Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 12,241
- 10,321
Tumekuwa wepesi wa kusahau au kijisahaulisha au kujifanya hatuoni. Wakati wa Mkapa mbona safu yote 100% ya juuu ilikuwa ni Wakristo?! watu hawakusema au dini ni Uislamu tu labda tukubaliane hapo kwanza.
100%? Hivi Shein ameslimu lini? Na huyu rais wetu wa sasa si alikuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa Mkapa? Na yeye alislimu lini? Tutetee kitu lakini tusiseme uongo.
Ni obvious kuwa kiongozi yeyote atataka kuwa na watu anaowaamini karibu yake. Wengi wao mara nyingi watakuwa washiriki wake kidini. Wengi lakini si wote. Mbona Obama amejaza watu kutoka Chicago na watu hawaoni tatizo? Kinachotakiwa ni utendaji. Wakiboronga wachukuliwe hatua bila kujali dini yao.
Amandla....