wachache sana wenye sifa za kuwa pale wengine wote ni sawa na wanafunzi tu
Wanakuja kusomea notes wanafunzi wakopi darasani badala ya kufanya lecturing.
Maprofesa wengi wao wapo kwenye foleni ya kufikirika kusubiri nafasi za uteuzi! Si ajabu wakijikomba komba! Wanatia huruma!
 
Halafu huyu aliingizwa chaka kwenye mazungumzo ya makinikia na barrick! Akaambiwa economic profit tutagawana nusu kwa nusu halafu akadhani faida halisi ya fedha itokanayo na biashara ya dhahabu tutagawana nusu kwa nusu! Mkuu naye akaingizwa chaka! Kumbe wenyewe wanamaanisha win win situation! Yaani kila MTU ajisikie amepata! Profesa mzima akaamini kuwa pamoja na kuwa na hisa 16% lakini faida apate 50%! Hiyo haiwezekani popote! Hamsini zetu ni ule mrahaba, kutengeneza miundo mbinu, kuchangia shule pamoja na hiyo 16% na tozo mbali mbali kwa pamoja zinafanya win ya upande wetu! Vilivyobaki vyote ni win ya upande wao!
Kweli mkuu eti ni msomi mwenye 1st class degree...
 
Mi Sijaelewa hapo yani wanachaguliwa cream of the nation halafu hawapati first Class
Wanajidanganya tu hao. Siku hizi hamna hayo... Vyuo kibao na kila mwanafunzi anaamua aende wapi.

Rafiki zangu walioenda UDSM walienda kwa division 3. Wengine tulichagua SUA, Mzumbe na UDOM according to the needs.

Isitoshe, kama swali umepata ni umepata tu! Huwezi kupata maswali katika mtihani halafu ukatwe tu ili usipewe GPA nzuri.
Rafiki zangu waligraduate na vi GPA vyao vya kuunga, na haikushangaza kwa maana hata hizo division 3 za form six walipigana sana kuzipata.

Hizo GPA ndio uwezo wao wa akili, period. Wasitafute mchawi
 
Sure Mkuu....
Hao wanaojiita ma-HR wamebase sana kuangalia ukubwa wa GPA.....wangekua wanatoa interview kwa wahitimu wote regardless of GPA afu mtu apimwe kwa performance ya kazi....

Kuna boya mmoja anasemekana alikua vizuri class ila kwenye practice inabidi mtu uwe una-question legitimacy ya iyo first class yake.....
Wata shortlist vipi wasipoangalia GPA? Nafasi moja ya kazi applicants 3800, unafikiri unawapunguzaje ili uite kwenye usaili?

Zinaangaliwa GPA na criteria zingine wanazoona zinafaa.
 
Wata shortlist vipi wasipoangalia GPA? Nafasi moja ya kazi applicants 3800, unafikiri unawapunguzaje ili uite kwenye usaili?

Zinaangaliwa GPA na criteria zingine wanazoona zinafaa.
Ndo tatizo ilo maana wenye first class wengi wao vilaza makazini
 
Wakati naenda kunywa maji na wewe GO MEMORIZE mnatia aibu aisee ....katika zunguka zunguka yangu yote mahakama za mjini hapa ni wakili mmoja tu niliona yupo fiti ni Aisha Bade nadhani alikua mwenyekiti wa TAWLA....wengine wengi japo sio wotr ni waganga njaa aisee ...typical bush lawyers
Aisha Bade mpiga pesa za home shopping
 
Back
Top Bottom