UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Ripoti ifuatayo inatudokeza mambo mbalimbali kuhusiana na mpango wa DART - Dar Rapid Transit - yaani Mradi wa Mabasi ya Abiria yaendayo kasi. Bila ya shaka watu wengi wamekuwa wakifiria kwua hiyo DART itakuja na mabasi yake n.k Kama inavyoonekana kwenye ripoti hii DART itahusisha makampuni binafsi katika kusafirisha abiria ambayo yata "qualify". Kwa mujibu wa ripoti hii ambayo "ka-nzi" kalidokeza kuwa imepitiwa hata na WB ni kampuni ya UDA ambayo ina mfumo, uzoefu na hata uwezo wa kuweza kushiriki vizuri kwenye DART.

Kwenye ile mada nyingine wengine tulikuwa tunajiuliza kwanini magenius wetu hawakufikiria kuibadili UDA na kuifanya iwe DARTA (Dar Rapid Transit Agency/Authority)? hasa ukizingatia kuwa ina uzoefu, miundo mbinu, na raslimali watu ya kutosha? Ni mpaka kuisoma ripoti hii ndio kwa upande wangu nimeelewa kuwa UDA imeuzwa kwa watu binafsi ili hao watu binafsi waje kuingia ubia na DART kufanya kitu ambacho kingeweza kufanywa bila UDA kuuzwa bali kuwezeshwa!

Baada ya ya kupitia ripoti hii ikabidi nikimbilia kusoma Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kuhusu Shirika la Usafiri Dar (UDA) niweze kuona alikuwa na maoni gani na kama yamezingatiwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) alisema hivi kwenye ripoti yake ya mashirika ya umma ya mwaka wa 2009/2010:
"Baadhi ya mashirika ya umma yanatakiwa kumilikiwa na Serikali kutokana na aina ya huduma inayotoa katika nchi...Kwa upande
mwingine, usafiri ni tatizo lingine, hasa kwa wanafunzi. Kama Serikali, ingelipa uwezo Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) angalau kuweza kujiendesha kwa nusu ya kiwango cha waendesha mabasi binafsi, tatizo hili kwa wananchi wa kawaida lingeweza kupungua."
Ni katika ripoti hiyo CAG anatudokeza kuwa iko kwenye mpango wa kuuza hisa asilimia 51 zinazomilikiwa na serikali. Wakati huo huo Jiji la Dar lilikuwa na hisa asilimia 49 na hivyo kufanya UDA kuwa shirika linalomiliwa kwa asilimia 100 na watu wa Tanzania. Lakini CAG anatudokeza:
"Jiji la Dar es Salaam limeshindwa kutambua thamani ya sasa ya hisa 3,631,046 zinazomilikiwa katika Shirika la Usafirishaji
Dar es Salaam (UDA) ambazo zilinunuliwa mwezi Oktoba, 2000 kwa Sh.363,104,600."
Sasa, tukiangalia ripoti hii na ripoti hizi nyingine tunabakia na swali moja; kwanini Jiji na au kwa kushirikiana na Serikali Kuu isiendeshe exclusively suala la usafiri wa umma baada ya kuleta Rapid Mass Transit System hasa kwenye Jiji kubwa kama la Dar? Na kutoka hapo kuboresha mfumo wa magari ya Taxi's na usafiri wa tour (vijigari vidogo maalum)? Lengo likiwa kuondokana na daladala? Kwanini suala la Mass Transit kwenye majiji yetu makubwa lisifanywe na Local Cities na Halmashauri za Miji?
 
Attachments:

rosemarie

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Messages
6,834
Points
2,000
Age
43
rosemarie

rosemarie

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2011
6,834 2,000
thank you for your "input" mwanakijiji!
 
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2009
Messages
372
Points
225
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2009
372 225
Ripoti ifuatayo inatudokeza mambo mbalimbali kuhusiana na mpango wa DART - Dar Rapid Transit - yaani Mradi wa Mabasi ya Abiria yaendayo kasi. Bila ya shaka watu wengi wamekuwa wakifiria kwua hiyo DART itakuja na mabasi yake n.k Kama inavyoonekana kwenye ripoti hii DART itahusisha makampuni binafsi katika kusafirisha abiria ambayo yata "qualify". Kwa mujibu wa ripoti hii ambayo "ka-nzi" kalidokeza kuwa imepitiwa hata na WB ni kampuni ya UDA ambayo ina mfumo, uzoefu na hata uwezo wa kuweza kushiriki vizuri kwenye DART.

Kwenye ile mada nyingine wengine tulikuwa tunajiuliza kwanini magenius wetu hawakufikiria kuibadili UDA na kuifanya iwe DARTA (Dar Rapid Transit Agency/Authority)? hasa ukizingatia kuwa ina uzoefu, miundo mbinu, na raslimali watu ya kutosha? Ni mpaka kuisoma ripoti hii ndio kwa upande wangu nimeelewa kuwa UDA imeuzwa kwa watu binafsi ili hao watu binafsi waje kuingia ubia na DART kufanya kitu ambacho kingeweza kufanywa bila UDA kuuzwa bali kuwezeshwa!

Baada ya ya kupitia ripoti hii ikabidi nikimbilia kusoma Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kuhusu Shirika la Usafiri Dar (UDA) niweze kuona alikuwa na maoni gani na kama yamezingatiwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) alisema hivi kwenye ripoti yake ya mashirika ya umma ya mwaka wa 2009/2010:

Ni katika ripoti hiyo CAG anatudokeza kuwa iko kwenye mpango wa kuuza hisa asilimia 51 zinazomilikiwa na serikali. Wakati huo huo Jiji la Dar lilikuwa na hisa asilimia 49 na hivyo kufanya UDA kuwa shirika linalomiliwa kwa asilimia 100 na watu wa Tanzania. Lakini CAG anatudokeza:

Sasa, tukiangalia ripoti hii na ripoti hizi nyingine tunabakia na swali moja; kwanini Jiji na au kwa kushirikiana na Serikali Kuu isiendeshe exclusively suala la usafiri wa umma baada ya kuleta Rapid Mass Transit System hasa kwenye Jiji kubwa kama la Dar? Na kutoka hapo kuboresha mfumo wa magari ya Taxi's na usafiri wa tour (vijigari vidogo maalum)? Lengo likiwa kuondokana na daladala? Kwanini suala la Mass Transit kwenye majiji yetu makubwa lisifanywe na Local Cities na Halmashauri za Miji?
Mwanakijiji tofautisha Study na Reality pls, Usichanganye watu hapa.Kubinafsishwa kwa UDA hakuhusiani na uwepo wa Mradi wa DART!! Ila tu study iliyofanyika inapendekeza kuwepo na kampuni mbili zitakazotoa huduma ya mabasi, Hata UDA ingekuwepo kama kampuni ya umma ilikuwa na nafasi sawa kujiunga na Mfumo huo wa DART Pls read btn lines!!
Basing on the findings that most of the operators do lack knowledge on DART
operations we strongly recommend that the client should prepare a grievances
plan and urgently implement it to ensure the concerned operators are informed
and involved in the process at the earliest possible stage. Implementation of the
grievances plan should be guided by multi-stakeholders
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Mwanakijiji tofautisha Study na Reality pls, Usichanganye watu hapa. Kubinafsishwa kwa UDA hakuhusiani na uwepo wa Mradi wa DART!! I
Inawezekana unaamini kabisa umesema kitu cha kina sana. Ila ukirudia taratibu utaona ulichosema hakina uzito huo. Mimi ndio nimesema kubinafsishwa kwa UDA kunahusiana na mradi wa DART vinginevyo kwanini UDA imebinafsishwa?
 
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2009
Messages
372
Points
225
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2009
372 225
Inawezekana unaamini kabisa umesema kitu cha kina sana. Ila ukirudia taratibu utaona ulichosema hakina uzito huo. Mimi ndio nimesema kubinafsishwa kwa UDA kunahusiana na mradi wa DART vinginevyo kwanini UDA imebinafsishwa?
Mkuu wewe uko mbali huko majuu yanayotokea Bongo waachie wenyewe.UDA limebinafsishwa kama mashirika mengine yote ya Umma yalivyobinafsishwa.Mbona hukuanza kuulizia kuvunjwa kwa shirika mama la Uchukuzi (NTC) ambalo lilikuwa lina hisa zaidi ya 50 kwa UDA? UDA limeshindwa kujiendesha kibiashara zaidi ya kutoa huduma.Na ujue UDA miaka hii ya karibuni halipati ruzuku hata senti tano kutoka serikalini.UDA unayoijua wewe siyo UDA iliyopo sasa ,Ni tofauti kabisa afadhali hata Daladala kuliko usafiri huo wa UDA.Hata hivyo wazo lako hapa lilikuwa na matiki ila tuu umeanza kwa kueleza U,O,N.G.O zaaidi kuliko fact, uki base kwenye hiyo report ya NIT waliofanya study kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka(DART),
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Mkuu wewe uko mbali huko majuu yanayotokea Bongo waachie wenyewe.
Wenyewe kina nani?

UDA limebinafsishwa kama mashirika mengine yote ya Umma yalivyobinafsishwa.Mbona hukuanza kuulizia kuvunjwa kwa shirika mama la Uchukuzi (NTC) ambalo lilikuwa lina hisa zaidi ya 50 kwa UDA? UDA limeshindwa kujiendesha kibiashara zaidi ya kutoa huduma.
Kwanini?

Na ujue UDA miaka hii ya karibuni halipati ruzuku hata senti tano kutoka serikalini.
Kwanini?

UDA unayoijua wewe siyo UDA iliyopo sasa ,Ni tofauti kabisa afadhali hata Daladala kuliko usafiri huo wa UDA.Hata hivyo wazo lako hapa lilikuwa na matiki ila tuu umeanza kwa kueleza U,O,N.G.O zaaidi kuliko fact, uki base kwenye hiyo report ya NIT waliofanya study kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka(DART),
Sasa wewe sema ukweli. Kwanini UDA imebinafsishwa na kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DART au DART nayo itakuja kubinafsishwa?
 
T

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Messages
443
Points
0
T

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2010
443 0
Pigia Msitari Mwanakijiji. Nimeshangazwa sana kukuta kwamba mwanzoni kabisa mwa hii
report UDA imeanza kupigiwa Chapua la kuwa Key Stakeholder kwenye hii project, wakati
objectives the study hazielekezi kutolewa kwa mapendekezo ya namna hiyo.

Inakuwa ngumu sana kupinga mawazo yako.
Nitarudi baadaye, ngoja nijipinde kuipitia yote, there must be more than eyes could see
 
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2009
Messages
372
Points
225
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2009
372 225
Wenyewe kina nani?Kwanini?Kwanini?
Sasa wewe sema ukweli. Kwanini UDA imebinafsishwa na kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DART au DART nayo itakuja kubinafsishwa?
Hapo sasa ulipaswa kuanzia na siyo kulete porojo kwa jambo usilolijua.Kwanza nimekujibu kwanini UDA imebinafsishwa ni kwamba ilishindwa kujiendesha kibiashara kwa sababu ya ushidani huria wa usafiri wa jijini, Mfumo wa UDA haukutoa nafasi ya kubadilika kutoka mfumo wa zamani wa kiuendeshaji na mfumo wa soko huria. UDA haikuchukua role za DART kwa sababu za kimuundo na mfumo wa uendeshaji ni tofauti kabisa.
DART Agency is a government entity established by GN No.120 of 25th May, 2007 under the Executive Agency Act No. 30 of 1997 and its subsequent amendments. The key role of the DART Agency is to establish and operate the Bus Rapid Transit (BRT) system for Dar es Salaam. The Agency aims at achieving the following objectives;
a) Establish and operate Bus Rapid Transit (BRT) system for Dar es Salaam, branded Dar Rapid Transit – DART,
b) Ensure orderly floor of traffic on urban streets and roads and
c) Ensure effective Management of the Agency.
The Agency operates under the guidance of the Prime Minister's Office, Regional Administration and Local Government – PMO-RALG

Aim
The DART aims at "effectively planning, coordinating and facilitating the provision of urban transport facilities and services and ensuring improved traffic management in Dar es Salaam". Hili halikuwa lengo la UDA
 
zumbemkuu

zumbemkuu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Messages
9,613
Points
2,000
zumbemkuu

zumbemkuu

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2010
9,613 2,000
uuuuuwiiii! everywhere and everything is dirty! tutakimbilia wapi sasa? na bado tunaendelea kusema Mungu anaona....looh!
 
kimatire

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Messages
373
Points
195
kimatire

kimatire

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2008
373 195
Inawezekana unaamini kabisa umesema kitu cha kina sana. Ila ukirudia taratibu utaona ulichosema hakina uzito huo. Mimi ndio nimesema kubinafsishwa kwa UDA kunahusiana na mradi wa DART vinginevyo kwanini UDA imebinafsishwa?
Mwanakijiji wewe ni mchokozi wa mada tuu, Ambaye mara nyingi unakuja na fact fake kuwahaadaa wa-JF kwamba umefanyia research yale unayoongelea,Yamkini mimi binafsi nimekuwanisoma thread nyingi zako ukweli ni asimia chache sana uongo ndo unachukua zamu kubwa zaidi .Kama yule Waziri fulani katika serikali ya JK atatoaaga figures kweli kweli kumbe asilia kubwa ya tarakimu anazowaeleza watu majukwaani ni uongo uliopitiliza,Sasa na wewe una kasumba hiyo.Ukweli umejidhihirisha katika thread hii.Mwana JF Kiroroma amekushushua kwa fact zako ulizoziweka asubuhi ya leo.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Hapo sasa ulipaswa kuanzia na siyo kulete porojo kwa jambo usilolijua.Kwanza nimekujibu kwanini UDA imebinafsishwa ni kwamba ilishindwa kujiendesha kibiashara kwa sababu ya ushidani huria wa usafiri wa jijini, Mfumo wa UDA haukutoa nafasi ya kubadilika kutoka mfumo wa zamani wa kiuendeshaji na mfumo wa soko huria. UDA haikuchukua role za DART kwa sababu za kimuundo na mfumo wa uendeshaji ni tofauti kabisa.
DART Agency is a government entity established by GN No.120 of 25th May, 2007 under the Executive Agency Act No. 30 of 1997 and its subsequent amendments. The key role of the DART Agency is to establish and operate the Bus Rapid Transit (BRT) system for Dar es Salaam. The Agency aims at achieving the following objectives;
a) Establish and operate Bus Rapid Transit (BRT) system for Dar es Salaam, branded Dar Rapid Transit – DART,
b) Ensure orderly floor of traffic on urban streets and roads and
c) Ensure effective Management of the Agency.
The Agency operates under the guidance of the Prime Minister's Office, Regional Administration and Local Government – PMO-RALG

Aim
The DART aims at "effectively planning, coordinating and facilitating the provision of urban transport facilities and services and ensuring improved traffic management in Dar es Salaam". Hili halikuwa lengo la UDA
Serikali iliyounda UDA siyo hiyo ihyo iliyounda DART? Ni mara ngapi Agencies Tanzania zimebadilisha na kuwwa kitu kingine bila kulazimisha kufuta kilichopo? Kwanini hayo yote uliyoyasema yasingefanywa na watu hao hao kwa UDA. Yaani, kwanini malengo ya UDA yasingebadilishwa yaendane na haja ya DART?

Kwa vile DART itatumia pia makampuni binafsi kwanini UDA isingekuwa sehemu ya mpango huo bila kuilazimisha kuibinafsisha kwa chee kwanza?

UDA iliundwa kwa sheria gani na ikiwa na malengo gani yasiyolingana na malengo ya DARTA?
 
Mkaa Mweupe

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
654
Points
195
Mkaa Mweupe

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
654 195
Kama mwendelezo, DART imeundwa toka ndani ya Jiji hivyo unavyosema kuwa serikali kuingilia majukumu ya halmashauri haiingii akilini
 
The Mockingjay

The Mockingjay

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2011
Messages
380
Points
195
The Mockingjay

The Mockingjay

JF-Expert Member
Joined Jan 11, 2011
380 195
We Kiroroma,

Hivi unafahamu ni mara ngapi mashirika ya umma yanakwamishwa makusudi ili yaonekane hayafai kujimudu ili yaende kwa bei che.
Tena mwekezaji si wakati wote ananua kwa bei chee tunayoisikia sie. Hapo ameshakamuliwa 10% nyingi na ma directors, makatibu wakuu. Na wizara ya uchukuzi ndio bingwa wa hizi 10%.
Kwa hiyo unayosema kuwa UDA ilishindwa ni sawa kwa macho ya wengi but ukweli ni most likely it was purposely sabotaged to fail, just like so many other mashirika ya umma.

Nawakilisha
 
Mkuu wewe ni mchanga wa kujua hayo kwa sababu huna uhakika na unachokisema,Inaonyesha umedandia gari kwa mbele.Piga usingizi kwanza ndo uje kwenye forum.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Waziri Kawambwa mwaka jana akiwassilisha bajeti yake alisema hivi kuhusu UDA

65. Mheshimiwa Spika, kuhusu Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Serikali imeendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuiwezesha UDA kuwa na mtaji wa kujiendesha yenyewe, hii ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mapendekezo Serikalini ya kufuta madeni ya muda mrefu ya UDA yenye thamani ya shilingi milioni 612.189 kwa lengo la kuboresha mezania ya Shirika ili iweze kupata fedha kutoka xtaasisi mbali mbali za kifedha. Aidha, kutokana na mapendekezo ya Bodi ya UDA kuhusu hatma ya shirika, Serikali iko katika majadiliano na mwekezaji ambaye amejitokeza kununua hisa za Serikali za aslimia 49. Kupatikana kwa mwekezaji kutawezesha UDA kuongeza uwezo wake wakutoa huduma za usafiri jijini Dar es salaam na kushiriki katika mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Did he say what I think he said? au miye macho yangu yanaona kile wengine hawataki kukiona? Hakuna uhusiano wa ubinafsishaji wa UDA na DART? yeah right.
 
RealMan

RealMan

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
2,366
Points
1,250
RealMan

RealMan

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
2,366 1,250
Mwanakijiji watu hawawezi wakakuelewa.

Watanzania tumeaminishwa na watawala kwamba shirika lisipojiendesha kwa faida dawa yake ni kubinafisisha bila kuangalia tatizo la msingi ni nini.
Tatizo kubwa la serikali haipendi haya mashirika yajiendeshe yenyewe, UDA haihitaji ruzuku ya serikali bali ilitakiwa ipewe uhuru wa kujiendesha kibiashara. Kwa asset ilizonazo UDA hakuna benki itajiuliza mara mbili kutoa mkopo wa mabilioni.

Kwa wasiojua ile stand ya daladala pale stesheni mkabala/opposite na TRA Long Room ni mali ya UDA.

Hayo ya DART mie siyajui na wala sijafungua hilo dokomenti la Mwanakijiji ila nitawapa niyajuayo kisha nisome dokomenti:

Simon Group Ltd kwa sasa anamiliki 52.535% ya hisa zilizobaki wanagawana Halimashauri ya jiji na Serikali/Msajili Hazina. Mwaka jana mwishoni SGL waliingiza kiasi cha Milioni 320 kwenye akaunti ya UDA kama malipo ya hisa zao. Mkataba ulitaka ndani ya wiki 2 mkutano wa wanahisa uitishwe ili kuteua bodi mpya, kumbuka hapo awali bodi ilikuwa chini ya Idd Simba.

Na wasioijua SGL: Hii ni kampuni ya mgombea ubunge aliyeshindwa na Shibuda, anamiliki kiwanda cha pamba Malampaka-Maswa kiwanda cha kukamua mafuta Mwanza iliyokuwa New Era Oil. Ana kampuni ya transport - aliingiza kama truck 100 mpya mwaka 2009.
Wenye kufikirisha akili zetu tunajua what is it all about.

Kwa taarifa zilizopo kati ya hizo mil 320 ni Mil 80 tu zimebaki zingine bodi na meneja wa UDA wanaaminika wamekula bila kunawa. Matokeo yake SGL kama mwanahisa mkuu aliitisha kikao cha wanahisa mwezi Juni tar 10, wameipiga chini bodi ya Idd Simba na kumfukuza kazi Meneja Mkuu (Victor Milanzi).

Kwa sasa ukienda pale UDA utawakuta Ultimate Security (mali ya mtuhumiwa wa ufisadi), ninaamini walinzi wa UDA waanze kutafuta ajira kwingine maana upepo unavuma kuelekea kusi kwa kasi. Kule nyuma kulipokuwa na karakana kubwa mbili, moja sasa hivi kunajengwa kuta kutengeneza magodown - tunasikia TBL wataanza kihifadhi bia pale.

Kule mbele kidogo ya UDA kama waelekea Geti no. 5 kuna eneo/yard alikuwa amepangishwa Manji kifisadi fisadi hawa waheshimiwa wameshamwambia aliachie. Sasa manaweza jua kwamba utajiri wa UDA hauko kwenye idadi ya mabasi.

Mipango iliyopo ni kuzinyakua share za serikali zilizobaki ili SGL awe na zaidi ya 70%.

Waelewa tunajua kuwa UDA ni prime area kwa port operations, wengi mmeona kuna ICD nyingi zimeibuka hivi karibuni na tuna yard za magari (imported) pale Shaurimoyo iliyokuwa mali ya TRC wanajiita TALL na kule Kibasilawapo FALION.

Sasa wenye kufikiri ni DART pekee ndio iko nyuma ya huu wizi halali nadhani tieni fikara mara mbili.

Ni hayo tu kwa sasa
 
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2009
Messages
372
Points
225
Kiroroma

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2009
372 225
Serikali iliyounda UDA siyo hiyo ihyo iliyounda DART? Ni mara ngapi Agencies Tanzania zimebadilisha na kuwwa kitu kingine bila kulazimisha kufuta kilichopo? Kwanini hayo yote uliyoyasema yasingefanywa na watu hao hao kwa UDA. Yaani, kwanini malengo ya UDA yasingebadilishwa yaendane na haja ya DART?

Kwa vile DART itatumia pia makampuni binafsi kwanini UDA isingekuwa sehemu ya mpango huo bila kuilazimisha kuibinafsisha kwa chee kwanza?
Mwanakiji elewa somo awali nimekuambia kuwa DART itashirikisha wadau mbali mbali binafsi kujiunga na uendeshaji wa mfumo huo wa mabasi yaendao haraka, UDA haijazuiliwa kujiunga kama ina ubavu,lakini kama haina ubavu kama hivyo basi ni bora ikijiunga na kampuni binafsi kupata nguvu za kushiriki katika mfumo.Sioni kipingamizi kwani UDA inameuzwa bei cheee au chaaa siyo kwa sababu ijiunge na DART ila ni kuipunguzia serikali kujiingiza kwenye biashara ambazo zimeshindwa.Soma zaidi hapa Dar Rapid Transit - Home
 
Mkaa Mweupe

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
654
Points
195
Mkaa Mweupe

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
654 195
Serikali iliyounda UDA siyo hiyo ihyo iliyounda DART? Ni mara ngapi Agencies Tanzania zimebadilisha na kuwwa kitu kingine bila kulazimisha kufuta kilichopo? Kwanini hayo yote uliyoyasema yasingefanywa na watu hao hao kwa UDA. Yaani, kwanini malengo ya UDA yasingebadilishwa yaendane na haja ya DART?
Nadhani hauelewi au unachanganya mambo, Serikali inaunda vyombo mbali mbali vya kuisaidia jamii kutokana na mahitaji. Katika taratibu za kuunda hivyo vyombo kuna urasimu wake na haiwezekani chombo kilichopo kuongezewa majukumu kwani ni kinyume na 'D2D'. Vile vile Serikali inakosa chombo (ingawa kuna tume ya mipango) kinachosimamia mipango ya Serikali achilia mbali 'Manifesto' za ki-siasa.

Kwa vile DART itatumia pia makampuni binafsi kwanini UDA isingekuwa sehemu ya mpango huo bila kuilazimisha kuibinafsisha kwa chee kwanza?
Kuuzwa kwa chee kwa UDA huo ni mpango wao (Serikali Kuu) na kuwa ni sehemu ya mpango inategemea kama hao (UDA) wameona kuna 'business opportunity'. Kwani katika DART uendeshaji wake ni kwa sera za PPP na sio Serikali kuendesha biashara. Hivyo basi si UDA pekee wangeweza kuwa kwenye huo mpango bali hata wewe unaweza kuwa kwenye huu mpango wa DART.

UDA iliundwa kwa sheria gani na ikiwa na malengo gani yasiyolingana na malengo ya DARTA?
UDA ilikuwa ni sehemu ya urithi kutoka katika ukoloni, nadhani wakati imeundwa PSRC huu mfumo wa BRT ulikuwa bado haujaeleweka, kwa hivyo basi UDA haikuweza kupewa majukumu ambayo DART inayo kwa sasa.
 
Forum statistics

Threads 1,296,485
Members 498,655
Posts 31,249,859
Top