UDSM; Chuo cha kutengeneza Mafisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDSM; Chuo cha kutengeneza Mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Gumzo, Oct 4, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati nchi inapambana na vitendo viovu ukiwemo ufisadi na rushwa tunategemea taasisi zetu hasa za elimu ya chuo kikuu kuwa mstari wa mbele kukemea uovu huo na kuonesha mfano wa kuigwa na wanajamii wengine.

  Hali inaonekana kuwa tofauti kabisa na ukweli huo.Chuo kikuu cha dar es salaam kimefunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa mpya wa masomo.Wanafunzi wengi wamekosa vyumba vya kulala katika mabweni ya liyopo eneo la chuo na hosteli ya mabibo.Imegundulika kuwa hali hiyo haitokani tu na uhaba wa vyumba kutokana na ongezeko la wanachuo bali kuna ufisadi wa hali ya juu.

  Jana nilianza uchunguzi wangu na kufanikiwa kupata vyumba kumi na sita ambavyo vilikuwa vinauzwa na kiongozi wa DARUSO ambaye sikutajiwa jina.Nilitakiwa kulipia laki moja kwa chumba kimoja kilichopo mabibo hosteli na laki moja naishirini kwa chumba cha campus.Leo nimeendelea na uchunguzi kwa kujifanya mtafuta chumba.Nimefanikiwa kumpata mwanfunzi wa mwaka wa pili anauza vyumba viwili.vyote hivyo amepewa na kiongozi wa daruso atafute wateja wa chap chap.

  Mbali na uchunguzi huu, kilio ni kikubwa sana kwa wanachuo waliokosa vyumba hasa pale wanapogundua kuwa vyumba vipo ila vimeshikiliwa na mafisadi wachache wanaoviuza kwa lengo la kujipatia fedha.

  Rushwa na uchafu wa kila aina umekuwepo katika zoezi la kuwapatia vyumba wanachuo mlimani lakini siku zinavyokwenda linakuwa sugu.Haiingii akilini kama wanakuwepo viongozi wa wanafunzi wanashiriki kwenye ufisadi wa kutisha hivyo.Tuntengeneza kada ya viongozi wa namna gani kwa hapo baadae?.Jamii inayotarajiwa kuhudumiwa na watu kama hao itapona kweli?.Tuna haja gani kupambana na mafisadi wa kubwa wa EPA wakati vyuo vyetu vinatuzalishia mafisadi wenye digrii za kutungua?

  Tatizo linaanzia UNIVERSITY STUDENTS ACCOMODATION BUREAU{USAB}Ni mamlaka yakusimamia suala la malazi lakini wanashindwa kuvalia njuga suala hili.Vilevile utawala wa chuo upo kimya wakati hali hii inajulikana wazi.

  Tusiache kipele kikue na kugeuka donda ndugu.
   
 2. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Tatizo dogo
  kachukue polisi mje naye kununua hivyo vyumba.
   
 3. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #3
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ni issue ya miaka mingi tu,kwani kwa sera ya chuo kikuu cha Dsm(kama ipo) ni kuwapa vyumba 1st year wa batch ya kwanza(Govt sponsored via loan board?) wale wa batch zifuatazo huwa hawana chao japo nao ni 1st year.Finalist wachache ambao wana network za kutosha huwa ndio 2nd priority then comes wanunuaji.Hata baadhi ya viongoz wa DARUSO hukosa vyumba sometime(mwaka jana ni mfano).Nadhan tatzo lnaanzia kwa utawala kuongeza udahili wa wanachuo bila kuhakikisha kuwa kuna mahali pa uhakika pa malazi kwa wanachuo hao,kwani elimu ni zaidi ya kukaa lecture rooms!Then USAB pia kuna tatzo kubwa kwani wanadai kuwa wana_allocate rooms using the software(zalongwa) ila ukwel ni kuwa certain rooms huwa znakuwa zmetengwa tayar kwa biashara kabla hata hiyo software haija_come into play.So zaidi ni viini macho!!!Mwenye nacho hununua ktanda(japo wenyewe huita room) na mwenzangu na mie asubiri kubebwa au apange mtaani.Hii ndo hali halisi ya suala zma la accomodatn UDSM.Naomba kuwakilisha!
   
 4. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa mwezi sasa hizi wanalipa ngapi?
   
 5. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi nina data za miaka ya nyuma (2004) tulikuwa tunalipa sh 300 kwa siku kwa vyumba vilivyopo pale main campus na sh 200 kwa siku kwa vyumba vilivyombo off campus (Mabibo na Kijitonyama). Siku hizi nahisi zitakuwa simepanda.
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, kwanza kabisa niseme wazi kuwa sina ugomvi na Wasomi wetu waliomaliza UDSM wala agenda binafsi ila ni wasiwasi mkubwa sana na UDSM ambacho ni kati ya Vyuo Vikuu vyenye sifa kubwa Afrika na Duniani. UDSM kimetoa viongozi mashuhuri Afrika miongoni mwao ni Dk John Garang, Yoweri Museveni na kadhalika.

  Baada ya sera ya Taifa kutoa mikopo kwa Wanafunzi, moja ya matokeo chanya ya Srea hiyo ni ongezeko la Wanafunzi katika Vyuo vyetu Vikuu hasa UDSM. Hata hivyo kama ilivyo kawaida hakuna kitu chema ambacho hakina mapungufu lakini haya ya UDSM linatakiwa mtazamo maalumu.

  Ongezeko kubwa la Wanafunzi pale UDSM limesababisha matatizo makubwa sana ya makazi kwa upande wa wanafunzi na kusabibisha wanafunzi wengi wishi mitaani kama vile Sinza, Ubungo, Msewe nk.

  HAbari nilizonazo ni kuwa baadhi ya Wafanyakazi wanaohusika na kutoa nafasi za Hosteli pale UDSM wameuza kazi hiyo kuwa mradi mkubwa wa kujipatia fedha na kinachonisikitisha ni kuwa Uongozi wa UDSM umeshindwa kudhibiti tatizo la rushwa kwenye utoaji wa vyumba kwa Wanafunzi. Binti mmoja alimpigia simu mama yake akimuomba shilingi laki mbili (200,000/-) ili ahonge na kupatiwa chumba pale main campus na nilipofuatilia niliambiwa kwamba ili mwanafunzi apte upendeleo katika kupata chumba hulazimika kutoa kati ya shilingi laki mbili hadi laki tano (200,000/- to 500,000/-). Kiasi hicho inawwezeka ikankuzwa na wanafunzi wenye ili waweze kupata pesa nyingi kutok kwa wazazi lakini sua;la la rushwa katika hilo eneo lipo na limekuwepo kwa muda mrefu sasa.

  Athari zake kwa Taifa
  Athari kubwa kuhusiana na rushwa za makazi kwa wanafunzi pa;le UDSM ni kujenga Taifa la Viongozi wasio waadili baadaye (MAfisadi) maana kama mwanafunzi amezoezwa kutoa rushwa ili kupata huduma ni wazi kwake kutoa na kupokea rushwa haitakuwa tatizo na itakuwa ni sehemu ya maisha yake.

  Wanafuzni hawa ndiyo wanokuja kuwa viongozi wetu kwenye Ofisi za Umma na Binafsi na hta kuwa viongozi wa Kisiasa- Uwaziri hata Urais! Sasa ikiwa maisha yao ya Chuo Kikuu yamezingirwa na rushwa ma jkuifanya kuwa ehemu ya maisha yao; Je; hatima yao na mustakabali kwa Taifa utakyuwaje?

  Ndiposa na sema UDSM ni kitivo cha kuzalisha Viongozi Mafisadi na wasio waadilifu kitu ambacho ni hatari kubwa kwa Taifa Tanzania.
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tafadhari naomba ufafanue, hiyo Rushwa anapokea nani hapo UDSM? Ni kiongozi wa DARUSO au kiongozi wa USAB? Tafadhari liweke wazi ili ufuatiliaji wake uwe rahisi. Ikiwezekana andika na jina la mtu aliyepokea hiyo laki mbili na anayehusika na upokeaji wa hiyo hela. Naamini upo anonymous, ukimtaja, hakuna atakayejua kama wewe ndo umetaja. Kwa ajili ya kulinda heshima ya chuo pia kukomesha vitendo hivyo katika taifa, ningependa kujua undani wa jambo hili ili personally niliwasilishe kwenye vyombo husika.
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa maada nzuri, ila nzuri zaidi ukaandika kwa upana zaidi, maana hii maada yako imelenga sana kwenye accomodation.

  Ni mpango wa chuo, sawa na vyuo vikuu vingi duniani,chuo kutokudeal na maswala ya accomodation, wenyewe wanasema, TEACHING, RESEARCH AND CONSULTANCY.kuwa unaishi wapi is none of their business

  Ukija kwa hawa jamaa wa accomodation, wao priority ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza,foreigners na wasichana ndio wanapewa first priority.

  kwa hiyo utaona wazi chuo hakijaweka mazingira ya rushwa au ufisadi, kwa wanaokaa mtaani, unahaja gani ya kutoa rushwa? tataizo tumelelewa katika mazingira na hali kuwa lazima ukae karibu na chuo ili usome vizuri,(boarding issues here). wanafunzi wanaweza kabisa wakakaa mitaani na kujifunza maisha, wajue jinsi ya kulipa maji, umeme na kujipikia.Wengine hivi sasa wanaamka na kuona kumbe unaweza ukakaa mtaani still ukafanya kazi na shule ikaendelea.Malezi yetu ndiyo yanafanya uone hiyo hali.

  Kumbuka kuwa hawa watu, hawajatokea tu chuo ghfla, wametokea katika jamii zao huko walikotoka, wamekaa miaka sita ya secondary, mazingira tofauti n.k.Hivyo urgument yako ya rushwa haitakiwi kuanzia wanapoomba vyumba chuo, issue ya rushwa wanaijua na wametoka nayo tangu huko walikotoka. wizi wa MITIHANI WA HAWA WANAFUNZI ni ishara tosha kabisa kuwa UFISADI hawajaanzia chuoni!!

  Ongezeko la wanafunzi lilipaswa lieendane na ongezeko la infrustructure, lakini tunaona wazi lile ongezeko lilikuwa ni lazima, Tz tuko nyuma sana.

  ISSUE ni kuwa wanafunzi wawe encouraged kukaa mitaani? tatizo mitaani wapi? are they able to catch their buses and dash to lectures on time? angalia traffic jam, angalia huduma za jamii kama maji, umeme n.k ndiyo utakuta mwanafunzi wa mwaka wa nne ambaye hatakiwi kukaa chuo atataka kulala kitanda kimoja na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, kwani mtaani hakutamaniki!

  naona accomodation ni swala dogo kati ya vitu vikubwa vinavyozalisha mafisadi vyuoni

  Vitu gani vinasababisha ufisadi????

  Mikopo ya wanafunzi hawa inatakiwa iwe asilimia 100. kuwepo kwa in-equality and unfairness katika issue za mikopo ndio zinazalisha ufisadi. Just imagine nilipewa mkopo asilimia 50, wazazi wangu wakauza vitu kunisomesha, nikifika OFISINI NITAJARIBU KULIPA FADHILA ZA WAZAZI HARAKA SANA kwa njia ya ufisadi. Imagine pia una wadogo zako ambao hawatasoma kwa sababu wazazi wako waliuza rasilimali ili usome.This will bring someone into pressures za kufanya ufisadi
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Dec 25, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  what do you mean ukisema USAB au DARUSO?

  Rushwa hii iko kila kona, DARUSO huwa hawachukui rushwa directly, ila wanapeleka majina ya watu wasio eligible! na hapa ndio tatizo lilipo. USAB ndio kumejaa uozo, mkuu hii issue ni ya vizazi na vizazi na sio leo, weka antenna zako vizuri!


  Vangi rushwa kubwa zaidi inafanywa na wanafunzi wenyewe kwa kujifanya udalali

  wanafunzi kuuziana vyumba ndiyo fashion ya UDSM na hili USAB na DARUSO hawamo. mwanafunzi ambaye ni eligible kupata chumba akipata anakilipia.kuna uwezekano atakaa mtaani, au atatafuta mtu wa kushare naye, Kile kitanda chake au room yake aliyoilipia atahakikisha anauza mara mbili hata mara tatu ya bei aliyoilipia USAB!!!

  kwa hiyo wanafunzi, DARUSO, USAB...

  Hapa wa kulaumiwa ni nani; issue hii inapaswa ichunguzwe kiundani zaidi. Mtoa maada natambua uchungu wake, ila I am sorry to say, ukitaka kuwa-shape watanzania you need to be crazy before they made you crazy.

  Ushauri wangu usiumize kichwa nenda mtaani katulie na misha

  Yaani kila kona kumeoza
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Weberoya,Nimekupata vyema na nilikuwa miongoni mwa watu waliokumbana na kasheshe hilo la vyumba mwaka 1998. Kweli hata mwaka wa kwanza walikaa off-campus kwa mara ya kwanza.Mimi binafsi niliambiwa nitoe laki moja ili nipewe kitanda pale hall 5 lakini nilikataa na nikakaa mtaani tena mbali. Nakubaliana na wewe kuwa rushwa pale ni kati ya wanafunzi wenyewe kuuziana vyumba na hapa ndo ufisadi unazaliwa.
   
 11. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #11
  Dec 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Suala la Rushwa pale USAB hasa kwa hao mawadern limeshazoeleka na wanafunzi wa Udsm washaliona la kawaida.
   
 12. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #12
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  hivi unadhani kwa ulkimwengu wa sasa ulivyobanjuka,matatizo yote wanayopata hawa vijana wataacha kulipiza kwa kuwa mafisadi??? hakuna wazalendo tena,serious...
   
 13. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #13
  Dec 25, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nadhani tuweke somo/kozi ya Maadili katika mitaala yetu ya ELimu kuanzia shule za Msingi hadi Chuo Kikuu labda inaweza kutwafanya Wanafunzi waone Ubaya wa rushwa. Nakumbuka wakati tukisoma Siasa enzi zile SHule za Msingi na Sekondari tulijifunza kuwa rushwa ni adui wa haki, na tena kabla ya somo la Siasa kuondolewa tulisoma sna kuhusu TANU, ASP na CCM na kukaririshwa ahadi za Mwana CCM....

  Rushwa nia adui wa haki,
  Bitapokewa wala kutoa rushwa,
  Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja... na tulikariri vizuri sana sas tangu waingize hilo somko la Uraia/Civics/General Studies sijui kuna kitu gani. Nakumbuka tulikuwa wanafunzi wa kwanza kufanya mtyihani wa Genral Studies kidato cha Sita na hakukuwa na maudhui ya rushwa wala maadili.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kachukue PCB na polisi then hawa viongozi wa DARUSO wafungwe na wafunguliwe mashitaka ya rushwa na wizi
   
 15. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  tatizo sio rushwa bali uongozi mmbovu??
  kitendo cha kiongozi wa daruso kuwa na vyumba zaidi ya kimoja ni uongozi mmbovu wa chuo, moja kwa moja kwa mkuu wa chuo???

  university lazima iwe na accomodation office ambayo inagawa chumba kimoja kwa mwanafunzi mmoja/student id moja wa mwaka wa kwanza.
   
 16. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Rushwa huzalishwa na UHABA (SCARCITY) full stop. Kitu chochote kinapokuwa kwenye supply ya kutosha rushwa haina nafasi.

  Uhaba wa vitanda vya kulala wagonjwa Muhimbili na hospitali zingine nchini husababisha Rushwa kwa wagonjwa kuwahonga wanaodhibiti upatikatanaji wa vitanda. Uhaba wa bidhaa huko nyuma ulisababisha rushwa kubwa sana kwa waliokuwa wakifanya kazi RTC. Maafisa mauzo enzi hizo walikuwa kati ya watu wa kutafutwa sana kwani kununua bidhaa ilikuwa hadi uhonge.

  Hadi leo, bidhaa fulani ikipungua, wafanyabiashara hupandisha bei (rushwa) kwa sababu bidhaa haipo ya kutosha na wanaoitafuta ili waipate inabidi kulipia zaidi.

  Mifano iko lukuki ya kuthibitisha hilo.

  Kama mitaani mazingira yangekuwa mazuri, nyumba za kutosha zinapatikana kwa bei zinazoeleweka (si kulipa ada ya mwaka mzima kabla ya kukaa kwenye chumba), hizo rushwa zisingekuwepo asilani.

  Uhaba wa vyumba unazalishwa na watunga sera wanaposema kuwa vyuo havijihusishi na wanafunzi wanakaa wapi (kama anavyosema Waberoya hapa) wakati wanajua mazingira yetu hayajatupa jeuri ya kusema hivyo. Kupata chumba Dar si kazi nyepesi, kuna madalali (wala rushwa) ambao wamejazana mtaani hula fedha kibao za watafuta nyumba za kupanga. Hivyo wanafunzi wakikwepa balaa la wala rushwa wa vyuoni, watakutana na madalali wa mitaani; kwani hatuna mahali maalumu ambapo unaweza kwenda na ukajua nikitaka chumba maeneo gani nitakipata wapi na vipi na kwa gharama gani. Soko la nyumba ni soko la mwenda wazimu na haliko regulated na yeyote na serikali haijihusishi nalo kama vile hakuna mabilioni yanayobadilishana mikono kila mwaka kama kodi za nyumba.

  Kukodisha nyumba ni biashara isiyo rasmi kwa hiyo kila mswahili anajipangia sheria na taratibu zake za upangaji. Wanafunzi wengi wanajaribu kukwepa kutotabirika kwa nyumba nyingi za mitaani na wako tayari kutoa rushwa kubwa ili kupata vyumba ndani ya maeneo ya chuo. Kuna kitu kinaitwa baraza la nyumba; kitu ambacho kinatakiwa kuregulate hili soko, lakini ukweli ni kama hakipo kabisa.

  Hili soko la nyumba likianza kudhibitiwa wapangishaji wote wa nyumba wakatakiwa kusajiri nyumba zao za kupangisaha mahali fulani, wakapewa leseni kama wafanyabiashara wengine na wakapewa masharti ya biashara kama wafanyabiashara wengine; hili tatizo litaisha mara moja. Tatizo lipo kwa sababu wanafunzi wanaogopa kuingia mtaani kwani wenye nyumba hawatabiriki na sheria na taratibu za upangaji ni juu ya mwenye nyumba kuamua. Hali hii imesababisha artificial scarcity ya nyumba.

  Je ni kweli kuwa serikali haiwezi kudhibiti soko la nyumba na kutunga sheria itakayowafanya wapangishaji wote wa nyumba wachukuliwe kama wafanyabiashara wengine? Uwezo upo na ni suala la kuamua tu. Serikali inapoteza mapato mengi sana kwa sababu kodi za nyumba wanazolipwa wenye nyumba hazitozwi kodi kwa sababu nyumba nyingi hazijasajiliwa kama nyumba za biashara.

  Hili ni tatizo dogo tu linaloweza kumalizwa na mtu mmoja makini hapo serikalini; wala si rais. Anaweza kuwa waziri wa ardhi na makazi!!
   
 17. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KipimaPembe,

  Umenena. Kama ulivyosema, tatizo hili ni dogo sana. Ni suala la uamuzi. Dodoma University pale hakutakuwa na tatizo la wanafunzi kukosa vyumba japokuwa watakuwa 40,000. Ukiangalia takwimu za wanafunzi wasio na vyumba UDSM na vyuo vingine, Serikali ikiamua kwa kutumia mikopo toka Pension and Social security Funds, ina uwezo wa kulimaliza tatizo la ukosefu wa vyumba kwa wanafunzi ndani ya miaka miwili kwa vyuo vyote vya umma.
   
Loading...