OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Ubia katika kuendeleza mji wa Kigamboni
NSSF iliiingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate.Katika mkataba huo Azimio ilitakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi iliyopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awali ingeanza na ekari 300. Jumla ya gharama za mradi ni USD 653.44M ambapo NSSF ingetoa 45% ya gharama na Azimio ingetoa 35% na ardhi inayodhaminiwa kwa 20% ya gharama ya mradi.
Ukaguzi wa hatimiliki unaonyesha kuwa Azimio inamiliki viwanja viwili yenye ukubwa wa 1.98 hekta na 114.11 hekta, hatimiliki hizi jumla zina ukubwa wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye hekari 300 zilizopangwa.
Hata hivyo CAG hakupatiwa ya hatimiliki ya ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uhangiaji katika mtaji. Hivyo hakuna uthibitisho wa uwepo wa viwanja hivyo ekari 19,700. Fedha za NSSF zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea.
Utekelezaji wa Mkataba wa Ubia katika mradi wa Mji wa kisasa Arumeru kati ya NSSF na Azania Housing Estate
Kwa mwaka 2014/2015 NSSF ilipokea upembuzi yakinifu wa mradi pendekezwa kutoka Azania ambapo bodi ya wazamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na Azania mkoa wa Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha.
Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9 na ilipangwa bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji.Hata hivyo kiasi kiliongezwa mpaka bilioni 43.9 bila idhini ya bodi ya uthamini.
Tarehe 20 January 2016 NSSF na kampuni ya Azania walisaini kusitisha utekelezaji wa mradi huo kwa makubaliano ya pamoja
Malipo yaliyofanywa na NSSF zaidi ya kiasi kilihokubali USD 9M
CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.
Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.
Kutolewa kwa Mikopo kwa SACCOS zaidi ya inavyostahili
Katika mradi wa mikopo kwa SACCOS, NSSF ilitoa mikopo kwa SACCOS tisa ikiwamo Bumbuli Development Corporation kinyume na sera ya kukopesha shirika. Mikopo ilitolewa zaidi ya 50% ya mali za SACCOS. Upembuzi wa awali ulionyesha kuwa SACCOS hizo ziliomba kiasi ambacho hazikustahili. Hata hivyo ushauri ulipuuzwa na uongozi. Hizo SACCOS ni za nani utajaza mwenyewe
S/N JINA LA SACCOS Ziada iliyotolewa
1 Bumbuli Development 948,956,192
2 Korongo SACCOS 481,630,640
3 UMMA SACCOS 63,469,000
4 SBC Saccos 384,770,255
5 Hekima saccos 39,782,033
6 Ukombozi SACCOS 137,097,246
7 Uzinza SACCOS 69,056,896
8 Harbor SACCOS 7,000,000
9 Umoja SACCOS 52, 348,000
To be continued