Uchawi niliowahi kuushuhudia!

Kuna **** mmoja hapa jirani anapiga muziki utadhani ameazima radio,anakera mpaka basi.
"
Nikija kwenye mada,kiukweli uliposema uchawi wa Zongo umenikumbusha wakati nasoma kitabu cha Uchawi namna unavyokupata na kujikinga,kilichoandikwa na marehemu Munga Tehenan,najua Mtambuzi anakijua hiki kitabu.
"
Kwa mujibu wa marehemu Munga huo ulioutaja sio uchawi hasa bali ni nguvu ambazo mtu anazaliwa nazo na kuna wengine wanajua namna ya kuepuka kuwadhuru watu na nguvu hiyo kwa kuwa wanajua wanazo.Japokuwa wapo wanaozitumia kudhuru kwa kujua au kutokujua.
"
Lakini kumbuka kuwa ili ulogwe ni lazima uwe na wewe ni mchawi.Usishangae kwani wengi wetu ni wachawi either kwa kujua au kutokujua!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna uchawi. Ni imani za watu zimejenga hofu kuwa kuna kitu kinaitwa uchawi. Siamini uchawi.
 
Hata HIV-AIDS inasababisha ugonjwa uitwao AIDS dementia complex. Hii nayo ni mental illness.

Ndugu zangu wa karibu, wawili, nadhani walikuwa na huu ugonjwa. Lakini kuna baadhi ya ndugu walidai eti wamerogwa.

Yaani si Waafrika tuna matatizo sana. Nikifikiria ya akina Zitto na Saanane kwenda kula yamini kwa mganga ndiyo naishiwa na matumaini kabisa.

Piga picha eti Obama na Hilary nao wanaenda kwa waganga ili wapate kura zaidi :becky:
 
Hakuna uchawi. Ni imani za watu zimejenga hofu kuwa kuna kitu kinaitwa uchawi. Siamini uchawi.

Uchawi na dini kimsingi havina tofauti maana vyote msingi wake mkuu ni imani. Labda tofauti iliyopo ni kwenye application tu ingawa hii nayo yaweza kuwa debatable.

Uchawi mtu unaweza kusema lengo lake ni ubaya wakati dini/imani kwa mungu lengo lake ni wema/ uzuri.
 
Nakubaliana na wewe 100%
 
Nyani Ngabu kimsingi mambo ya uchawi hayawezi kuthibitishwa,lakini hii haimaanishi kuwa uchawi haupo.
"
Wazungu ni wachawi kuliko sisi,tena uchawi wao ni kiboko zaidi.Obama na Hillary ni wachawi sana.Uchawi wao ni black Magic ambao una asili ya Kabalah.Usidhani huko haupo.
"
Hata kuipata nafasi ya kuwa mgombea uraisi wa Marekani achilia mbali kuwa raisi,ni lazima uwe mchawi na unashiriki uchawi.
"
Tatizo tumeaminishwa Ulaya na Marekani hakuna uchawi na uchawi upo Africa tu,kuamini hivi ni jambo la ajabu sana.Hakuna jamii isiyokua na uchawi.Na uchawi ukifanyika kokote ni uchawi tu!
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahahahahahaha
Zinduna hapo kwenye kula alaf ana shiba mwingine umeniacha hoi sana!
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo Pacha Zinduna na Shostito gfsonwin mnakiri kbs kuwa Tanga ndo kumejaa Uchawi???????????????

Hawadanganyi maana hata mie nimekaa na kushuhudia sana ndumba na mambo kama hayo.
Nakumbuka shule ya msingi niliyokua nasoma(jina nalihifadhi) ipo karibu kabisa na baharini, pembezoni mwa barabara ya kwenda Mombasa. Wakati wa usiku ilikua inageuka kuwa treni...sasa ole wako upande,unaenda okotwa huko Lamu umechizika.
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenye Red nakubaliana na wewe, japo ipo Dini ambayo inaongoza kwa hayo Mambo ya Ulozi.
Hapo kwenye Green si imani pekee, Bali pia na Tamaduni au Kurithishana pia huchangia.
 

dah! nimecheka ile mbaya. pole sana mkuu. hii dunia we wacha tu-
 

Santeeeeeeee.............
 

sijui wachezaji wa mpira wa miguu wa sasa. lakini wale wa miaka 1975 - 1985 cha moto walikiona.
masuala ya kulala makaburini, kuogeshwa maji ya ajabu ajabu tulikuwa tukisema "maji ya maiti" n.k ndio ilikuwa mpango mzima. ukikataa na mechi hupangwi!
 
sijui wachezaji wa mpira wa miguu wa sasa. lakini wale wa miaka 1975 - 1985 cha moto walikiona.
masuala ya kulala makaburini, kuogeshwa maji ya ajabu ajabu tulikuwa tukisema "maji ya maiti" n.k ndio ilikuwa mpango mzima. ukikataa na mechi hupangwi!

yaani miaka ile, Acha tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…