Mlaria Sugu, udini ni ubaguzi unaojielekeza kwenye dini fulani na wala sio wingi wa watu wa dini fulani. Ubaguzi huu, ndio hushabikiwa kama kigezo cha mwelekeo wa mtu au taasisi husika, mathalan, asilimia 98 ya wakaazi wa Zanzibar ni Waislamu, hivyo wanachama wa chama chochote cha siasa Zanzibar ni lazima watakuwa Waislamu, lakini bado chama hiki hakiwezi kuitwa cha kidini, kwasababu Uislamu sio kigezo cha uanachama, lakini chama hicho hicho kama CUF, kwa upande wa Bara, Wakristu ni Asilimia 60% na Waislamu asilimia 40%, lakini wanachama wa CUF bara nao bado ni Asilimia 98%, then, chama hicho kinaweza kubebeshwa shutuma za udini, hata kama hakuna kigezo chochote cha kidini kujiunga na chama husikasa.
Sambamba na Chadema, nguvu kubwa ya chama hiki, imejikita kanda ya Kaskazini ambalo ni eneo la Wakristo wengi, na Kigoma ambao ni Waislamu wengi. Zitto ambaye ni Mwislamu alipotaka kugombea uenyekiti na Mbowe, alipigwa zengwe na hatimaye kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Habari za chini chini zikavuma kuwa Zitto amepigwa zengwe kwa sababu Muslamu kamwe hawezi kuongoza Chadema, hizi ni shutuma za udini, hata kama sio za kweli lakini huo ndio mwelekeo.
CCM imetokana na TANU na ASP, vyote ni vyama vilivyokuwa na waislamu wengi. Baada ya uhuru, Nyerere ambaye ni Mkristo aliwapa uongozi watu wengi walikuwa na elimu nzuri, bahati mbaya ikatokea wengi ni Wakristu, shutuma za Udini pia zilimwangukia.
Mzee Mwinyi alipoachia ruksa kwenye kila eneo, ikatokea Waislamu wengi ndio wenye ndugu Arabuni waliomwagika kwa wingi na kununua karibu majumba yote Kariakoo viwanja sehemu za heri, hivyo nae akabebeshwa tuhuma za udini kuwapendelea Waislamu.
Alipoingia JK kwa kuanzia CCM, alimpiga chini Mangula (Mkristu) kumpa ulaji Makamba (Mwislamu). Kwenye teuzi mbalimbali akawapachika Waislamu akiwemo IGP, Saidi Mwema, Mkurugenzi wa TISS, Rashid Othman, Ramadhani Khalfani (BET). etc. etc. Wale waliokuwa wakizimezea mate posti hizo, ndio wa kwanza kupiga kelele za kichinichini 'udini', 'udini', lakini Wakristu wote walio kwenye posti zote za ulaji miakla yote hawaonekani.
Uchaguzi wa rais, nao unanyemelewa na turufu ya udini, kama vyama vyote vya upinzani wataamua kumsimamisha Dr. Slaa, kuna wana CCM, watampigia kura kwa sababu ya Ukristo wake tuu, wakijisemea kimoyo moyo, huyu ndie mcha Mungu. Na Waislamu vya vyama vyenye mrengo huo, watampigia JK hata kama wao ni CUF, wakijisemea, bora kumpa Mwislamu mwenzao kuliko Kafir.
Matokeo yeyete atakaibuka mshindi, ni kicheko kwa kundi moja na kilio kwa kundi jingine na ndipo mbegu ya chuki za kidini itakapokuwa imepandwa na kuanza kumea, matokeo yake siku zote, huishia kwenye umwagaji wa damu.