Father of All
JF-Expert Member
- May 30, 2026
- 214
- 310
Taratibu, ule, msimamo kuwa nchi haina dini ila watu wake wana dini unaanza kumomonyolewa tena na wale usiowategemea. Naona kama Zenj, taratibu, inaanza kuwa taifa la kiislam. Ni bahati mbaya na hasara kiasi gani. Nilidhani msomi kama Daktari Mwinyi asingekuwa hovyo hivi. Ama kweli, elimu ya mja haiondoi upumbavu wa mhusika. Je, tungoje na Tanzania nzima kuwa taifa la kiislam? Je, hatua hii haivunji muungano japo ushavunjika zamani kwa kukosa maana na mantiki? Zaidi ya hitajio la kuvunja huu muungano wa kinafiki na kinyonyaji, nini kifanyike kuunusuru kama kweli unapaswa kunusuliwa? Je, kwa uchawa, ukihiyo na uzwazwa uliopo, kuna mtanzania mwenye uwezo wa kukemea na kukomesha udini na uhafidhina huu uchwara? Je, na Bara ikitangaza kuwa ni taifa la kibantu lenye dini asilia kinzani na hizi nyemelezi na za kitumwa, itakuwaje? Je inawezekana wakati huu chini ya huyu expert?