Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

Udondozi katika ripoti ya CAG kuhusu Dr.Dau na NSSF

teh teh teh
Kumbe wafuasi wa Dauism ni wengi humu eenh.

CAG ndio kamfumua Dau sio mimi, kalie na CAG wako muheshimiwa sana Alhaj Assad sio mimi....
Kamanda unakumbuka hii ripoti yako uliyotuletea.

ujenzi wa Arumeru, inadaiwa kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.

Uchunguzi unaonesha Azimio iliuza eka 300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113 (sawa na madafu bilioni 217.8), wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa ekari 655 kwa dola 556, 764, 924 (trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla ya fedha ambazo ‘zimeliwa’ katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke yake kufikia trilioni 1.3.


Teh teh teh!
 
Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.

Maninaaa!!
 
Ritz una upofu wa udini huwezi kuona ubaya wowote.Tizama hayo kama ni ya "kigango" unaelewa
Mie na upofu wa udini na hawa hapa wagalatia wenzako na hio ripoti yao wanasema ya CAG wana upofu wa nini?

Nasema Dau anahusika kwa sababu si ndiyo alikuwa bosi mkuu? Maana yake ni kwamba hakuna kilichokuwa kikifanyika bila ya yeye kujua. Ni lazima anajua mwanzo mwisho. Mimi naona hata huo ubalozi ungetenguliwa tu kwani ameacha doa NSSF.”Kauli ya kutaka watu wote waliohusika kufisadi fedha hizo wasubulubiwe, pia ilitoka kwa wananchi waliopiga simu kutoka Mwanjelwa Mbeya, Tukuyu (pia Mbeya), Iringa mjini, Mtwara, Simiyu, Kondoa (Dodoma), Tanga na Mwanza.Ufisadi ulioibuliwa hivi karibuni ni kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kinadaiwa kutumiwa na NSSF katika mazingira yanayotia shaka katika ununuzi wa ardhi ili kutekeleza miradi miwili ya ujenzi wa nyumba huko Kigamboni na Arumeru mkoani Arusha. Jijini Dar es Salaam, mfuko huo ulianzisha mradi uitwao Dege Eco Village ambao Bodi ya NSSF iliunda Kampuni ya Hifadhi Builders inayosimamia ujenzi huo ikishirikiana na Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited.
 
Safari ya Kikwete China imefanikiwa 100%.

Amerudi na mradi mkubwa wa reli ya kati kwa standard gauge.

Mwenye wivu ajinyonge.
 
Ubia katika kuendeleza mji wa Kigamboni

NSSF iliiingia ubia na Kampuni ya Azimio Housing Estate.Katika mkataba huo Azimio ilitakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi iliyopo Kigamboni ambapo kwa hatua ya awali ingeanza na ekari 300. Jumla ya gharama za mradi ni USD 653.44M ambapo NSSF ingetoa 45% ya gharama na Azimio ingetoa 35% na ardhi inayodhaminiwa kwa 20% ya gharama ya mradi.

Ukaguzi wa hatimiliki unaonyesha kuwa Azimio inamiliki viwanja viwili yenye ukubwa wa 1.98 hekta na 114.11 hekta, hatimiliki hizi jumla zina ukubwa wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye hekari 300 zilizopangwa.

Hata hivyo CAG hakupatiwa ya hatimiliki ya ardhi ambayo Azimio iliahidi kutoa kama uhangiaji katika mtaji. Hivyo hakuna uthibitisho wa uwepo wa viwanja hivyo ekari 19,700. Fedha za NSSF zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea.


Utekelezaji wa Mkataba wa Ubia katika mradi wa Mji wa kisasa Arumeru kati ya NSSF na Azania Housing Estate

Kwa mwaka 2014/2015 NSSF ilipokea upembuzi yakinifu wa mradi pendekezwa kutoka Azania ambapo bodi ya wazamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na Azania mkoa wa Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha.

Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9 na ilipangwa bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji.Hata hivyo kiasi kiliongezwa mpaka bilioni 43.9 bila idhini ya bodi ya uthamini.

Tarehe 20 January 2016 NSSF na kampuni ya Azania walisaini kusitisha utekelezaji wa mradi huo kwa makubaliano ya pamoja


Malipo yaliyofanywa na NSSF zaidi ya kiasi kilihokubali USD 9M

CAG aligundua kuwa NSSF imewekeza bilioni 205.14, kampuni ya Azania imechangia USD 5.5M kwenye mradi husika.

Makubaliano kati ya NSSF na Azania ilikuwa NSSF itawekeza mpaka thamini ya uwekezaji uwe sawa na thamini ya ardhi iliyotolewa na Azania ndipo pande zote zianze kuchangia katika uwiano ulio sawa. Hii ina maana kuwa NSSF ilichangia USD 9M zaidi ya kiasi ilichotakiwa kuchangia.

Kutolewa kwa Mikopo kwa SACCOS zaidi ya inavyostahili

Katika mradi wa mikopo kwa SACCOS, NSSF ilitoa mikopo kwa SACCOS tisa ikiwamo Bumbuli Development Corporation kinyume na sera ya kukopesha shirika. Mikopo ilitolewa zaidi ya 50% ya mali za SACCOS. Upembuzi wa awali ulionyesha kuwa SACCOS hizo ziliomba kiasi ambacho hazikustahili. Hata hivyo ushauri ulipuuzwa na uongozi. Hizo SACCOS ni za nani utajaza mwenyewe



S/N JINA LA SACCOS Ziada iliyotolewa

1 Bumbuli Development 948,956,192

2 Korongo SACCOS 481,630,640

3 UMMA SACCOS 63,469,000

4 SBC Saccos 384,770,255

5 Hekima saccos 39,782,033

6 Ukombozi SACCOS 137,097,246

7 Uzinza SACCOS 69,056,896

8 Harbor SACCOS 7,000,000

9 Umoja SACCOS 52, 348,000

To be continued
Naomba msaada.
1) Hizo USD 653.44M ni gharama za kuendeleza ekari yote 20,000 za ardhi iliyopo Kigamboni au ekari 300 tu?
2) Ada ya Ushauri kwa kampuni iliyobuni mradi huo ilikuwa ni bilioni 468.9??? Kuna makosa kwenye uandishi au ndio ada yenyewe?
 
Kamanda unakumbuka hii ripoti yako uliyotuletea.

ujenzi wa Arumeru, inadaiwa kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.

Uchunguzi unaonesha Azimio iliuza eka 300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113 (sawa na madafu bilioni 217.8), wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa ekari 655 kwa dola 556, 764, 924 (trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla ya fedha ambazo ‘zimeliwa’ katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke yake kufikia trilioni 1.3.


Teh teh teh!
Yap nakumbuka sana mkuu.

Ripoti ya CAG ya sasa imeainisha yote hayo, ukipata muda na nafasi ya kuiona utaisoma.

Hiki alicholeta hapa mleta uzi ni dodoso tu ya ripoti, na kati ya zile kesi 10 ambazo Majaliwa kazidokeza kuwa wataanza nazo mwezi July kwenye mahakama yao ile.

Mark that last sentence maana baada ya dakika 10 nitaedit hii comment kufuta hayo maneno.
 
Back
Top Bottom