Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

Since 2010 tumekuwa tunaambiwa NSSF imefilisika imebaki fupa lakini ndio unazidi kufanya uwekezaji wa Mabilion ikiwemo daraja la kihistoria sasa sijui Kamusi zao neno kufilisika linatafsiriwa vipi?
Inaweza Kuwa ina maana mpya.....!?
 
Ubia katika kuendeleza mji wa Kigamboni

NSSF iliiingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate.Katika mkataba huo Azimio ilitakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi iliyopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awali ingeanza na ekari 300. Jumla ya gharama za mradi ni USD 653.44M ambapo NSSF ingetoa 45% ya gharama na Azimio ingetoa 35% na ardhi inayodhaminiwa kwa 20% ya gharama ya mradi.

Ukaguzi wa hatimiliki unaonyesha kuwa Azimio inamiliki viwanja viwili yenye ukubwa wa 1.98 hekta na 114.11 hekta, hatimiliki hizi jumla zina ukubwa wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye hekari 300 zilizopangwa.

Hata hivyo CAG hakupatiwa ya hatimiliki ya ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uhangiaji katika mtaji. Hivyo hakuna uthibitisho wa uwepo wa viwanja hivyo ekari 19,700. Fedha za NSSF zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea.


Utekelezaji wa Mkataba wa Ubia katika mradi wa Mji wa kisasa Arumeru kati ya NSSF na Azania Housing Estate

Kwa mwaka 2014/2015 NSSF ilipokea upembuzi yakinifu wa mradi pendekezwa kutoka Azania ambapo bodi ya wazamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na Azania mkoa wa Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha.

Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9 na ilipangwa bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji.Hata hivyo kiasi kiliongezwa mpaka bilioni 43.9 bila idhini ya bodi ya uthamini.

Tarehe 20 January 2016 NSSF na kampuni ya Azania walisaini kusitisha utekelezaji wa mradi huo kwa makubaliano ya pamoja


Malipo yaliyofanywa na NSSF zaidi ya kiasi kilihokubali USD 9M

CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.

Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.

Kutolewa kwa Mikopo kwa SACCOS zaidi ya inavyostahili

Katika mradi wa mikopo kwa SACCOS, NSSF ilitoa mikopo kwa SACCOS tisa ikiwamo Bumbuli Development Corporation kinyume na sera ya kukopesha shirika. Mikopo ilitolewa zaidi ya 50% ya mali za SACCOS. Upembuzi wa awali ulionyesha kuwa SACCOS hizo ziliomba kiasi ambacho hazikustahili. Hata hivyo ushauri ulipuuzwa na uongozi. Hizo SACCOS ni za nani utajaza mwenyewe



S/N JINA LA SACCOS Ziada iliyotolewa

1 Bumbuli Development 948,956,192

2 Korongo SACCOS 481,630,640

3 UMMA SACCOS 63,469,000

4 SBC Saccos 384,770,255

5 Hekima saccos 39,782,033

6 Ukombozi SACCOS 137,097,246

7 Uzinza SACCOS 69,056,896

8 Harbor SACCOS 7,000,000

9 Umoja SACCOS 52, 348,000

To be continued
Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9

Teh teh teh kwi kwi kwi!!
 
Hahahaha!

Mzee wa ripoti ya heka moja milioni 800 Karatu umejitokeza?

Hebu tuwekee kiduchu ripoti hii mifuko PSPF,PPF,GEPF ,LAPF au wewe una deal na NSSF tu.
Leo umeingia ubaridi utadhani umefungiwa kwenye jokofu.
 
Report ya CAG imebeba reports za pension funds zote NSSF,PSPF,PPF, LAPF na GEPF tuwekeeni zote tuchambue kipengele kwa kipengele na mwisho tuone Auditors Opinion ikoje ni Mifuko ipi imepewa hati safi, ipi hati chafu na ipi hati yenye mashaka!
Tuwekee mifuko gani umepata hati chafu na mifuko ipi imepata hati safi.

CAG kafanya yote hayo.

Tunasubiri mkuu.

Title ya uzi inasema NSSF. Mnaweza kuanzisha title nyingine pia. Hata hivyo wizi hauhalalishi wizi mwingine
 
Since 2010 tumekuwa tunaambiwa NSSF imefilisika imebaki fupa lakini ndio unazidi kufanya uwekezaji wa Mabilion ikiwemo daraja la kihistoria sasa sijui Kamusi zao neno kufilisika linatafsiriwa vipi?
ripoti inaonyesha serikali kudaiwa bilioni 723,hata miradi iliyokwama ni kutokana na kukosa fedha
 
Hata hivyo CAG hakupatiwa ya hatimiliki ya ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uhangiaji katika mtaji. Hivyo hakuna uthibitisho wa uwepo wa viwanja hivyo ekari 19,700. Fedha za NSSF zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea.........................................
=hapa ni wazi kuwa hizo hekali 19700 haziko chini ya hiyo azimio,kwani azimio wanamiliki ekali 300 tu,kwahiyo hawako responsible kuwapa hati ya hizo ekari 19700.
Hivi hizo ekari sio zile wakazi wa kigamboni wanatakiwa wapewe fidia?kama ndizo ni wazi kuwa wamiliki hawawezi kutoa hati kabla hawalipwa.
Au nimejichanganya hapa?
 
BOBAN kwa hiyo hii ndiyo ripoti original ya CAG ile ya mwanzo ilikuwa fake?
 
Yap nakumbuka sana mkuu.

Ripoti ya CAG ya sasa imeainisha yote hayo, ukipata muda na nafasi ya kuiona utaisoma.

Hiki alicholeta hapa mleta uzi ni dodoso tu ya ripoti, na kati ya zile kesi 10 ambazo Majaliwa kazidokeza kuwa wataanza nazo mwezi July kwenye mahakama yao ile, hii ya NSSF imo.

Mark that last sentence maana baada ya dakika 10 nitaedit hii comment kufuta hayo maneno.
Teh teh teh!!

Nikipata muda kwenda kusoma ile ripoti yenu ya kwenye vigango?

Mbona ripoti ya CAG hapa chini bofya.

National Audit Office of Tanzania

Pitia kama utakuta ule uharo uliyoleta hapa na kuuita ripoti ya CAG.
 
Back
Top Bottom