Ni hali halisi. Kanzu ni nguo iliyokuwa na inayoendelea kuvaliwa sana Middle East na North Africa. Na huko kote wakristu na waislamu wakiarabu wanavaa kanzu. Wayahudi hawavai kwa sababu ni wahamiaji na wamerudi na tamaduni za walikotoka.
Mtanzania wa kawaida ana amini "Salaam Aleykhum" ni salamu ya kiislamu wakati ni " amani iwe kwako " kwa kiarabu.
Hata kwenye harusi za kihaya, wageni wengi hawavai kanzu. Ni vazi la kitamaduni lakini halitumiki sana.
Inawezekana. Lakini wanakosea kama vile siku hizi wanavyosalimia " As salam Aleykhum" pamoja na "Bwana Asifiwe" ambayo nayo inachukuliwa kama salam ya kikristu. Kwangu mimi sioni tatizo kwa wao kuvaa kanzu hata kama ni kwa ajili ya kuheshimu imani yake. Ni heshima tu, sio uchawa.
Ubaya wa hili jambo ni kuwa watu wanataka kuhusisha Mbowe kuvaa kanzu na unafik. Hiyo ni quite low.
Amandla....
..kusema Mbowe ni mnafiki kwasababu amevaa kanzu sio sawa.
..lakini hatutakosea tukisema Mbowe amevaa kanzu kwa nia ya kuheshimu dini ya KIISLAMU kwasababu kanzu ni vazi la dini hiyo.