UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Ripoti ifuatayo inatudokeza mambo mbalimbali kuhusiana na mpango wa DART - Dar Rapid Transit - yaani Mradi wa Mabasi ya Abiria yaendayo kasi. Bila ya shaka watu wengi wamekuwa wakifiria kwua hiyo DART itakuja na mabasi yake n.k Kama inavyoonekana kwenye ripoti hii DART itahusisha makampuni binafsi katika kusafirisha abiria ambayo yata "qualify". Kwa mujibu wa ripoti hii ambayo "ka-nzi" kalidokeza kuwa imepitiwa hata na WB ni kampuni ya UDA ambayo ina mfumo, uzoefu na hata uwezo wa kuweza kushiriki vizuri kwenye DART.

Kwenye ile mada nyingine wengine tulikuwa tunajiuliza kwanini magenius wetu hawakufikiria kuibadili UDA na kuifanya iwe DARTA (Dar Rapid Transit Agency/Authority)? hasa ukizingatia kuwa ina uzoefu, miundo mbinu, na raslimali watu ya kutosha? Ni mpaka kuisoma ripoti hii ndio kwa upande wangu nimeelewa kuwa UDA imeuzwa kwa watu binafsi ili hao watu binafsi waje kuingia ubia na DART kufanya kitu ambacho kingeweza kufanywa bila UDA kuuzwa bali kuwezeshwa!

Baada ya ya kupitia ripoti hii ikabidi nikimbilia kusoma Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kuhusu Shirika la Usafiri Dar (UDA) niweze kuona alikuwa na maoni gani na kama yamezingatiwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) alisema hivi kwenye ripoti yake ya mashirika ya umma ya mwaka wa 2009/2010:
"Baadhi ya mashirika ya umma yanatakiwa kumilikiwa na Serikali kutokana na aina ya huduma inayotoa katika nchi...Kwa upande
mwingine, usafiri ni tatizo lingine, hasa kwa wanafunzi. Kama Serikali, ingelipa uwezo Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) angalau kuweza kujiendesha kwa nusu ya kiwango cha waendesha mabasi binafsi, tatizo hili kwa wananchi wa kawaida lingeweza kupungua."
Ni katika ripoti hiyo CAG anatudokeza kuwa iko kwenye mpango wa kuuza hisa asilimia 51 zinazomilikiwa na serikali. Wakati huo huo Jiji la Dar lilikuwa na hisa asilimia 49 na hivyo kufanya UDA kuwa shirika linalomiliwa kwa asilimia 100 na watu wa Tanzania. Lakini CAG anatudokeza:
"Jiji la Dar es Salaam limeshindwa kutambua thamani ya sasa ya hisa 3,631,046 zinazomilikiwa katika Shirika la Usafirishaji
Dar es Salaam (UDA) ambazo zilinunuliwa mwezi Oktoba, 2000 kwa Sh.363,104,600."
Sasa, tukiangalia ripoti hii na ripoti hizi nyingine tunabakia na swali moja; kwanini Jiji na au kwa kushirikiana na Serikali Kuu isiendeshe exclusively suala la usafiri wa umma baada ya kuleta Rapid Mass Transit System hasa kwenye Jiji kubwa kama la Dar? Na kutoka hapo kuboresha mfumo wa magari ya Taxi's na usafiri wa tour (vijigari vidogo maalum)? Lengo likiwa kuondokana na daladala? Kwanini suala la Mass Transit kwenye majiji yetu makubwa lisifanywe na Local Cities na Halmashauri za Miji?
 

Attachments

EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
Nadhani kuna issue mbili ambazo ni muhimu kuziangalia. Mwananchi/Citizen kama watu wengine wamelichukulia suala hili kwa mwanga wa "kutouzwa halali" kana kwamba ingeuzwa kwa bei ya juu na halali basi kusingekuwa na issue. Kwangu mimi, tatizo ni zaidi ya kuuzwa kwa bei ya chini, tatizo langu ni kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DAR na kubadilishwa kuwa huo wakala wa Usafiri wa Haraka? Kiakili na kimantiki haikubaliki kuona kwamba UDA iiliyoundwa kusimamia usafiri wa umma jijini la Dar haikubadilishwa na kuifanya iwe ndio DART - yaani angalau wangeweka iwe UDART kuonesha mabadiliko hayo. Tatizo langu ni kuwa kwa jiji kama Dar lenye wakazi milioni karibu 4 wengi wao wakiwa ni wa kima cha chini na kati usafiri wa umma ndio suluhisho sahihi kwa wakazi hao. Haiwezekani kila sikuw awatu wanalalamikia usafiri na congestion lakini hawaoni kwamba kwa mtindo uliopo sasa wanalazimisha watu wengi kuwa na magari yao hata kama si lazima kiuchumi.

Ningefurahi sana kama kungekuwepo na watu kule Mwananchi/Citizen ambao wangeweza kuarticulate hii issue kwa mwanga huo. Tatizo siyo bei ya UDA ilivyouzwa bali gharama ambayo wananchi wanalipa na taifa linalipa hasa jijini Dar kwa UDA kuuzwa.
Uko sahihi. Naona hata bungeni leo wabunge walioghusia hili suala kwenye bajeti ya wizara husika wamelenga zaidi kwenye ufisadi uliofanyika: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-wizara-ya-uchukuzi-yagaragazwa-bungeni.html.

Kuna umuhimu wa kufikiria kwa mapana zaidi.
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
kuhusu suala la UDA ni kuwa hawa jamaa wameuziana kimagumashi sana na hapa nilipo nina nyaraka zenye kur.180 kuhusiana na suala hili na jinsi ambavyo fedha ziliingizwa kwenye account za Idd Simba na Pride. Account hizo ni kama ifuatavyo na kiasi kilichowekwa humo.

Fedha zilitumwa kwenye accounti 0210001002 iliyopo benki M tawi la sea view Dar Es Salaam ambayo ni ya Iddi Simba kiasi cha shilingi milioni mia nne (400,000,000) ziliingizwa na ni kwa maelekezo ya barua yenye kumb.UDA/J.10/06 .

nyingine zilitumwa kwenda account namba 6033500127 account inaitwa Pride Tanzania kiasi cha shilingi milioni 20,000,000 ziliingizwa na hizi ziliingizwa tawi la mlimani city.

kiasi cha shilingi milioni 30,000,000 ziliingizwa kwenye accounti namba 6033500127 na hii ni accounti ya Pride.

hizo ni baadhi ya accounti za Idd simba ambako fedha hizo ziliingiziwa ,

Lingine ni kuwa Juma Kapuya ni miongoni mwa wenye share huko Simon Group na huyu kamati ya miundombinu ilimuingiza kama mjumbe kwenda kuchunguza suala hili.
Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wizara-ya-uchukuzi-yagaragazwa-bungeni-7.html

Hizi nayaraka tutazipataje?
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
kuhusu huyu Simon Group ni kuwa alichopeleka kwa ajili ya kununua hisa alisema yafuatayo kwa barua yao yenye kumbukumbu namba UDA/T.20/3 ya tarehe 12/01/2010 ni kuwa anataka kufanya mambo yafuatayo;

1. kununua mabasi 150 kwa ajili ya usafiri jijini DSM yanayotumia nishati ya gesi.
2. kununua mabasi 50 ya luxury yatakayotoa huduma nchi jirani za DRC,RWANDA,ZAMBIA NA MALAWI.

wamesema kuwa fedha hizo ni za kwao wenyewe na watatumia kiasi cha shilingi 39 bilioni , na pia watakopa kwenye mabenki ya nje na ndani.
Kaaazi kweli kweli.
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
MPs: Arrest those behind UDA sale deal

Pressure mounted yesterday on the government to terminate the reported sale of Dar es Salaam transport company (UDA), with some Members of Parliament demanding the arrest of those behind the deal, which they roundly described as "a sham." On the day the media revealed that up to Sh320 million in reported commitment fees for UDA purchase ended up in the private accounts of its board chairman and former cabinet minister Iddi Simba, the saga took centre stage in Parliament as government came under severe criticism over the manner in which it has handled the matter.

The chairman of the Parliamentary Committee for Infrastructure, Mr Peter Serukamba (Kigoma Urban-CCM), shadow minister for Transport Mohanga Said Ruhwanya (Special Seats-Chadema) and several MPs rooted for investigations while noting that there were grave mistakes in the deal that raise suspicions. MPs Abdi Karim Shah (Pangani-CCM) and Dr Charles Tizeba (Buchosa-CCM) were among those who demanded that the Controller and Auditor General (CAG) and the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) be immediately dispatched to carry out a special probe of UDA affairs. They were contributing to the budget of the Transport ministry which was tabled in the National Assembly yesterday by minister Omar Rashid Nundu (Tanga Urban-CCM).

Mr Nundu irked the MPs when in his budget plan, he appeared to skirt around the controversy surrounding the sale of the company, which is owned jointly by the government and the Dar es Salaam City Council. Despite revelations that the government's stake had been sold to a private company, Simon Group Limited, Mr Nundu told Parliament his ministry would engage a consultant this year to carry out an asset audit and prepare UDA for privatisation. According to the minister, investors who showed interest had been found wanting.

However, Mr Serukamba noted that the government was in the dark, and suggested it immediately summons a shareholders' meeting to review the whole process that led to the sale of its shares and the contract with Simon Group.Mr Serukamba said his committee has in the meantime formed a team to closely monitor developments and report back to Bunge.

Ms Ruhwanya said it was surprising that Simon Group that was rejected in 2008 over single sourcing concerns was back in the picture.The shadow minister queried the whereabouts of Sh320 million paid by the private firm, ostensibly as part of a total of Sh400 million in commitment fees. She said despite owning property estimated at over Sh12 billion, the sale of the state's 49 per cent stake at UDA was pegged at just Sh1.2 billion.

MPs: Arrest those behind UDA sale deal
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Kuna mambo mengi ya kujiuliza, na linalonisumbua ni kuhusu uuzwaji wa UDA. Hivi shirika lililoanzishwa kwa sheria na ambalo limetoa huduma kwa wakazi wa jiji la Dar kwa miaka dahari inafikiaje liuzwe bila wakubwa wa serikali kujua? Ina maana ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya rais haikujua biashara hiyo! Kweli?

Tullikuwa na shirika la KAMATA na lilipokufa ilipitishwa sheria ya bunge kuhitimisha ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kugawa mali na madeni.
Imekuwaje UDA mambo yafanyike uani bila serikali kujua?
UDA ina uhusiano mkubwa sana na jiji ikiwa ni pamoja na madiwani, je na wao hawakujua au kuuliza kwanini mambo yanakwenda kienyeji namna hii? na miongoni mwao ni mameya na madiwani vijana!!!

Ikifika hapo sioni mantiki ya PCCB kuchunguza,kwanza PCCB ilipaswa kujua hujuma hizi kupitia vyombo mbali mbali kama usalama wa taifa. Endapo kila kitu lazima kitoke bungeni ili PCCB kufanyia kazi ni wazi hicho ni chombo cha ajabu kupewa kazi nzito ya kuchunguza utumbo wa namna hii.
Pili kama walivyofanya Richmond wanaweza kuja na hadithi ili kuua hili suala. Nadhani ingeundwa kamati kama ya Richmond na taarifa iwekwe wazi.

Tujiulize, endapo UDA imekuwa inatoa huduma miaka mingi katika bara bara mbovu za Dar, na sasa tunatarajia kuwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi kwanini kusiwe na jitihada za kuliboresha shirika na huduma hiyo mpya.
'Basing on the current strategic plan of UDA and with experienced partners capable of providingcapital and professionals in BRT this company could attain the status needed to participate in the​
DART project. However, with the given short period of time, the Company needs to be
aggressive and fast to solicit for such arrangements' NIT report page 29.
Katika miji mingi duniani usafiri wa umma upo mikononi mwa umma. Kama kuna haja ya uwekezaji basi uwe katika taratibu zinazokubalika na kueleweka.

Kitendo cha kuuza mali za UDA ni njia ya kuua usafiri wa umma na kwa mwendo huo tusitarajie dala dala kuleta ufanisi. Kama dala dala zinataka zilete ufanisi basi inabidi ziwe katika makampuni makubwa yenye kuweza kuwekeza na si mtu mmoja na coaster kwa ujumla wa dala dala 5000. Hii ni vurugu mechi ambayo wenzetu wanaojua taratibu hawakubaliani nayo.

'It should be noted that with exception of the Shirika la Usafiri Dar es Salaamand Cordial Transport Services Public Limited Company, other commuter operators in Dar esSalaam confirmed not having neither well documented annual reports, strategic plans, business profiles nor preventive maintenance schedules. This compelled the consultant to review and evaluate operating framework of the two companies only'

Recommendation
Given the current local transport industry conditions (bus and truck operators)and basing on the consultant's international experience on BRT, we believe thatit is extremely difficult to build a corporate structure suitable to operate DARTsystem without the cooperation from investors and international commuter busoperators with proven expertise on BRT systems to enhance local capacitybuilding.
Basing on the current strategic plan of UDA, through Public Private Partnershipwith experienced partners capable of providing capital and professionals in BRTthis company could attain the status needed to participate in the DART project.However, with the given short period of time, the Company needs to beaggressive and fast to solicit for such arrangements. Subsequently the current commuter bus operators could participate in the DART project through UDA

Ukisoma report kwa makini utaona mambo yameanza kwenda kombo zaidi 2006, hapa ndipo tunajiuliza nini kimetokea?
Taarifa hii ya utafiti ilikuwepo serikalini, nini kimetokea shirika likauzwa kinyemela bila serikali kujua?
Na katika taarifa hii mbona sijaona mahali pametajwa Simon Company japo kupata idea ya kampuni?

Ijue UDA Brochure
UBORA NA USALAMA​
Katika kuhakikisha mabasi ya UDA yapokatika ubora na usalama kwa abiria wakekampuni inazingatia mambo kama;-Matengenezo ya mara kwa mara kablaBasi halijaanza mzunguko,-Kutokubadilisha njia Basi lilipopangiwa,-Kuajiri madereva wenye ubora,-Usafi wa mabasi wa mara kwa mara,-Kuajiri makondakta wenye ubora na wanaotambua na kuthamini haki za abiria​


Kwa wale waliosihi wakati huo mtakumbuka UDA ilikuwa inakwenda kwa 'time' na utaratibu wa kupakia na kushusha. Tunakumbuka breki za UDA na ilikuwa nadra kusikia ajali za mara kwa mara.

Hii ni hujuma kubwa na inahusisha mikono mingi na mizito!
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
Pinda aagiza waliohujumu UDA wachunguzwe

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewaagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina wa madai ya wizi katika Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA). Katika agizo hilo, Pinda amesema, baada ya uchunguzi huo, watakaobainika kulihujumu shirika hilo wawajibishwe mara moja.

Akitoa ufafanuzi bungeni jana, Pinda alisema kanuni ya 38(4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, inaruhusu kutolewa kwa ufafanuzi kwa jambo linalojadiliwa bungeni lenye umuhimu na maslahi makubwa kwa umma. "Serikali imesikia kilio cha wabunge, kwa sasa tumeviagiza vyombo hivyo kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa serikalini mapema iwezekanavyo, alisema Pinda na kuongeza: "Baada ya uchunguzi huo, tutachukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa watakaobainika kulihujumu shirika hili," alisema Pinda.

UDA inasemekana kuuzwa isivyo halali na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, akiwamo Meya wa Jiji hilo, Didas Masaburi, Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba. Wengine wanaohusishwa na kashfa hiyo ni Mkurugenzi wa Jiji, Bakari Kingobi, Meneja Mkuu wa UDA, Victor Milanzi na viongozi wengine akiwamo Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya, ambaye ilielezwa ana hisa 10,000 kwenye kampuni ya Simon Group inayodaiwa kununua UDA isivyo halali.

Katika hatua nyingine, wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam na wadau wa mkoa huo, walitoa tamko la kusikitishwa na tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa taratibu kwenye shirika hilo na kusema wako tayari kutoa ushahidi kwa vyombo vilivyopewa kazi ya kuchunguza kadhia hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini hapa, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa huo, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), alisema pamoja na Serikali kuagiza uchunguzi wa suala hilo, wabunge hao wanaomba pia isitishe mara moja mkataba batili wa ununuzi wa UDA. "Tumekubaliana sisi wabunge wote wa Dar es Salaam, tuko tayari kutoa ushahidi kwenye vyombo hivyo, pamoja na kushirikiana na Serikali kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa, ili kulinda mali za umma," alisema Mtemvu.

Alisema uamuzi wote uliofanywa na Meya Masaburi ambao unataja kuridhiwa na vikao vya Jiji ni batili kwa kuwa ulifikiwa na vikao visivyo halali. Aliongeza kwamba uamuzi huo pia ulifanywa bila kuheshimu maelekezo ya barua ya ofisi ya Waziri Mkuu ya Februari 28 mwaka jana, ikiagiza kusitishwa mara moja kwa mchakato wa kuuza hisa ambazo hazijagawiwa. Aliongeza kuwa vikao hivyo vya kamati ya uongozi na Baraza la Madiwani viliitishwa kinyemela wakati wabunge wakihudhuria mkutano wa Bunge la Bajeti mjini hapa, hivyo wabunge wa mkoa huo kutoshirikishwa.

Alisema mikutano maalumu ambayo ni batili, iliitishwa kuhalalisha uamuzi haramu wa Masaburi kwa kikao cha Kamati ya Fedha na uongozi cha Juni 29 na cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji Julai 20. Mtemvu alitoa mwito kwa wakazi wa Jiji hilo kuwaunga mkono wabunge hao ili kuhakikisha mali za umma zinasimamiwa kikamilifu na watakaobainika wamehujumu UDA, wachukuliwe hatua za kisheria.

HabariLeo | Pinda aagiza waliohujumu UDA wachunguzwe
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Mimi bado naona ni maigizo tu! haiwezekani mh Waziri mkuu hakujua uhalifu huu, haiwezekani ofisi ya Rais haikujua uhalifu huu. UDA ni shirika kubwa sana na kama viongozi hawakujua! basi ipo siku tutaamka asubuhi na kusikia wilaya ya Kibondo imeuzwa Burundi na hakuna anayejua.

Uhalifu wa UDA unahusisha mikono mingi na mizito, si DCI, PCCB, wala CAG wenye ubavu wa kuhoji.
mh Pinda anatumia ile njia inayotumika kuwadanganya Watanzania yaani kuunda tume au kuagiza uchunguzi.
Hakuna anayeweza kwenda kuhoji mikono iliyojaa uchafu wa UDa ni mikubwa sana ina watu wakubwa sana, pinda anahadaa ili kufunika kombe.

Mnakumbuka uchunguzi uliokuwa umeagizwa ufanywe na IGP, AG,PCCB kuhusu EPA umeishia wapi! hakuna taarifa miaka 6 sasa. Kimya!!
Siku 10 zilizopita Jairo ilikuwa hot issue,ikazungushwa zunguswa na tukaambiwa siku 10 kila kitu hadharani, iko wapi hakuna kesi wala nini, Jairo ni wao hawawezi kumtosa ndio maana Pinda alikuwa ananjiuma uma kuhusu maamuzi.

Mtakumbuka kuwa UBT (ubungo bus terminal) kulikuwa na madudu na Waziri mkuu Pinda akasema haiwezekani, akaagiza CAG afanye uchunguzi, je kuna mtu anajua nini kiliendelea? Hivi Pinda anaweza kumchukulia hatua Kingunge kweli!! Alilazimika kusema anafanya uchunguzi ili kutuliza hasira za wanaoibiwa lakini rmoyoni alijua hana la kufanya.

Leo Pinda huyo huyo anaunda tume ya kuchunguza UDA!!! kama hakuweza kumwajibisha Jairo hata kwa simu kutoka kwa mkuu wake, sijui anawezaje kugusa mikono ya UDA. Jamani mikono ya UDA ni mizito sana, hapa Mh Pinda kaagiza mchezo wa kuigiza, hakuna lolote lile litakalofanyika.

Tusichoke, tumwambie Mheshimiwa Waziri mkuu Pinda, ujanja anaofanya wa kufunika wizi huu wa mali zetu kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa rasilimamli zetu miaka nenda rudi, sisi wananchi tunajua fika. Tuna hasira na uchungu na nchi yetu, na msidhani mtatudanganya kila siku kila mwaka na kila saa.

Hakuna aliyejua kuwa Hosni Mubarak angeishiwa nguvu za kidola na kimamlaka hadi kufikishwa kizimbani.

Mchezo mnaocheza wa kuunda tume au uchunguzi usiokuwa na mwanzo wala mwisho ili kulindana tunaujua, na nyote mnaingia kumbu kumbu za vitabu vyetu na historia ya nchi yetu, pengine mola akijaalia ipo siku tutawaomba mtoe ufafanuzi!
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
Pinda sasa amekuwa a non-executive prime minister. Anachofanya inaonyesha ni jinsi gani amekuwa exceluded completely from the executive. He does not even have the theoretical executive power or any role, even formal within the government. Kila wakati ikitokea ufisadi anaunda timu au kuamuru uchunguzi ufanyike. Lakini hakuna hakuna ripoti yoyote inayotolewa juu ya hizi chunguzi. Completely waste of time and money wakati vitu viko so obvious.

Eti anasema "Serikali imesikia kilio cha wabunge, kwa sasa tumeviagiza vyombo hivyo kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa serikalini mapema iwezekanavyo." Ana maana kama sio kilio cha bunge, serikali ingeweka kapuni suala la UDA? Ana maana kuwa serikali inapambana na ufidadi pale tuu inaposukumwa na bunge? Ana maana kuwa tokea huu ufisadi ugundulike bado CAG, DCI na TAKUKURU hawajafanya uchunguzi wowote? BTW uchunguzi alioamuru Pinda utafanyajwe wakati kuna kesi mahakamani?

Hatua aliyochukua Pinda inadhihirisha kuwa serikali ilikuwa inajua huu ufisadi lakini ilikuwa haina mpango wa kufanya lolote mpaka pale ilipolazimishwa na bunge. Pinda is completely unable to rein people behaving badly kwenye wizara yake, sembuse wizara nyingine. Kuwa mtoto wa mkulima hakutoshi tuu kama unapanda bila kuvuna. Pinda ataingia kwenye rekodi as the worthlessness prime minister we have ever had.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Pinda sasa amekuwa a non-executive prime minister. Anachofanya inaonyesha ni jinsi gani amekuwa exceluded completely from the executive. He does not even have the theoretical executive power or any role, even formal within the government. Kila wakati ikitokea ufisadi anaunda timu au kuamuru uchunguzi ufanyike. Lakini hakuna hakuna ripoti yoyote inayotolewa juu ya hizi chunguzi. Completely waste of time and money wakati vitu viko so obvious.

Eti anasema "Serikali imesikia kilio cha wabunge, kwa sasa tumeviagiza vyombo hivyo kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa serikalini mapema iwezekanavyo." Ana maana kama sio kilio cha bunge, serikali ingeweka kapuni suala la UDA? Ana maana kuwa serikali inapambana na ufidadi pale tuu inaposukumwa na bunge? Ana maana kuwa tokea huu ufisadi ugundulike bado CAG, DCI na TAKUKURU hawajafnya uchunguzi wowote?

Hatua aliyochukua Pinda inadhihirisha kuwa serikali ilikuwa inajua huu ufisadi lakini ilikuwa haina mpango wa kufanya lolote mpaka pale ilipolazimishwa na bunge. Pinda is completely unable to rein people behaving badly kwenye wizara yake, sembuse wizara nyingine. Kuwa mtoto wa mkulima hakutoshi tuu kama unapanda bila kuvuna. Pinda ataingia kwenye rekodi as the worthlessness prime minister we have ever had.
This is what I'm talking about EMT. Anajua kila kitu ila uchunguzi ni kwa ajili ya kusikiliza kilio cha wabunge.
Kumbuka huyu ndiye Waziri mkuu aliyewahi kutamka kuwa mafisadi ni watu hatari sana, sasa FISADI wa UDA atawezaje kuwashughulikia!!
Ndiyo maana nasema hakuna uchunguzi ila ni ku buy time, wakijua Watanzani ni wepesi kusahau na waandishi wa habari katika nchi yetu si wa uchunguzi wala ufuatiliaji bali matukio.

Hivi vyombo vya PCCB,DCI,DPP,CAG n.k havina meno vipo kuhalalasha uhalifu. Hivi kuna ripoti gani ataitoa Hosea mtu mwenye akili aiamini, huyu kimaadilili ni 'morally decay' ushahidi ni Richmond, yeye akiwa mtovu wa maadili anapewa kazi ya kuchunguza watovu wa UDA, c'mon!

Hosea hana Public trust, DCI hajui kazi ila kuomba wananchi wampe ushahidi hata kama wizi na mwizi wapo wazi, halafu anaenda kumchunguza fisadi wa UDA! Taarifa ngapi za CAG zimeonyesha ulaji na ubadhirifu wa fedha za umma kuna nini kinatokea zaidi ya kuona CAG akimkabidhi Rais kitabu cha taarifa kwenye magazeti na TV. C'mon! let us stand up, hawa watu wanatufanya ndondocha!! No, let us stand up and tell Hon Pinda we dont trust your investigation!

Kwa hili wanaharakati wanatakiwa walifanyie kazi ikiwa ni pamoja na upinzani na sisi sote. Huu uchunguzi ni upotevu wa pesa na muda, ofisi ya Waziri mkuu M.k.Pinda inajua ukweli wa jambo hili. Tutafuatilia hadi tujue ushiriki wa kila ofisi, tuna uhakika kuwa ofisi ya PM injua kuhusu uozo huu.
 
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
Idd Simba azungumzia kilichotokea

Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua. Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd. Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela. "Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza; "Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema; "Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo. Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma. Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.

Majira.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Mimi nawaambia tuwakatalie tu kubinafsisha mtaona wanavyovurugana.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Idd Simba azungumzia kilichotokea

Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd. Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwaakiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).
"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema; "Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo. Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma. Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo
Nimewahi kuhoji mara 3 kama serikali ilikuwa haijui mpango huu, nashukuru ukweli umejulikana serikali ilikuwa ina taarifa zote na kwahiyo Mheshimiwa Pinda kusema anafanya uchunguzi ni kutafuta muda wa kupoza hasira za wazawa. Wizara zote zipo chini yake na alikuwa na taarifa, na kwa mantiki hiyo uchunguzi unaoendelea kwangu mimi ni kiini macho. Kwanza Pinda angewasimamisha kazi wote wanaotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike, lakini hawezi kwasababu alijua nini kinaendelea.

Simba anasema yeye anauza maneno, Kisena anasema malipo ni ya UDA. Angalia mpraganyiko huo. Na je kwa kanuni za maadili ya kazi hapakuwepo na conflict of interest hapo, yaani mwenyekiti wa bodi inayouza UDA ndiye mtaalamu mshauti(consultant), ha! hii imetokea wapi duniani. Mchezaji Messi anapiga kona halafu anakimbia kwenda kuzuia goli ! ha ha ha ha jamani!

Ili kutaka kutuzuga analeta hoja ya kutaka mzawa amilikishwe UDA, fair enough! mzawa ni nani na aliwezaje kumchagua Simon bila kutoa tangazo kwa wazawa wengine. Hapa Idd Simba anatafuta public sympathy kuwa ana uchungu na nchi hii! Not!

Kama ungefanyika uchunguzi huru halali na wakweli tungeona madudu na mtandao mzima wa ufisadi, lakini kwa kutumia PCCB isiyo na uhalali wa kimaadili, DPP na CAG asiye na meno tumeliwa! changa la macho.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
Kama ungefanyika uchunguzi huru halali na wakweli tungeona madudu na mtandao mzima wa ufisadi, lakini kwa kutumia PCCB isiyo na uhalali wa kimaadili, DPP na CAG asiye na meno tumeliwa! changa la macho.
Halafu Simba ameanza kuchezea hoja ya uzawa tena; ila alichokisema basically kinaweka serikali kuonekana one of the most confused duniani. Yaani sijui ni kitu gani wanakijua kwa uhakika. Tulipoizungumzia TRL wakaanza kubisha mwisho wamevunja mkataba, tuliposema ATCL na dege lao la A320 wakakataa mwisho yakawa yalivyokuwa.. sasa hili.

UDA isibinafsishwe hapo ndio patanoga..
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
Didas Masaburi naye kutafuta mahali pa kujishikiza asisombwe na maji, anasema atawaumbua wabunge waliongia mikataba ya ulaghai. Utadhani hoja ya UDA na mkataba wa machinga complex ni kitu kimoja. Kama alijua kuna matatizo alitakiwa kuyashughulikia kabla ya hili vinginevyo ni mfa maji tu kama yule anayehubiri uzawa wa akaunti yake na si Watanzania.

Ni hao hao akina mwenyekiti na meya walimfukuza Milanzi, sasa leo wanasema Kisena alikosea kuvamia UDA. Wakati haya yote yanatokea hatukujua kuwa Simba ndiye mwenyekiti, na Masaburi alikuwa mstari wa mbele kumfukuza Milanzi. Leo Masaburi ameacha ya Milanzi na sasa anapambana na wabunge.

Hoja asiyotaka kuijibu ni kwanini alifanya vikao na kuwaacha wabunge ambao ni wajumbe muhimu sana katika baraza.
Bado hatujasikia katibu mkuu wa wizara ya miundo mbinu anasema nini kuhusu taarifa za kuuzwa UDA. Je waziri wake hakujua na kama alijua aliwasiliana na mkuu wake ambaye ni Waziri mkuu?

Mkanganyiko huu unawahusu Meya na naibu wake, mameya wa manispaa, mwenyekiti wa bodi ya UDA, 'mzawa' mnunuzi Simon group, Meneja UDA, Katibu mkuu miundo mbinu, Waziri miundo mbinu, Ofisi ya waziri mkuu, hazina na CHC, Wabunge wa Dar, Consultant Idd Simba n.k.

Study iliyofanywa na Watanzania (NIT) imeonyesha wazi kuwa ni mashirika mawili tu UDA liki mojawapo yenye kuendeshwa kwa kanuni za biashara. Consultant ambaye ni mwenyekiti wa UDA anasema serikali imeachia UDA, halafu ni yeye huyo huyo anauza assets zenye thamani ya mabilioni kwa bei anayoijua!!

Watanzania hiki ni sehemu ya madudu, tuachane na uchunguzi wa kulindana. Sasa ni wakati wa kusimama na kusema enough is enough l, no stone to be left unturned, mwenye mkono katika hili aondoke na tukutane Kisutu pale wanapopelekwa vibaka. Tutageuzwa mazezeta hadi lini?
Shirika letu watu wanauza kama fenicha, wameuza 400 tukiwa tumesinzia sasa tumeamka bado tuwashangilie tu! wajinga ni wao au sisi?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
EMT

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,468
2,000
Sasa nafikiri tuna vyombo zaidi ya vitano vinachunguza tuhuma hizi kwa wakati mmoja. CAG, TAKUKURU, Halmashauri ya Jiji, Kamati ya Bunge na taasisi nyingine za serikali. Ina maana tumefikia extent ya hata taasisi zetu kutoaminiana kiasi kwamba kila moja inafanya uchunguzi kivyake?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,933
2,000
T[SIZE=-1]h[/SIZE]e only t[SIZE=-1]h[/SIZE]ing t[SIZE=-1]h[/SIZE]ey are not investigating is t[SIZE=-1]h[/SIZE]e rationale for privatization of UDA. For me its not t[SIZE=-1]h[/SIZE]e price nor t[SIZE=-1]h[/SIZE]e process tat I find appaling and offensive : its t[SIZE=-1]h[/SIZE]e motivation be[SIZE=-1]h[/SIZE]ind t[SIZE=-1]h[/SIZE]e privatization t[SIZE=-1]h[/SIZE]at drives me crazy WE s[SIZE=-1]h[/SIZE]ould NOT PRIVATIZE UDA.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,629
2,000
T[SIZE=-1]h[/SIZE]e only t[SIZE=-1]h[/SIZE]ing t[SIZE=-1]h[/SIZE]ey are not investigating is t[SIZE=-1]h[/SIZE]e rationale for privatization of UDA. For me its not t[SIZE=-1]h[/SIZE]e price nor t[SIZE=-1]h[/SIZE]e process tat I find appaling and offensive : its t[SIZE=-1]h[/SIZE]e motivation be[SIZE=-1]h[/SIZE]ind t[SIZE=-1]h[/SIZE]e privatization t[SIZE=-1]h[/SIZE]at drives me crazy WE s[SIZE=-1]h[/SIZE]ould NOT PRIVATIZE UDA.
This has been my point ab initio, the government is aware of rationale to privatize UDA. Any investigation on the same will unveil libertine if not dubious business.The only way to circumnavigate the vice is to complicate the process. The whole process is well known by the authority.
In the end the buck stops with either PM or Ikulu.
 
W

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
663
195
MM, kwa level yako ya uandishi wa mada, ni watu wachache tena makini, wanaoweza kuona mudhui ya mada zako. Wasamehe bure hawa wengine kwani tayari ni waathirika wa mfumo.
 
Top Bottom