Uchawi katika nyumba za kupanga

Uchawi katika nyumba za kupanga

Mi picha linaanza nlikua natafuta chumba cha elfu 40 single ajabu madalali wakanipeleka chumba cha elfu 20 full singboad tailiz had rangi nzur mno nyumba inawapngaji 5 pamoja na mm wa 6 nikaona hapa hapa pazur si kwa jeul nikalipia mwaka mmoja madalali walikua wawili nikawapa 20 20 sa cku nilivyoamia ote majirani wananiangalia kwa jicho la uruma na wengine wanatingisha kichwa nikajisemea moyoni ndio hawa wambea wambea ila tutaoneshana na hivi nilivyo single watafurai na show kumbe wenzangu walikua wananionea huruma sa kumaliza kupanga panga vizur mwenye nyumba akanijia ni bb mjane akaanza kunipa mashart ya hapa na pale kubwa zaid la zamu ya kufagia nikasema ntatoa hela ikifika zam yangu, uxk asa kufika uxk mda kama sa kumi hivi nikaota mtu kanikaaba kila nikikukurusana nae naishiwa nguuvu nikajua hapa nakufa nikajilegeza 2fasta nikashtuka ucngizin kuangalia uku na uku sikuona kitu nikahema kwanza nikawasha taa nikasema ngoja nisilale tena nikawasha tv nikaweka cd gafla nikaanza kusikia skuna kwenye korido kama kuna mtu anaenda anasimama nikajua atakua mpangaji 2 nikatulia mara ikaanza tena yan anaenda anafika mwisho anatulia alafu akiianza tena kama anaanzia pale pale uyu atakua kalewa nn ngoja nikamcheki gafla kufungua mlango nakuta kitu kama nguo hivi au upande wa mtu unamalizikizikia kuingia ndani na mlango ukifungwa nikajua labla mama mwenye nyumba alitoka nje c nikatoka nje nikojoe nikamuona paka mweusi kakaa ukutani tukatumbuliana macho mwili ukanisisimka balaa nikajikaza uku naenda uku tunaangaliana axa cha ajabu ile kubadilisha ndalapale chooni nageuka simwon na kuna ukuta mkubwa 2 nikais kaingia kwangu nikaanza kuungia ndani kwangu kwa tahadhali kuanza kumtafuta sijamuona nikapumua mara yule mtu akaanza kupita tena nikasema asaiv stok nje nikaongeza sauti ya tivi gafla kamsingizi kazur kakaanza kulegeza macho yangu nikasema sio kwel nikawai maji kunawa uso aikusaidia nikapitiwa asa nipo ndotoni nikajiona natoka nje kamakuna mtu ananielekeza kitu yule mtu simwoni vizur nikikaza macho kumuangalia vizur kama yule bb vile anacheka kwa kebehi hivi kile kicheko chake hadi nikastuka ndo ckulala tena ad asubh cha ajabu nilipo amka nje majirani ote wameaka wananiangalia nikawasalimia bado wananiangalia kwa jicho lile nusu niwaulize nikakausha nikaoga nikasepa zangu nakumbuka cku hiyo nilala oficn balaa usiku wake sasa cku hiyo mwe mwe mwe jamani kama yupo mtu aamin uchawi aanze kuamini 2 ckulala kabisa ni vitimbwii kwa kwenda mbele mara watu wanacheka kolidon mara wanatembea mara mtu anatwanga niliomba pakuche mbona
Wachaw ni wajinga sana wao Raha yao ni kutesa wenzako tu
 
Wachawi watu paka katumwa amini nakwambia mkuu
Macho ya binadamu ya vision cell mbili cones and rods ,cones inajihusisha na Kuona vizuri wakati wa mchana na rods zinasaidia wakati wa usiku ,paka hawana cones ndo maan mchana kutwa wanalala na popo mchana Huwa hawaoni vzr wao Wana rods zinazofanya kazi wakati wa usiku ,Huwa anatumika na wachaw unakuta Analia kama mtoto mchanga
 
Miaka tisa nyuma nilikuwa naishi Mbeya.
Basi kipindi hicho ndio nimeanza maisha hivyo kupatiwa apartment eneo la maghorofani jijini mbeya.

Si unajua mbanga za vijana, akija mgeni wako pale anatakiwa aandike anaenda kwa nani, kufanya nini na atakaa muda gani.

Yale maeneo ni karibia na chuo Cha Mzumbe, Grace college, CBE, Open university, Tia na SAUT mbeya.

Hivyo kubadilisha ikawa kawaida ila mkikosa kabisa, mnahamia Mwailubi ilikuja baadae, City lounge, Mbeya pazuri au sagura sagura Carnival.

Kelele zikaanza mpaka kijiweni pa kujitafutia ridhiki hivyo Mimi na wanangu tukashauriane tuhame.
Uzuri ukitoka kwenye premises Yao, kuna kahela kanaingia kanaitwa house allowance.

Mimi nikachugua gheto Veta ya kule juu chini ndio mnaita CCM.
Siku ya kwanza tu michanga chwaa,
Mbwa analia kichizi

Baada ya wiki, nikawa nikilala naota anakuja mtu ananiangalia ila nashindwa kufanya chochote

Hivyo nikaanza mikesha either nikiwa kwenye mambo yetuna minyau au kuangalia Tv gheto

Siku moja nikasema hili haiwezekani, nikasubiria usiku wa manane wakaja wengi.

Nikaamka kitandani nikamlenga mmoja, nikamtia kichwa,
Kumbe nikapiga kwenye pembe ya chumba, huku ikitoka sauti kama bom limelipuka.

Kuja kushtuka damu zinatoka na nundu la kutosha.
Kufika kijiweni naamriwa nirudi kwenye makazi rasmi na niwe na Dem mmoja.

Haya mambo haya yasikie tu, wale wanangu waliludishwa kila mmoja na namna yake.

Wa mwisho Dem wa kisangu kutoka mbarali alitaka kuondoka na mavuzi yake bila hivyo amuoe 🤣🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😂😂😂😂
 
Nakumbuka katika harakati za kutafuta maisha nikajikuta niko Mbeya soko matola kwenye nyumba moja ya bibi anaitwa binti wa kuchinja,hilo jina lina maana yake
Basi nikapata fremu ya duka,kabla ya yote nikaenda kumsimulia shangazi yangu kama nimepata fremu sehemu inatwa hilo jina,mwenyeji wangu alimind sana akaniambia yule bibi ni mchawi mkubwa watu wengi wanafilisika, kwa hiyo ile fremu ya duka ilikuwa inaogopwa kupangishwa na wenyeji,wakati huo mimi nilikuwa nimetokea Iringa gangilonga uzunguni kabisa
Basi nikaingia naye mkataba kwa kupitia wajukuu zake maana yeye alikuwa mzee sana. NI mnene,mweusi,ngozi imebabuka na midomo myekundu huwa wanasema sababu ya kula nyama za watu,
Nikasafisha duka nikatia mzigo,maana ilikuwa miaka 1995,

kisa kinanza tuko na braza wangu tumelala usiku nikaota nimetumbukizwa kwenye kaburi,halafu ndani ya kaburi kuna joka kubwa jeusi,ile kuangukia ndani ya shimo nikawa nimeanguka kimgongo,nilipiga kelele za nguvu sijawahi kupiga vile,hakuna aliyetoka wala kuja kuuliza kuna nini? Hatukulala usiku mzima tunaogopa
Cha maajabu bibi alikuja kuwa rafiki yangu mkubwa kila kitu kikitokea utasikia mkamuite Marasta,maana nilikuwa na dread miaka hiyo, Nikafanikiwa kimaisha kupitia duka nikapiga hela ndefu sana,badaye nikahamia dar kufungua biashara kubwa
Nzuri ila kuna kitu umeruka hapa mzee wetu. Urafiki ulianzaje maana mchawi hana rafiki.
 
Yaani kuazia nyumba ya kwanza mpaka ya mwisho kila unapoulizia, hamna baba,alishakufa wamebaki wa bibi na wa mama,kumbe walishauwa wame zao,salute sokomatora
Wanawake wengi wa kinyakyusa Mbeya wanaishi bila waume. Ni wanawake watata sana, waume zao wanakufa kwa manyanyaso ukiacha hao wachawi
 
Mm nilihamia nyumba moja asubuhi yake wakaninyoa kiduku halafu wakanipaka na breech,eeh kesho yake wakaninyoa kipara wakanipaka na mafuta,nikaone eeh siku ya tatu yatatokea makubwa na mafuta Tena nikahama
Kaliwa mtu hahaha
 
Inafikia wakati naanza kuogopa watanzania wote maana ukisikia neno uchawi apo ujue tanzania wala nigeria inausika😓
Bongo noma Nigeria movie, mi kuna house nilihamia aisee, mother house nikawa naota anakuja ananishika kifua kama tufanye sex, nakurupuka. Lakini miguso naiskia kabisa yenyewe. Baadae ile hali imeisha. Ila ni mkarimu sana na mkubwa kwangu..gap lipo ila anajipenda. Na mimi huwa namsifia akipendeza, akiwa kanuna nawajibika kumchekesha, mpaka ananiona kama ndugu.....Somtimes watu wana vimbwanga vyao tu.

Ila kitu nimejifunza unatakiwa ujue miiko ya watu na kuangalia namna usiwaudhi udhi watu wana ujuzi wa ajabu sana
 
Bongo noma Nigeria movie, mi kuna house nilihamia aisee, mother house nikawa naota anakuja ananishika kifua kama tufanye sex, nakurupuka. Lakini miguso naiskia kabisa yenyewe. Baadae ile hali imeisha. Ila ni mkarimu sana na mkubwa kwangu..gap lipo ila anajipenda. Na mimi huwa namsifia akipendeza, akiwa kanuna nawajibika kumchekesha, mpaka ananiona kama ndugu.....Somtimes watu wana vimbwanga vyao tu.

Ila kitu nimejifunza unatakiwa ujue miiko ya watu na kuangalia namna usiwaudhi udhi watu wana ujuzi wa ajabu sana
Aiseeee
 
Back
Top Bottom