EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Nadhani kuna issue mbili ambazo ni muhimu kuziangalia. Mwananchi/Citizen kama watu wengine wamelichukulia suala hili kwa mwanga wa "kutouzwa halali" kana kwamba ingeuzwa kwa bei ya juu na halali basi kusingekuwa na issue. Kwangu mimi, tatizo ni zaidi ya kuuzwa kwa bei ya chini, tatizo langu ni kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DAR na kubadilishwa kuwa huo wakala wa Usafiri wa Haraka? Kiakili na kimantiki haikubaliki kuona kwamba UDA iiliyoundwa kusimamia usafiri wa umma jijini la Dar haikubadilishwa na kuifanya iwe ndio DART - yaani angalau wangeweka iwe UDART kuonesha mabadiliko hayo. Tatizo langu ni kuwa kwa jiji kama Dar lenye wakazi milioni karibu 4 wengi wao wakiwa ni wa kima cha chini na kati usafiri wa umma ndio suluhisho sahihi kwa wakazi hao. Haiwezekani kila sikuw awatu wanalalamikia usafiri na congestion lakini hawaoni kwamba kwa mtindo uliopo sasa wanalazimisha watu wengi kuwa na magari yao hata kama si lazima kiuchumi.
Ningefurahi sana kama kungekuwepo na watu kule Mwananchi/Citizen ambao wangeweza kuarticulate hii issue kwa mwanga huo. Tatizo siyo bei ya UDA ilivyouzwa bali gharama ambayo wananchi wanalipa na taifa linalipa hasa jijini Dar kwa UDA kuuzwa.
Uko sahihi. Naona hata bungeni leo wabunge walioghusia hili suala kwenye bajeti ya wizara husika wamelenga zaidi kwenye ufisadi uliofanyika: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-wizara-ya-uchukuzi-yagaragazwa-bungeni.html.
Kuna umuhimu wa kufikiria kwa mapana zaidi.