Uchumba kuvunjika ...kisa HARUSI

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
833
Wasalaam

Iko hivi ...Ni rafiki wa karibu wa familia yetu,ameajiriwa na taasisi ya fedha mwaka wa tatu huu Yuko kwenye mahusiano na mdada waliekutana chuo...Ni muda kiasi tunamuita shemeji yetu

Jamaa anataka kutoa mahari,lakini mwanamke amegoma anasema mpaka jamaa akubali sharti la kufanyika harusi

Familia ya jamaa yetu,Ni watu wenye uwezo wao kiasi,ila mzee wao Ni mtu wa kuchukia Sana Sherehe na harusi,anasema atachangia misiba na majanga mengine sio mambo ambayo mtu anayapanga mwenyewe halafu anasumbua watu kwa michango,ndivyo anavyishi

Dada za mshikaji wameozwa Tena kwa mahari ndogo,harusi hakuhudhuria,ila baada ya hapo aliwapa kiasi Fulani (kikubwa) Kama Cha kuanzia maisha,imekua utaratibu wake

Na mwaka Jana Kaka yake mshikaji kaoa kwa mtindo huo huo...alienda half day jmos...akatoka kuwaambia staff wenzie naenda funga ndoa ,hawakuamini,lakini jamaa alifunya ndoa,na home walikuja watu wachache tuu kwa ajili ya evening dinner

Jamaa anasema sio kuwa Hana uwezo,ila Ni namna Anaona atamhuzunisha mzee wake ..mzee wake kamwambia mikosi na mambo ya shetani huanzia kwenye tafrija/Sherehe...anasema Ni kujikweza...jamaa atanye Nini tukivaa viatu vyake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CarloJesus, Huyo mzee wake namkubali kwa 100%

Kuhangaika na sherehe za harusi Hakuna Maana Wala mantiki yoyote, Ni uupuzi tu kwangu!!

Hata Mimi nikifika hatua ya kuoa Basi sitahangaika na upuuzi wa sherehe

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
huyo mke hafai.. atakuja kumsumbua mbeleni..

wanawake wengi wenye tabia za kupenda harusi kubwa ni wapenda show offs na hata bikira huwa hawana maana waliipoteza kwenye show off za chips mayai ujanani

hapo anakomalia harusi ya gharama ili mashost na maex wake awakomeshe kwa photoshoots za harusi.. hawazi hata mtakula nini mbeleni
 
Mimi pia Sina mpango wa kufanya harusi, kama shemeji yenu ataendelea kukaza mwambie jamaa azame PM, tutasaini tu cheti altarini basi. Kwanza muda wa kukimbizana na kamati na kuomba michango Sina!
mimi pia mkuu sina mpango na harusi hizo me nataka mke tu ni pm twende altaren tu
 
Ukute mwenzie kasubiri ndoa na alikua anaipigia picha ndoa flani hiviii halafu Leo umwambie hamna sherehe weeeee.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ndoa hajakataliwa...mzee kasema Yupo radhi ifanyike hata jumuiyani nyumbani kwao,na habari ya chakula atasimamia kifamilia anavyojua yeye kama yeye,anajivuna atachinja hata ng'ombe

Ila Kama wanataka pia wanaweza kufunga wao peke yao bill watu wengi ye atafanya arrangements na paroko...anasema fahari Ni USHETANI na kujikweza na laana huanzia hapo kwa sababu muda huo Kuna wengi wanateseka,hataki hayo yamkute kijana wake,na jamaa Ni daddy's boy...mzee kafikia Hadi ku point ndoa kadhaa zilizovunjika Kama mfano hai kwa mshikaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo mke hafai.. atakuja kumsumbua mbeleni..

wanawake wengi wenye tabia za kupenda harusi kubwa ni wapenda show offs na hata bikira huwa hawana maana waliipoteza kwenye show off za chips mayai ujanani

hapo anakomalia harusi ya gharama ili mashost na maex wake awakomeshe kwa photoshoots za harusi.. hawazi hata mtakula nini mbeleni
Mkuu lakini si wote,Kuna wengine hili tuu ndo furaha yao...Kama wengine football,kahawa,kazi(workholic) nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom