"Udhati, Nia njema, Upendo, Matokeo Halisi", kama matanga ya kusukuma "Maendeleo" ya China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1.jpg


Mwezi Machi mwaka 2013, rais Xi Jinping alifanya ziara yake ya kwanza barani Afrika baada tu ya kuingia madaraka kama Rais wa China. Akiwa nchini Tanzania, alitoa hotuba yenye kichwa "Daima Tuwe Marafiki wa Kutegemewa na Washirika wa Dhati" wakati alipokutana na wenyeji wake katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere, na kuweka mbele dhana ya sera ya " Udhati, Nia njema, Upendo, Matokeo Halisi " na maana halisi ya sera ya Afrika ya mtazamo wa haki na faida.



Wahenga wa Afrika wanasema: "Ndege wa rangi moja huruka kwa pamoja". Maendeleo ya mshikamano na ushirikiano na nchi za Afrika siku zote yamekuwa msingi wa sera ya mambo ya nje ya China, bila kujali China ina tofauti gani ya nguvu na hadhi ya kimataifa. Watu bado wanakumbuka mwaka 2014, wakati virusi vya Ebola vilipozuka Afrika na kuleta madhara makubwa, ambapo Marekani na nchi nyingine za Magharibi zikifunga balozi zao na kuwahamisha wanadiplomasia na raia wao huko Afrika Magharibi, China ilikimbilia Afrika. Baada ya janga jipya la virusi vya Corona kuzuka mwanzoni mwa mwaka 2020, China ikiwa kwenye wakati mgumu zaidi wa kupambana na janga hilo, Afrika ilituma msaada muhimu; na baada ya janga hilo kuenea barani Afrika, China ilisimama kidete na nchi na watu wa Afrika.



Wahenga wa Afrika wanasema "Kidole kimoja hakivunji chawa". Katika miaka michache iliyopita, China na Afrika zimefanikiwa kuwa na ushirikiano wa kivitendo katika maeneo mengi zaidi. Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zikiwa kama taratibu muhimu, China imekuwa mshirika mkuu na mjenzi mkuu wa uboreshaji wa miundombinu barani Afrika, na kusaidia kujenga miradi mikuu mfululizo ikiwa ni pamoja na makao makuu ya Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa(Africa-CDC), Reli ya Mombasa-Nairobi, na Bandari ya Lekki nchini Nigeria, na hata ushirikiano umepenya hadi kwenye maeneo yasiyoweza kufikika barani Afrika.



Wahenga wa Afrika wanasema: "Kila mtu ni faraja ya mwingine". Mwenyekiti Mao Zedong na viongozi wengine wa kizazi cha kwanza cha China Mpya, na kizazi kikongwe cha wanasiasa wa Afrika kwa pamoja walianzisha hali ya ukaribu baina ya watu wa China na Afrika. Leo, vijana wengi zaidi kutoka China na nchi za Afrika wanachagua kusoma, kuishi na kufanya kazi katika nchi za upande mwingine. Mwezi uliopita, matokeo ya Shindano la kwanza la "Meet You" la Watayarishi Vijana wa Video kutoka China na Afrika yalitangazwa. Miongoni mwa kazi hizo, vijana wa China na Afrika walianzisha biashara pamoja, walikula chakula cha mitaani pamoja, walifanya kazi kwa bidii na kukua pamoja, wakionyesha urafiki wao. Kwa mujibu wa Utafiti wa Vijana wa Afrika wa mwaka 2022 uliofanywa na taasisi ya mfuko mmoja nchini Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu, asilimia 77 ya vijana wa Afrika waliohojiwa, wanaamini kuwa katika bara la Afrika, China ndiyo nchi yenye ushawishi mkubwa zaidi nje ya Afrika; 76% walisema kuwa athari za China kwa nchi yao na maisha yao ni chanya. Katika zama mpya, uhusiano kati ya China na Afrika unahitaji juhudi za vijana wa China na Afrika wa vizazi kwa vizazi ili kudumisha milele urafiki kati ya China na Afrika.



Wahenga wa Afrika pia wanasema: "Kutembea peke yako ni haraka, lakini kutembea wengi mtafika mbali ". Ni jambo lisilopingika kwamba maendeleo yoyote hayaji kwa urahisi tu. China na Afrika ziko katika mchakato wa maendeleo ya haraka, na mahitaji yao ya pande zote yanasonga mbele na wakati. Kwa matatizo yanayoibuka kwenye ushirikiano, pande zote mbili zitatatua ipasavyo kwa udhati mkubwa na moyo wa kuheshimiana. Kama alivyosema Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Faki Moussa Mahamat, : China na Afrika ni marafiki, na muhimu zaidi, ni makomredi wanaoshikana, na hakuna kinachoweza kubadilisha au kuharibu uhusiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.



Wachina husema: “bahari haina mipaka, tunasafiri kwa kufuata upepo.” Chini ya unahodha wa wa China na Afrika, " Udhati, Nia njema, Upendo, Matokeo Halisi " vinaendesha Meli kubwa ya "Maendeleo", na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.
 
Back
Top Bottom