Uchumba kuvunjika ...kisa HARUSI



Pale unapopania kucheza "my baby" ya joeboy alafu upande wa mwanaume hawataki sherehe.. mvurugano na mvunjiko lazima utokee.

Ila huyo dada huyo dada nae..angekubali tu sherehe kitu gani bwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri harusi huandaliwa upande wa kiumeni na ni maamuzi yao kufanya ama kutofanya tafrija.

sasa bibie kama anataka sherehe afanye sendoff na kitchen party kwa sababu sherehe hizi huandaliwa upande wa kikeni

Asikubali kuvunja uchumba wake kisa sherehe jamani.
asipokusikia hapa basi tena
 
Huyo mzee wake ningekuwa na pesa ningemrushia.

Huyo dada hana akili kabisa. Idiot
Wasalaam

Iko hivi ...Ni rafiki wa karibu wa familia yetu,ameajiriwa na taasisi ya fedha mwaka wa tatu huu Yuko kwenye mahusiano na mdada waliekutana chuo...Ni muda kiasi tunamuita shemeji yetu

Jamaa anataka kutoa mahari,lakini mwanamke amegoma anasema mpaka jamaa akubali sharti la kufanyika harusi

Familia ya jamaa yetu,Ni watu wenye uwezo wao kiasi,ila mzee wao Ni mtu wa kuchukia Sana Sherehe na harusi,anasema atachangia misiba na majanga mengine sio mambo ambayo mtu anayapanga mwenyewe halafu anasumbua watu kwa michango,ndivyo anavyishi

Dada za mshikaji wameozwa Tena kwa mahari ndogo,harusi hakuhudhuria,ila baada ya hapo aliwapa kiasi Fulani (kikubwa) Kama Cha kuanzia maisha,imekua utaratibu wake

Na mwaka Jana Kaka yake mshikaji kaoa kwa mtindo huo huo...alienda half day jmos...akatoka kuwaambia staff wenzie naenda funga ndoa ,hawakuamini,lakini jamaa alifunya ndoa,na home walikuja watu wachache tuu kwa ajili ya evening dinner

Jamaa anasema sio kuwa Hana uwezo,ila Ni namna Anaona atamhuzunisha mzee wake ..mzee wake kamwambia mikosi na mambo ya shetani huanzia kwenye tafrija/Sherehe...anasema Ni kujikweza...jamaa atanye Nini tukivaa viatu vyake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom