Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,090
- 143,305
Wanaweza kuwa waisilamu lakini hawana Uisilamu.Who knows.
Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.
sumu ya ubaguzi huwa haikomi.. ikishaingia kwenye kundi fulani basi kundi hilo huanza wa kubagua. Likimaliza kubagua linatafuta kipimo kingine cha kutumia kubagua. Ukishabagua makabila na kuamua kabila fulani ni duni halistahili, basi unaenda kwenye kipimo kingine; dini. Ukishawabagua watu kwa dini, ukimaliza utajiuliza "hivi wengi ni dhehebu gani?" hivyo utaanza kuwatenganisha Sunni na Shia, Wakatoliki na Waprotestanti n.k mwisho unaweza kujikuta unaanza kubagua watu kwa kuwaanangalia (nani anafanana na Mtutsi)..
La maana ni lazima tuukatae ubaguzi mapema unapojitokeza. Ratio ya CC inasema wajumbe saba kutoka pande zote mbili za Muungano (which is absurdy in itself) hiyo kutoka Zanzibar you'll probably get all seven wakiwa ni Waislamu. Halafu ukija bara wale saba hata wakristu wakiwa wanne bado kwenye general membership utakuta waislamu 10.. Sasa ukija na nafasi za viongozi wanaoingia kwa nyadhifa zao Kikwete, Shein, Karume, Makamba bado namba ya Waislamu inaongezeka. So, hilo ni jambo la mantiki, utaweza kuepuka vipi isipokuwa useme "Zanzibar ichague wakristu, au Bara ilete wagombea wakristu tu" .. na ukishafanya hivyo.. ile sumu itakuwa imekuingia!!
Binafsi nilikataa hayo mambo ya kuita chama fulani cha kidini au kikabila kwa kuangalia idadi ya viongozi. Nililikataa hili kwa CHADEMA na CUF. Ninakataa tena hapa kwa CCM.
Ninachoomba ni wale wenzetu waliotumia kigezo hiki ku-lable vyama vyetu vya CHADEMA na CUF kwamba ni vya kidini na kikabila wasiwe na double standards wakati huu wakijadiliwa CCM. Nakumbuka waliyoongoza hii hoja ni mgongomgongo, Fikira Duni, Kada Mpinzani, Mtalii, Mswahili, Nugwi, na wengine ambao sasa wamebadili majina. Naomba watoke clean waseme hivyohivyo na kwa CCM; vinginevyo kwa ustaraabu uliojengeka katika forum hii watoke mbele waombe msamaha na kuyakana maneno yao.
Mkuu,
Naona hapa umechukia kweli kweli kwi kwi kwi!!!
Hivi Mgongo Mgongo kapotelea wapi?
Kitila utawaweza hao sisiemu na double standard zao. Mie nilishangaa wengi wao wakimuunga mkono hapa mchambuzi kuwa eti rais ajaye lazima awe mkristo at the same time wakipondea CUF eti ni chama cha kidini!
haya yaliyotokea dodoma ingawa hayanisumbui ila kwa standard ambayo wanasisiemu wameika hapa, ingetakiwa waje kuomba msamaha au kutoa maelezo kuhusu hili. Wenyewe utawaona wako kimyaaaaaa
Kitila, ndugu yangu wavumilie tu kwani unachowaomba kufanya ni sawa na kukinga mikono kuombea mvua jangwani!
Bado namsubiri kada atoke hapa, maana nasikia yeye kateuliwa rasmi kuwa msemaji wao kwenye mawasiliano ya internet (wink)!
Mgaya, hawa CCM siku zote hutumia ujanja wao na umbumbumbu wa Wtz kwa maslahi yao kisiasa; ni hao hao ndiyo huanzisha propaganda chafu dhidi ya wapinzani wao kisiasa kwa kuwaita CUF ni chama cha kidini na CHADEMA chama cha kifamilia!
Nijuavyo mimi siku zote composition ya NEC ya CCM na CC yao wengi wao ni Waislam kwa maana ya kuwa NEC ya CCM huwa na idadi sawa ya wajumbe toka pande zote za Muungano. Mara nyingi utakuta upande wa Bara Wakristo wanazidi kidogo au inakuwa 50:50 lakini kwa sababu nusu ya Wajumbe wengine hutoka Zanzibar basi kule utakuta 99% ya wajumbe niu Waislam na hapo lazima NEC ya CCM inakuwa na Waislam wengi vivyo hivyo CC.
Kwa miaka mingi hilo halikuwa tatizo hadi pale Mwalimu Nyerere alipofariki ndipo likanza kuw issue maana hatuna tena mtu wa kukemea upuuzi huo. Sasa hili suala la kazi linapata nguvu kwa kuwa Mwalimu hayupo na Serikali kwa influence ya Waislamu wengi kuwepmo katika NEC na CC ya CCM usishangae hayo unayosema yakawa kweli maana hili suala halikuwahata la kujadiliwa, lingekemewa mapema lakini kwa kuwa wanahisi umaarufu wao (CCM) umepungua wemelazimika kuweka hilo katika Ilani kwa ahadi ya kulitafutioa ufumbuzi suala hilo na ukweli ni kuwa hawawezi kulipatia ufumbuzi sahihi hadi pale watakaporuhusu Mahkama ya Kadhi ianzishwe.
Kwa maoni yangu, madai hayo yanatiwa nguvu na udhaifu uliomo katika Serikali hii ya CCM.