Uchawi haupo, ni imani tu

Uchawi haupo, ni imani tu

Nitumie majina yako halisi matatu,na ya wazazi wako uone nitakachokufanyia
 
Alafu kuna mtu Kwa uchache wake wa kutambua nini maana ya Mapepo, ,
Anasema mapepo ni uchawi
Mapepo ni neno la kiswahili( majini)
Wapo majini wabaya na wapo majini wazuri
hii nayo ni mada kubwa
Wakristo wote duniani wanaamini mapepo( majini wote ni mashetwan
Awajui ya kwamba shetwan ni sifa sio kiumbe..
Nini tofauti kati ya Mapepo na Majini?
 
Tatizo hapa mtoa mada ni mlokole
Anaingiza iman yake ya DINI katika neno uchawi ,,,
Uchawi ni neno lenye tafsiri pana
Hata paulo mtume wa Kristo Yesu aliitwa mchawi kwa sbb alikuwa anacheza na nyoka katika moto na nyoka awakuungua
Watu wakamuita Paulo ni mchawi
Mimi siyo Mlokole,lkn sitaki kuwa mtumwa wa hiari wa Imani za ajabu ajabu.Ukimwamini Mungu yote yanawezekana.
 
Nnachoona tunatofautiana kwa kuwa hujui maana ya imani.

Kwa kuwa umemtaja Mungu, tuende na Yeye.

Soma hapa:-

Mambo ya Walawi 19:31 inasema: "Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao ..
Mambo ya Walawi 20:6 inasema: "Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.
Kumbukumbu la Torati 18:12 inasema kwamba kuwasiliana na pepo wala mchawi wa wafu ni "chukizo."

Ufunuo wa Yohana 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

IKIWA MUNGU ANASEMA UCHAWI UPO, WEWE UNAPATA WAPI AUDACITY YA KUPINGANA NA MUNGU KWAMBA UCHAWI HAUPO?
Mkuu naona hukunielewa bado,Nimesema hivi Uchawi haupo kwa mwenyewe, isipokuwa mindsets zetu ndio zinafanya Uchawi uonekane kuwa upo.
 
Kwa


Soma habar ya mussa, uchawi upo na utaendelea kuwepo.
Nani kakwambia kwamba fimbo ya mussa siku ile ilimaliza wachawi wote?
Iman thabiti, husaidia kuwa kinga na tiba ya mambo ya kichawi.
Ila usishangae, siku moja ukija sikia/ambiwa/shuhudia kuwa hata Padri wako, Baba au Mama mchungaji wako, paroko wako, au Askofu wako ni Mchawi.
Kuna wachawi ukiambiwa huyu ni mchawi, unaweza bisha. Kutokana na status zao kwenye jamii.
Madhara ya kuamini sana uchawi, ni jamii kuwa jinga na maskini.
Indicator mojawapo ya jamii inayothamini sana uchawi ni uwepo kwa umaskini wa kutupa.

#Mshana Jr. anaweza toa maelezo ya ziada hapa.
U
Nashukuru kwa kutambua madhara ya Uchawi.Kuhusu watu wenye vyeo kanisani kuhusika na Uchawi,wewe isikuchanganye,Hao ni binadamu tu,Wewe mtazame Yesu Kristo Msulibiwa huyo ndiye Role model wako.
 
Heshima zenu mabibi na mabwana...!!!!,Kuna hii hoja ya Uchawi kuwa upo,lkn mimi nasema hivi Uchawi haupo,kilichopo ni Imani tu za ushirikina ambazo kimsingi hujengwa tu ktk akili ya mtu,yaani mind set.Sasa unabisha??.Tuliza kimukhe mukhe nikupe mambo wewe.

Nakwambiaje Uchawi haupo ila ubongo wako tu ulivyouset. Ni sawa na kuamini kuwa wewe huna akili,nakwambia itakuwa hivyo hivyo.Sasa unataka kujua hoja yangu imelala wapi? Hebu nisimulie matukio yafuatayo uone jinsi ambavyo Uchawi haupo kabisa.

Mwaka 2009,nilikuwa Rukwa,kwaajili ya Field ya muda mrefu ktk Wilaya ya Nkasi,kutokana na muda kuwa mrefu nikalima mahindi ekari moja,Kabla ya kupanda mama mwenye nyumba (nilipopanga)akanishauri kuwa anipe dawa ya kienyeji ili niichanganye na mbegu ili kuweka ulinzi dhidi ya Chuma ulete au wakupaji wa mazao,nikakataa nikasema shamba langu litalindwa na damu ya Yesu,akanicheka sana lkn kwenye mavuno nikamzidi.

Mwezi mmoja baadaye niliamuru ng'ombe mzima afukiwe (Km Afisa kilimo na mifugo)kwasababu hakuwa anafaa kuliwa,wazee wakanifata wakanisii sana kuwa nisifanye hivyo kwa ujumla kamati nzima ya Serikali ya kijiji walinifuata nikawakatalia,yule mwenye ng'ombe alilia sana na alikuwa mzee,wakasema watafanya yao,lkn sikutishika.

Nakwambia hadi leo hakuna jambo lolote baya la kipekee lililonipata.Sasa kuna sababu gani ya mimi kuamini uchawi??.Ni upuuzi tu.

Nilipoajiriwa,nilikwenda Ngara,huko nikajishughulisha na kilimo cha Maharage,Nyanya na Mpunga,jamaa mmoja tuliyekuwa tunalima naye alikuwa anaogopeka kijijini pale kuwa ni bonge la chuma ulete,baba yake aliogopwa na wakazi wa pale kwa uchawi wa kila namna,jamaa yule akanishawishi kuwa anipe dawa niichanganye na mbegu ili kuzuia chuma ulete aka wakupaji wa mazao,huyu naye nikamtolea nje,nilimwambia mimi siogopi kitu,mbegu zangu nitazipeleka tu Kanisani kwaajili ya Baraka ya Padre,hiyo dawa aitumie yeye mwenyewe,nakwambia ktk mavuno nilikuwa nampiga gepu kubwa sana kwa eneo linalofanana ukubwa,jamaa akaniambia aisee,wewe jamaa una Imani kubwa!!!!,Mimi nilimsihi kumwamini Mungu na kutumia utaalamu ktk kilimo wala haina haja ya kuhangaika na dawa za kienyeji,ni kupoteza muda tu.

Siku nyingine kuna mama mmoja alishikwa na Mapepo km Kiongozi wa jumuiya nikaenda na wenzangu kumuombea,Jamaa mwingine(hakuwa Mkristo)aliyeamini sana ktk uchawi,alikuja na dawa kwaajili ya kumsaidia yule mama,lkn akiwa anakuja alikamatwa na mapepo yaliyotoka kwa yule mama yakampiga sana hadi jamaa akazirai,yakisema unaenda wapi?,wewe hutuwezi tulikuwa tunatafuta kwa kwenda sasa tumepata,wakati huo sisi tunaendelea na maombi,kwa hiyo mapepo yamemtoka mgonjwa na kumqingia yule jamaa aliyeamini uchawi.

Ndugu zangu Nina shuhuda nyingi za kutosha kusema kuwa "UCHAWI HAUPO" ila ni jinsi ulivyoiseti halmashauri ya Ubongo wako.Nakumbuka siku za nyuma kuna jamaa hapa JF aliwahi kusema "ikiwa kuna mtu anayejua kuroga amroge,akaleta mrejesho kuwa hakuna aliyejitikeza kumroga", Kumbe uchawi haupo ni fikra zetu tu.

HITIMISHO.
Ukimwamini Yesu na nguvu zake huna sababu ya kuhofu na kudhani kuwa UCHAWI upo,Kuamini uchawi ni matokeo ya kutokuwa na Imani kwa Mungu aishiye milele.Uchawi una madhara mengi ktk jamii sina haja ya kuyataja maana yaliyotokea Shinyanga kila mmoja ni shahidi,Uchawi unasababisha watu wasifanye maendeleo,na hatari zaidi kuliko yote,Uchawi unafanya watu kuwahusu binadamu wenzao ambao wanawadhani kuwa wachawi.Km kweli kuna MTU ni Mchawi humu JF aniroge mimi tuone.
uchaw upo
 
Baraka za Mungu haziondolewi na kitu chochote isipokuwa mtu mwenyewe aliyezipokea atakapokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu hapo ndipo Baraka za Mungu zinaondoka.Uchawi hauna ngebe hizo.
Kama unaamini kuna mwanga basi lazima giza pia liwepo
 
Back
Top Bottom