Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9 na ilipangwa bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji.Hata hivyo kiasi kiliongezwa mpaka bilioni 43.9 bila idhini ya bodi ya uthamini.
Tarehe 20 January 2016 NSSF na kampuni ya Azania walisaini kusitisha utekelezaji wa mradi huo kwa makubaliano ya pamoja...

Kama mradi ulisitishwa then why are we still talking about it here?

Kwa ufupi hii ripoti ya kamanda wa bavicha mimi siielewi elewi,labda mkuu sunzu ufafanue,
walipanga nini,chumba,ama walikodi ardhi,haileweki kupanga nini kwa bilioni 2 na kwanini ripoti haielezi kwanini bei ya kupanga sijui plot ama ofisi ilishoot mpaka bilion 40 na ushee
 
CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.
Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.

=hapa pia ni maluelue tu.
Hizo bilioni 9 ni malipo ya nini?
Na hizo bilion 205 zimewekezwa kwenye nini,nini tofauti ya hizo bilion 9 anazosema zimezidi na hizi bilioni 205?
Na pia zile bilioni 43 badala ya bilion 20 zilikuwa za kulipia nini?

Ripoti ya huyu bavicha haifafanui na inachanganya tu
 
Jiwe limetupwa kwenye kichaka tusubiri kutatoka nini naona vindege vinaanza kuchomoka bado kidogo watatoka walengwa
 
Malipo yaliyofanywa na NSSF zaidi ya kiasi kilihokubali USD 9M

CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.

Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.

Hivi hii ripoti ya huyu Bavicha mbona inajichanganya yenyewe pro-Chadema msaidieni mwenzenu.
 
Hata hiyo mikopo hao bambuli inaonekana wamepewa milioni 900,je mikopo hailipwi?,walipewa sandakalawe?
Ni kweli walipewa mkopo kiwango zaidi na wanavyostahili au ni majungu?
 
Iwavo lakini Kwa upande mkubwa Nssf inatuibia fedha zetu.
Unaungia katika miradi kisiasa na mashinikizo.
Miradi hii hauna faida yoyote kwa wana chama hawa wakistaafu.
Fedha watazo rejeshewa ni chache.
Watu wanazungushwa kupewa haki zao.
Nimekwenda pale nikiona watu wanahangaishwa njoo kesho...faili haiinekani..
Na visingizio kibao.
Ni wizi kuchukua fedha za masikini kujijengea majumba wakauziwa matajiri...na wanachama kuhangaishwa kulipwa fedha yao.
 
Prof Ngongo, ripoti ingine ya CAG imetoka karibu tuijadili imejaa data na facts za kutosha.
 
Iwavo lakini Kwa upande mkubwa Nssf inatuibia fedha zetu.
Unaungia katika miradi kisiasa na mashinikizo.
Miradi hii hauna faida yoyote kwa wana chama hawa wakistaafu.
Fedha watazo rejeshewa ni chache.
Watu wanazungushwa kupewa haki zao.
Nimekwenda pale nikiona watu wanahangaishwa njoo kesho...faili haiinekani..
Na visingizio kibao.
Ni wizi kuchukua fedha za masikini kujijengea majumba wakauziwa matajiri...na wanachama kuhangaishwa kulipwa fedha yao.
Mkuu haya malalamiko yako ungeyafungulia uzi tuje kuchangia nadhani hapa tunajadili hii ripoti ya pili ya CAG kuletwa hapa JF.
 
Jamaa wanawaokota mno humu wanatunga scandal hewa na kuweka tarakimu za mabilioni ya kutisha ili kuwateka watu,
hao NSSF Kwani wanamtambo wa kufyatulia hela maana mabilioni yote haya kama yanaliwa ina maana haziishagi?,ha ha ha
bilioni karibu 700 hapa,bilioni 600 pale,huku tena trilioni 1 sijui point 2,wanazitoa wapi?kama si hekaya hizi
 
Ahahahaha!!!

Hawa jamaa bana wao kila kitu ni bilioni tu.

Inadaiwa kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.Uchunguzi unaonesha Azimio iliuza eka 300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113 (sawa na madafu bilioni 217.8), wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa ekari 655 kwa dola 556, 764, 924 (trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla ya fedha ambazo ‘zimeliwa’ katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke yake kufikia trilioni 1.3.
 
Kiufupi ndugu mleta mada, tuwekee ripoti ya CAG tujisomee wenyewe, wewe maelezo yako yana mushkeli
 
Teh teh teh!
 
Kiufupi ndugu mleta mada, tuwekee ripoti ya CAG tujisomee wenyewe, wewe maelezo yako yana mushkeli
Hii nchi ina majipu mengi sana huyu mleta mada naye eti uwa muhajiriwa ofisi ya CAG.

Hahahahaha!
 
c5d340b9cd71ca987c6ae5ae44290b29.jpg
 
Ubia katika kuendeleza mji wa Kigamboni

NSSF iliiingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate.Katika mkataba huo Azimio ilitakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi iliyopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awali ingeanza na ekari 300. Jumla ya gharama za mradi ni USD 653.44M ambapo NSSF ingetoa 45% ya gharama na Azimio ingetoa 35% na ardhi inayodhaminiwa kwa 20% ya gharama ya mradi.

Ukaguzi wa hatimiliki unaonyesha kuwa Azimio inamiliki viwanja viwili yenye ukubwa wa 1.98 hekta na 114.11 hekta, hatimiliki hizi jumla zina ukubwa wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye hekari 300 zilizopangwa.

Hata hivyo CAG hakupatiwa ya hatimiliki ya ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uhangiaji katika mtaji. Hivyo hakuna uthibitisho wa uwepo wa viwanja hivyo ekari 19,700. Fedha za NSSF zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea.

Utekelezaji wa Mkataba wa Ubia katika mradi wa Mji wa kisasa Arumeru kati ya NSSF na Azania Housing Estate

Kwa mwaka 2014/2015 NSSF ilipokea upembuzi yakinifu wa mradi pendekezwa kutoka Azania ambapo bodi ya wazamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na Azania mkoa wa Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha.

Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9 na ilipangwa bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji.Hata hivyo kiasi kiliongezwa mpaka bilioni 43.9 bila idhini ya bodi ya uthamini.

Tarehe 20 January 2016 NSSF na kampuni ya Azania walisaini kusitisha utekelezaji wa mradi huo kwa makubaliano ya pamoja

Malipo yaliyofanywa na NSSF zaidi ya kiasi kilihokubali USD 9M

CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.

Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.

Kutolewa kwa Mikopo kwa SACCOS zaidi ya inavyostahili

Katika mradi wa mikopo kwa SACCOS, NSSF ilitoa mikopo kwa SACCOS tisa ikiwamo Bumbuli Development Corporation kinyume na sera ya kukopesha shirika. Mikopo ilitolewa zaidi ya 50% ya mali za SACCOS. Upembuzi wa awali ulionyesha kuwa SACCOS hizo ziliomba kiasi ambacho hazikustahili. Hata hivyo ushauri ulipuuzwa na uongozi. Hizo SACCOS ni za nani utajaza mwenyewe

S/N JINA LA SACCOS Ziada iliyotolewa

1 Bumbuli Development 948,956,192

2 Korongo SACCOS 481,630,640

3 UMMA SACCOS 63,469,000

4 SBC Saccos 384,770,255

5 Hekima saccos 39,782,033

6 Ukombozi SACCOS 137,097,246

7 Uzinza SACCOS 69,056,896

8 Harbor SACCOS 7,000,000

9 Umoja SACCOS 52, 348,000

To be continued
Ni kweli kabisa mkuu, Kwenye ufisadi ni Dr Dau, ila kwenye ujenzi wa daraja wamefanya wengine
 
Nimeisoma ripot dr dau dini imemsaidia sana yaaani ripot iko safi mbaya ni ushauri tuu umetolewa period hakuna sehemu anayotuhumiwa kufanya ubadhirifu
 
Back
Top Bottom