UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,874
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,874 2,000
Ripoti ifuatayo inatudokeza mambo mbalimbali kuhusiana na mpango wa DART - Dar Rapid Transit - yaani Mradi wa Mabasi ya Abiria yaendayo kasi. Bila ya shaka watu wengi wamekuwa wakifiria kwua hiyo DART itakuja na mabasi yake n.k Kama inavyoonekana kwenye ripoti hii DART itahusisha makampuni binafsi katika kusafirisha abiria ambayo yata "qualify". Kwa mujibu wa ripoti hii ambayo "ka-nzi" kalidokeza kuwa imepitiwa hata na WB ni kampuni ya UDA ambayo ina mfumo, uzoefu na hata uwezo wa kuweza kushiriki vizuri kwenye DART.

Kwenye ile mada nyingine wengine tulikuwa tunajiuliza kwanini magenius wetu hawakufikiria kuibadili UDA na kuifanya iwe DARTA (Dar Rapid Transit Agency/Authority)? hasa ukizingatia kuwa ina uzoefu, miundo mbinu, na raslimali watu ya kutosha? Ni mpaka kuisoma ripoti hii ndio kwa upande wangu nimeelewa kuwa UDA imeuzwa kwa watu binafsi ili hao watu binafsi waje kuingia ubia na DART kufanya kitu ambacho kingeweza kufanywa bila UDA kuuzwa bali kuwezeshwa!

Baada ya ya kupitia ripoti hii ikabidi nikimbilia kusoma Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kuhusu Shirika la Usafiri Dar (UDA) niweze kuona alikuwa na maoni gani na kama yamezingatiwa. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) alisema hivi kwenye ripoti yake ya mashirika ya umma ya mwaka wa 2009/2010:
"Baadhi ya mashirika ya umma yanatakiwa kumilikiwa na Serikali kutokana na aina ya huduma inayotoa katika nchi...Kwa upande
mwingine, usafiri ni tatizo lingine, hasa kwa wanafunzi. Kama Serikali, ingelipa uwezo Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) angalau kuweza kujiendesha kwa nusu ya kiwango cha waendesha mabasi binafsi, tatizo hili kwa wananchi wa kawaida lingeweza kupungua."
Ni katika ripoti hiyo CAG anatudokeza kuwa iko kwenye mpango wa kuuza hisa asilimia 51 zinazomilikiwa na serikali. Wakati huo huo Jiji la Dar lilikuwa na hisa asilimia 49 na hivyo kufanya UDA kuwa shirika linalomiliwa kwa asilimia 100 na watu wa Tanzania. Lakini CAG anatudokeza:
"Jiji la Dar es Salaam limeshindwa kutambua thamani ya sasa ya hisa 3,631,046 zinazomilikiwa katika Shirika la Usafirishaji
Dar es Salaam (UDA) ambazo zilinunuliwa mwezi Oktoba, 2000 kwa Sh.363,104,600."
Sasa, tukiangalia ripoti hii na ripoti hizi nyingine tunabakia na swali moja; kwanini Jiji na au kwa kushirikiana na Serikali Kuu isiendeshe exclusively suala la usafiri wa umma baada ya kuleta Rapid Mass Transit System hasa kwenye Jiji kubwa kama la Dar? Na kutoka hapo kuboresha mfumo wa magari ya Taxi's na usafiri wa tour (vijigari vidogo maalum)? Lengo likiwa kuondokana na daladala? Kwanini suala la Mass Transit kwenye majiji yetu makubwa lisifanywe na Local Cities na Halmashauri za Miji?
 

Attachments:

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,852
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,852 2,000
Nakumbuka kuna watu walisema tunaongopea.... leo hawarudi hata kusema "oops"
Au wanashangaa wakijifanya hawajui tulifikafikaje hapa tulipo.
Nadhani wapo busy somewhere wakiutangaza na kuuhubiri Uzalendo
Uzalendo na usaliti, upiganaji uhuru na ugaidi...like beauty, it all depends on the eyes of the beholder!
 
Thread starter Similar threads Forum Replies Date
Red Giant Great Thinkers 2

Forum statistics

Threads 1,390,254
Members 528,131
Posts 34,047,390
Top