Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Leo nimekumbuka historia hii kama kumbukumbu:
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM kilianzishwa mwaka 1961 kikiwa na kitivo kimoja tu cha Sheria. Kilianzia Lumumba na sasa Mwalimu Julius Nyerere Mlimani Campus kikiwa na Koleji na Shule Kuu mbalimbali.
Tangu kuanzishwa kwake,Kitivo cha Sheria kimetoa wahitimu wanne tu waliokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza(yaani First Class-GPA ya 4.4 hadi 5.0).
Hao ni Dr.Ringo William Tenga,Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro na Prof. Hamudi Ismail Majamba. Hawa wanastahili sifa.Wanastahili kuitwa 'the Big Four'.Tangu mwaka 1992,hakukuwa na Daraja la kwanza lingine.
Wengine tulijaribu lakini tukashindwa.Tukaishia na Daraja la Pili la Juu (Upper Second Class). Ikumbukwe kuwa,Kitivo cha Sheria ndicho kinachochukua wanafunzi wanaofaulu zaidi,'the Cream of the Nation' kwa masomo ya sanaa(lakini kwasasa TCU wanaleta hata daraja la pili).
Juhudi ziongezwe kwa wengine kupata Daraja la Kwanza kitivoni hapo.Wapo watakaoweza. Wajiunge na wastahili hao. Mazingira ya kujisomea UDSM yanaboreshwa kila kukicha. Inawezekana hata kwa wengine.