Uchawi haupo, ni imani tu

Uchawi haupo, ni imani tu

Hijalishi unaamini au vipi, kwani wale wasioamini kwamba Mungu yupo inafanya asiwepo? Imani yako haijakamilika kama huamini kazi za shetani zipo na ndio huo uchawi na mabaya mengine mengi.
Msumamo wangu ni huu kwamba,Uchawi haupo kwa wenyewe bali upo ktk akili za watu, hivyo uwepo wake unategemea akili za watu (mind set).
 
Kama unataka uamini uchawi upo pata utajiri! Ukipata utajiri na ukawa huna msimamo wowote kiroho yaani nuru/giza ukawa vuguvugu tu lazima uondoke/ufe chap! Ni either Yesu awe Mungu na mwokozi wa maisha yako haswahaswa au uwe na mganga wako ndipo utasurvive!
Fatilia utaona, kaa na watu waliofanikiwa kimaisha hata ambao si matajiri sana utagundua!
Matajiri wengi wako vizuri Sana kiroho,siyo blabla tu
Nimeshafanya biashara za kusafirisha mazao nje ya nchi,wafanyabiashara wenzangu (baadhi)walikuwa wakichukia kwasababu ya ushindani,lkn sijawahi kumbwa na chochote.Ndio maana naendelea kupigilia msumari kuwa Uchawi haupo ila mawazo yetu tu.
 
Nimeshafanya biashara za kusafirisha mazao nje ya nchi,wafanyabiashara wenzangu (baadhi)walikuwa wakichukia kwasababu ya ushindani,lkn sijawahi kumbwa na chochote.Ndio maana naendelea kupigilia msumari kuwa Uchawi haupo ila mawazo yetu tu.
Bado unasafirisha? Ulikuwa na mtaji kiasi gani? Inawezekana ulitakiwa uwe mbali Sana na Hiyo biashara lakini, uchawi unaweza kukufanya mediocre
 
Kuna Dada mmoja alipangwa kazi ya ualimu katika moja ya wilaya za mkoa wa Rukwa. Siku moja asubuhi akajikuta (akajipata)amelala ziwani.
Aliondoka bila kuaga.
Kutokuamini hakufanyi kitu kisiwepo.
Nashangaa zaidi unapoonesha kumwamini Mungu (ambaye hujawahi kumwona), uliyemjua kupitia Biblia, ambayo imetaja Mara nyingi wachawi. Je unaipinga biblia?
 
Heshima zenu mabibi na mabwana...!!!!,Kuna hii hoja ya Uchawi kuwa upo,lkn mimi nasema hivi Uchawi haupo,kilichopo ni Imani tu za ushirikina ambazo kimsingi hujengwa tu ktk akili ya mtu,yaani mind set.Sasa unabisha??.Tuliza kimukhe mukhe nikupe mambo wewe.

Nakwambiaje Uchawi haupo ila ubongo wako tu ulivyouset. Ni sawa na kuamini kuwa wewe huna akili,nakwambia itakuwa hivyo hivyo.Sasa unataka kujua hoja yangu imelala wapi? Hebu nisimulie matukio yafuatayo uone jinsi ambavyo Uchawi haupo kabisa.

Mwaka 2009,nilikuwa Rukwa,kwaajili ya Field ya muda mrefu ktk Wilaya ya Nkasi,kutokana na muda kuwa mrefu nikalima mahindi ekari moja,Kabla ya kupanda mama mwenye nyumba (nilipopanga)akanishauri kuwa anipe dawa ya kienyeji ili niichanganye na mbegu ili kuweka ulinzi dhidi ya Chuma ulete au wakupaji wa mazao,nikakataa nikasema shamba langu litalindwa na damu ya Yesu,akanicheka sana lkn kwenye mavuno nikamzidi.

Mwezi mmoja baadaye niliamuru ng'ombe mzima afukiwe (Km Afisa kilimo na mifugo)kwasababu hakuwa anafaa kuliwa,wazee wakanifata wakanisii sana kuwa nisifanye hivyo kwa ujumla kamati nzima ya Serikali ya kijiji walinifuata nikawakatalia,yule mwenye ng'ombe alilia sana na alikuwa mzee,wakasema watafanya yao,lkn sikutishika.

Nakwambia hadi leo hakuna jambo lolote baya la kipekee lililonipata.Sasa kuna sababu gani ya mimi kuamini uchawi??.Ni upuuzi tu.

Nilipoajiriwa,nilikwenda Ngara,huko nikajishughulisha na kilimo cha Maharage,Nyanya na Mpunga,jamaa mmoja tuliyekuwa tunalima naye alikuwa anaogopeka kijijini pale kuwa ni bonge la chuma ulete,baba yake aliogopwa na wakazi wa pale kwa uchawi wa kila namna,jamaa yule akanishawishi kuwa anipe dawa niichanganye na mbegu ili kuzuia chuma ulete aka wakupaji wa mazao,huyu naye nikamtolea nje,nilimwambia mimi siogopi kitu,mbegu zangu nitazipeleka tu Kanisani kwaajili ya Baraka ya Padre,hiyo dawa aitumie yeye mwenyewe,nakwambia ktk mavuno nilikuwa nampiga gepu kubwa sana kwa eneo linalofanana ukubwa,jamaa akaniambia aisee,wewe jamaa una Imani kubwa!!!!,Mimi nilimsihi kumwamini Mungu na kutumia utaalamu ktk kilimo wala haina haja ya kuhangaika na dawa za kienyeji,ni kupoteza muda tu.

Siku nyingine kuna mama mmoja alishikwa na Mapepo km Kiongozi wa jumuiya nikaenda na wenzangu kumuombea,Jamaa mwingine(hakuwa Mkristo)aliyeamini sana ktk uchawi,alikuja na dawa kwaajili ya kumsaidia yule mama,lkn akiwa anakuja alikamatwa na mapepo yaliyotoka kwa yule mama yakampiga sana hadi jamaa akazirai,yakisema unaenda wapi?,wewe hutuwezi tulikuwa tunatafuta kwa kwenda sasa tumepata,wakati huo sisi tunaendelea na maombi,kwa hiyo mapepo yamemtoka mgonjwa na kumqingia yule jamaa aliyeamini uchawi.

Ndugu zangu Nina shuhuda nyingi za kutosha kusema kuwa "UCHAWI HAUPO" ila ni jinsi ulivyoiseti halmashauri ya Ubongo wako.Nakumbuka siku za nyuma kuna jamaa hapa JF aliwahi kusema "ikiwa kuna mtu anayejua kuroga amroge,akaleta mrejesho kuwa hakuna aliyejitikeza kumroga", Kumbe uchawi haupo ni fikra zetu tu.

HITIMISHO.
Ukimwamini Yesu na nguvu zake huna sababu ya kuhofu na kudhani kuwa UCHAWI upo,Kuamini uchawi ni matokeo ya kutokuwa na Imani kwa Mungu aishiye milele.Uchawi una madhara mengi ktk jamii sina haja ya kuyataja maana yaliyotokea Shinyanga kila mmoja ni shahidi,Uchawi unasababisha watu wasifanye maendeleo,na hatari zaidi kuliko yote,Uchawi unafanya watu kuwahusu binadamu wenzao ambao wanawadhani kuwa wachawi.Km kweli kuna MTU ni Mchawi humu JF aniroge mimi tuone.
Biblia ina kili uchawi upo wewe pangu pa kavu unaleta story za kutunga juu ya uongo wako huo?


Kwamba imani ikutume kua nimenyolewa nywele kichawi na unakuta nywele hakuna sio?
 
Miujiza iliyofanywa na Musa huwezi kusema kuwa ni uchawi,bali ilifanyika kwa nguvu ya Mungu.Na lengo hapo ni kuonyesha kuwa Mungu ni mwenye nguvu.Siku nyingine usirudie tena kuiita miujiza ya Mungu ni uchawi.
Ni uchache wako tu wa kuelewa uchawi na miujiza ni kitu kimoja
Nabii Musa alifanya kafara ya kuchinja mbuzi usiku kisha akaichukua damu ile ya mbuzi akaipaka katika milango ya nyumba za wamisri
Kuamka asubuhi kila nyumba ya mwana wa Misri alikufa mtoto wa kwanza kuzaliwa
Nambie nabii Musa alifanya uchawi au miujiza ?
Na usitafsiri uchawi kwa akili zako
Uchawi ni tecnorojia ya kiswahili
Mfano kufunga mvua, kupaa na ungo iwe usiku au mchana , kutembea juu ya maji, kukaa ndani ya mtungi hiyo ni sayansi tu ndio uchawi wenyewe. Sio mbaka mtu akirogwa ndio uitwe uchawi.
 
Niroge nisiipende JF,maana muda mwingi nautumia kuchat JF badala ya kufanya mambo ya msingi km vile Kusali,Kufanya kilimo,n.k.


Urogwe ufe??, kwasababu ukifa hautotokea tena ndani ya jf, sasa kubali au kataa.---- sisi hatutanii na wala usimlaumu mtu kwa hili, wewe si unapinga juu ya uchawi wakati unasoma Biblia ambamo kuna wachawi wa Pharaoh wametajwa.
 
Ni kweli yameongelewa lkn hiyo haimaanishi kuwa tujenge imani hapo.Ktk Biblia mambo mazuri na mabaya yote yamezungumzwa,halikadhalika watu wema na wabaya.Sasa ni kazi kwako kufahamu Mungu anakutaka uelekee upande upi?.
Unaamini uchawi haupo, kwanini uweke kwenye matendo, wakati haupo.
Kwakua umekili uchawi, umeandikwa ndani ya Bibilia, unayoiamini, je hivyo, Bibilia imeandika mambo mengine ambayo hayapo?
 
Hivi mapepo hayaingii kwenye kundi la uchawi?
Linaingia sema tu haijui Bibilia vizuri, angepinga uwepo wa Uchawi bila kuitaja dini, nisingepingana nae, ila Dini hata hiyo anayoiamini inatambua uchawi upo, na Kinga yake ni Yesu.
Hivyo kukataa kwake ni kuipinga Bibilia
Angalie hizo picha alafu aweke coment.
Screenshot_20200930-230048_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20200930-230109_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20200930-230122_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20200930-230143_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20200930-230230_Opera%20Mini.jpg
 
Acha uutani wewe uchawi upoo na unazuri
 
Urogwe ufe??, kwasababu ukifa hautotokea tena ndani ya jf, sasa kubali au kataa.---- sisi hatutanii na wala usimlaumu mtu kwa hili, wewe si unapinga juu ya uchawi wakati unasoma Biblia ambamo kuna wachawi wa Pharaoh wametajwa.
Fanya hivyo mkuu tuone.Uone moto wa Yesu ulivyo na nguvu.
 
Ni uchache wako tu wa kuelewa uchawi na miujiza ni kitu kimoja
Nabii Musa alifanya kafara ya kuchinja mbuzi usiku kisha akaichukua damu ile ya mbuzi akaipaka katika milango ya nyumba za wamisri
Kuamka asubuhi kila nyumba ya mwana wa Misri alikufa mtoto wa kwanza kuzaliwa
Nambie nabii Musa alifanya uchawi au miujiza ?
Na usitafsiri uchawi kwa akili zako
Uchawi ni tecnorojia ya kiswahili
Mfano kufunga mvua, kupaa na ungo iwe usiku au mchana , kutembea juu ya maji, kukaa ndani ya mtungi hiyo ni sayansi tu ndio uchawi wenyewe. Sio mbaka mtu akirogwa ndio uitwe uchawi.
Mkuu mambo yanayofanywa na nguvu ya mkono wa Mungu huwezi kusema ni uchawi,huko ni kumtukana Mungu,nakusihi usiingie ktk mkumbo huo.
 
Kabla sijasoma khadithi yako ya kitoto, nikueleze uchawi upo mwanangu...kama hayajakukuta shukuru Mungu.
Jichawi,wewe ni mchawi?,hebu nionyeshe Uchawi wako kwa kuniroga kwanza.Niroge utakavyo,sikuchagulii.
 
Sasa wewe umaamini Yesu wa nini sasa kama hamna uchawi? Hata yeye hakuna haja ya kumuamini kwa sababu anaamini mapepo na majini yapo na ndio uchawi wenyewe.
 
Back
Top Bottom