Wahaya wanavaa kanzu kama sehemu ya utamaduni wao. Watu wengi wa Middle East wanavaa kanzu bila kujali dini zao. Hata Yesu alivaa kanzu. Waislamu wetu wengi wanachanganya utamaduni wa kiarabu na uislamu. Siku hizi wanavaa mpaka Keffiyeh kama ishara ya uislamu.
Majority misikitini wanakuwa wanavaa nguo za kawaida tu.
Wanavaa kuiga utamaduni wa wazanzibari. Na baadhi kweli wanavaa kwa sababu mfiwa ni muislamu. Wanawake wengi wanavaa mitandio wakienda kutoa pole kwa waislamu wenzao. Ni ishara ya heshima tu na sio kosa. Hata Nyerere alivaa sana Balaghashia ambao wengi waliiona kama kofia ya waislamu.
Wasingevaa maana pasingekuwa na haja. Jamii yetu inaishi kwa heshimu tamaduni za wenzetu. Ndio maana wakristu wakitaka kuchinja wanamtafuta Abdallah awachinjie. Kufanya hivyo sio uchawa kwa waislamu bali heshima.
Hivi karibuni nimewaona Boni na Sugu wakiwa na virasta. Nao tuseme wanafanya hivyo kwa sababu ya uchawa?
Amandla...